978 Onyo la Mungu kwa Mwanadamu

1 Nina matamanio mengi. Natamani muweze kutenda kwa njia inayofaa na yenye mwenendo mzuri, muwe waaminifu kutimiza wajibu wenu, muwe na ukweli na ubinadamu, muwe watu ambao wanaweza kuacha vitu vyote na kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu, na mengineyo. Matumaini haya yote yanatokana na upungufu wenu na upotovu na kutotii kwenu. Kwanza, fanya uchunguzi wa dhambi zako zote, na kuchunguza mwenendo na mawazo yako yote ambayo hayafuati ukweli. Ninatumai kwamba hamtalicheka hitaji hili kwa siri, au hata zaidi, kwamba hamtaliangalia kwa dharau au kulichukulia kimzaha. Lichukulieni kwa umakini, na msilipuuze.

2 Pili, kwa kila moja ya dhambi na kutotii kwako tafuta ukweli unaoambatana na utumie ukweli huu kuzitatua, kisha badilisha vitendo vyako vya dhambi na mawazo yako na vitendo vya kutotii na kutenda ukweli. Tatu, kuwa mtu mwaminifu, si mtu ambaye siku zote anakuwa mjanja, mwenye hila daima. (Hapa Ninakusihi tena uwe mtu mwaminifu.) Kama unaweza kutimiza vipengee hivi vyote vitatu basi una bahati, wewe ni mtu ambaye ndoto zake zinatimia na ambaye hupata bahati nzuri. Kwa vyovyote vile, azma Yangu ni kutimiza ndoto zenu, kuweka mawazo yenu katika matendo, si kuwadhihaki au kuwadanganya.

3 Hivyo Mimi nawaambia sasa kwa uzito kabisa: Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kusifiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile ambacho Nimedai, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe. Yafuteni hayo mawazo na hesabu zenu zote mapema iwezekanavyo, na muanze kuyachukulia madai Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote wawe majivu ili Niitamatishe kazi Yangu. Kwa sababu Siwezi kuwaleta katika ufalme Wangu maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani, katika enzi ijayo.

Umetoholewa kutoka katika “Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 977 Unapaswa Kutafuta Kukubaliwa na Mungu

Inayofuata: 979 Kile Afikiriacho Mungu Kuhusu Matendo ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp