102 Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Zimemwokoa Mwanadamu Kabisa

1 Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika hatua tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hatua hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, yaani, ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu ambao wamepotoshwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati uo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani. Hivyo, kama kazi ya wokovu ilivyogawanywa katika hatua tatu, kwa hivyo pia vita dhidi ya Shetani vimegawanywa katika hatua tatu, na vipengele hivi viwili vya kazi ya Mungu vinafanywa sawia. Vita dhidi ya Shetani kwa kweli ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na kwa kuwa kazi ya wokovu wa wanadamu silo jambo linaloweza kukamilishwa kwa mafanikio katika hatua moja, vita dhidi ya Shetani pia vimegawanywa katika hatua na vipindi, na vita vinapiganwa dhidi ya Shetani kulingana na mahitaji ya mwanadamu na kiwango cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani.

2 Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, hatua tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika hatua tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizwa kupitia kwa hatua kadhaa za kazi: kumpa mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu akamilishwe. Kusema ukweli, vita na Shetani hajiandai kupigana na Shetani, bali ni wokovu wa mwanadamu, kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kubadilishwa kwa tabia ya mwanadamu ili kwamba aweze kumshuhudia Mungu. Hivi ndivyo Shetani anashindwa. Shetani anashindwa kwa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Wakati Shetani ameshindwa, yaani, wakati mwanadamu ameokolewa kabisa, basi Shetani aliyeaibika atafungwa kabisa, na kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa.

3 Na kwa hivyo, kiini cha wokovu wa mwanadamu ni vita dhidi ya Shetani, na vita na Shetani vitajitokeza kimsingi katika wokovu wa mwanadamu. Hatua ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni hatua ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, na baada ya hapo kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.

Umetoholewa kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 101 Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

Inayofuata: 103 Kazi ya Kumsimamia Mwanadamu ni Kazi ya Kumshinda Shetani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp