961 Siku ya Adhabu ya Mungu kwa Mwanadamu Imewadia

1 Watu wengi huhisi kusumbuka na kuona haya kwa sababu wametenda makosa mabaya, na wengi wanajionea aibu kwa sababu hawajawahi kutenda tendo lolote zuri. Tena wapo pia wengi ambao, mbali na kutahayari kwa ajili ya dhambi zao, wanakuwa wabaya zaidi, wakiitoa kabisa barakoa inayoficha sura zao mbaya—ambayo haikuwa bado imewekwa wazi kikamilifu—ili kujaribu tabia Yangu. Sijali, wala sitilii maanani yoyote matendo ya mtu yeyote. Badala yake, Mimi hufanya kazi Ninayopaswa kufanya, iwe kukusanya habari, kuzunguka katika nchi au kufanya jambo ambalo linanipendeza. Katika nyakati muhimu, Mimi huendelea na kazi Yangu miongoni mwa wanadamu kama ilivyopangwa awali, bila kuchelewa au kuwa mapema hata kidogo, na kwa urahisi na kwa makini.

2 Hata hivyo, katika kila hatua ya kazi Yanu, watu wengine wanawekwa pembeni, kwa sababu Ninadharau hali yao ya kujipendekeza na hali yao ya kujifanya wanyenyekevu. Wale wanaonichukiza sana hakika watatelekezwa, iwe ni kwa kupenda au kwa kutopenda. Kwa ufupi, Ningependa wale wote Ninaowadharau wawe mbali sana Nami. Ni dhahiri kwamba, Sitawahurumia wale waovu ambao wamebaki katika nyumba Yangu. Kwa kuwa siku ya adhabu ya mwanadamu inakaribia, Sina haraka ya kuzitupa nje zile nafsi zote zinazostahili dharau kutoka katika nyumba Yangu, kwa kuwa Nina mpango Wangu mwenyewe.

Umetoholewa kutoka katika “Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 960 Jinsi ya Kutoikosea Tabia ya Mungu

Inayofuata: 962 Tabia ya Mungu Yenye Haki Haistahimili Kosa Lolote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp