315 Njia Za Mungu Haziwezi Kueleweka

I

Tunaona uadhama Wako unaopanda juu ya mbingu.

Hatutakuja mbele Yako kamwe bila heshima.

Nani anaweza kujua mapenzi Yako, nani anaweza kuthubutu kuhisi hasira Yako?

Nani anatamani uadhama Wako, utakuja lini?

Hapa tunalala, tumeshikwa mikononi Mwako,

tukifurahia upendo Wako kama ule wa mama,

ingawa ghadabu Yako inatufanya kuogopa.

Eh, Wewe ni mama tunayemwabudu,

baba tunayempenda na kumheshimu.

Mioyo yetu inajificha kutoka Kwako, lakini hatuthubutu kwenda mbali.

Na eh, mioyoni mwetu tunakuhisi Wewe ukiwa karibu,

tunakuhisi Wewe karibu sana.

Bila kujua tunahisi Wewe huwezi kueleweka.

Eh, kisha tunaweza tu kukuheshima kwa umbali.

Eh, tunaweza tu kwa kukuheshimu kwa umbali tu.

II

Mioyo yetu inakupenda lakini bado tunakuogopa

maneno yana maana gani?

Upendo wa binadamu utawezaje kueleza hisia kama hizi?

Yote tuwezavyo kufanya ni kuja mbele Yako na mikono mitupu,

na kukuomba Wewe tu, kama mtoto na wenye uoga.

Unatutolea kila hitaji letu, chochote kile.

Sifa isiyokoma inainuka juu kutoka kwa mioyo yetu inanayofurahi.

Eh, bila uchoyo Wewe umetoa yote, hakuna madai hakuna malalamishi.

Kwa nadra sana tunauona uso Wako, ilhali tumepata Yako yote.

Eh, sisi wenyewe tuna uchafu mwingi sana ndani yetu,

lakini Umeshapata nafsi yetu yote kitambo sana.

Eh, macho ya kimwili yatawezaje kuona ukweli uliokamilishwa kutoka zamani,

eh, ukweli ambao Wewe umekamilisha kutoka siku za zamani?

III

Kutoka wakati wa zamani, mwisho mmoja wa dunia hadi mwingine,

vitu vyote vimefichuliwa machoni Mwako.

Tunakuwa kimya, hakuna anayethubutu kujifananisha na Wewe.

Kwa muda wote neno Lako linaendelea kutiririka bila mwisho.

Na jinsi gani utajiri Wako ni mkubwa, hakuna anayeweza kusema.

Nani anayethubutu kusifu uzuri Wako kwa maneno rahisi?

Na nani anathubutu kuimba kwa urahisi kuhusu unyenyekevu Wako?

Eh, dakika moja Uko mbali na sisi, kisha katikati yetu,

mbali, kisha unaegemea karibu, sasa mbali, sasa karibu.

Eh, hakuna ambaye ameona nyayo Zako kamwe, ama kuona kivuli Chako.

Kumbukumbu ya furaha tu ndiyo ambayo imebaki kwetu.

Eh, tamu tamu sana ladha ambayo inaendelea zaidi na zaidi.

Eh, ladha ya uwepo Wako ni tamu ambayo unaendelea kuwepo.

IV

Ya milele kama mbingu, dunia,

nani anayejua mwelekeo wa matendo Yako?

Tunaona tu chembe moja katika ufuo wa changarawe,

kwa upole tukingoja katika mamlaka Yako.

Wanyenyekevu kama mchwa,

tunawezaje kujifananisha na Wewe uliyeinuliwa juu?

Eh, kutusafisha Kwako kumejawa, kumejawa na huruma.

Tunaona haki Yako imefichwa katika huruma Yako, eh,

eh, haki iliyofichwa ndani ya uadhama Wako takatifu,

tunaiona imefichwa katika upendo Wako na katika matendo Yako.

Eh, nani anaweza kuyahesabu matendo Yako, ni mengi zaidi.

Eh, nani anaweza kuyahesabu, ni mengi sana.

Eh, nani anaweza kuyahesabu matendo Yako, ni mengi zaidi.

Eh, nani anaweza kuyahesabu, ni mengi sana.

Iliyotangulia: 314 Nampenda Mungu Sana

Inayofuata: 316 Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki