290 Mpango wa Mungu Haujawahi Kubadilika

1 Sijafanya mabadiliko yoyote katika mpango Wangu tangu uanzishwe. Ni kwamba tu, kwa binadamu, wale ambao kwao Mimi huelekeza maneno Yangu wanaonekana kupungua kwa idadi, sawa na wale Ninaowakubali kwa kweli. Hata hivyo, Ninasisitiza kwamba mpango Wangu haujawahi kubadilika; badala yake, ni imani na upendo wa mwanadamu ambavyo hubadilika daima, kufifia daima, kiasi kwamba kuna uwezekano wa kila mwanadamu kubadilika kutoka kujipendekeza Kwangu hadi kufikia hali ya kunidharau au hata kunitupa nje.

2 Mtazamo Wangu kwenu hautakuwa baridi wala moto, hadi pale Nitakapohisi kuchukizwa na karaha, na hatimaye kutoa adhabu. Hata hivyo, katika siku ya adhabu yenu, bado Nitawaona lakini nyinyi hamtaweza kuniona tena. Kwa kuwa maisha miongoni mwenu yameshakuwa ya kuchosha na ya taabuKwangu, basi, ni wazi kwamba Nimechagua mazingira tofauti ya kuishi, afadhali kuepuka kuumizwa na maneno yenu maovu na kuwa mbali na tabia zenu mbovu kwa namna isiyovumilika, ili msinipumbaze au kunitendea kwa namna ya uzembe tena. Kabla Sijawaacha, lazima bado Ninawasihi mjiepushe kufanya yale ambayo hayaambatani na ukweli. Badala yake, mnafaa kufanya kile ambacho kinawapendeza wote, kile kilicho na manufaa kwa wote, na kile kinachofaidi hatima yenu wenyewe, la sivyo, yule anayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe.

Umetoholewa kutoka katika “Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 289 Mungu Apitia Shida za Binadamu

Inayofuata: 291 Nani Awezaye Kumjua Mungu Ajapo?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp