145 Hekima ya Mungu Huja Mbele Kulingana na Njama za Shetani

1 Haikujalisha ni vipi ambavyo binadamu walizidi kupotoka au vipi nyoka alivyowajaribu, Yehova bado alikuwa na hekima Yake; kwa hivyo, Amekuwa Akijihusisha katika kazi mpya tangu Alipouumba ulimwengu, na hamna hatua zozote za kazi hii zimewahi kurudiwa. Shetani ameendelea kutekeleza njama zake; binadamu wamekuwa wakipotoshwa siku zote na Shetani, na Yehova Mungu pia ameendelea kutekeleza kazi Yake ya hekima siku zote. Hajawahi kushindwa, na Hajawahi kusita kufanya kazi Yake kuanzia uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa. Kwa kufanya kazi hii yote, Hajaruhusu tu binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia amewaruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atawaruhusu binadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu waovu na kuwatuza wema.

2 Amepambana na Shetani hadi siku hii ya leo na Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake hutumika kutokana na njama za Shetani. Na kwa hivyo mbali na kufanya tu kila kitu mbinguni kitii mamlaka Yake; pia Hufanya kila kitu duniani kipumzike chini ya kigonda Chake na pia, Huwafanya wale waovu wanaoshambulia na kunyanyasa binadamu wajipate katika kuadibu Kwake. Matokeo yote ya kazi yanaletwa kutokana na hekima Yake. Ni katika muda huu tu ndipo kila kitu kule mbinguni na duniani huweza kushuhudia hekima ya Mungu, uweza Wake, na hasa uhalisi wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 144 Umuhimu wa Jina la Mungu

Inayofuata: 146 Jina la Mungu Linatukuzwa Kati ya Mataifa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp