471 Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele

1 Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele. Mimi Ndiye msambazaji wa binadamu na kiongozi wa pekee wa mwanadamu. Thamani na maana ya maneno Yangu haibainishwi na kama yanakubaliwa au kutambuliwa na mwanadamu, ila ni kwa kiini cha maneno yenyewe. Hata kama hakuna mtu hata mmoja duniani anaweza kupokea maneno Yangu, thamani ya maneno Yangu na usaidizi wake kwa mwanadamu hayapimiki na mwanadamu yeyote.

2 Kwa hivyo, Ninapokumbwa na wanadamu wengi wanaoasi, kukataa au kudharau kabisa maneno Yangu, msimamo Wangu ni huu tu: Wacha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai. Wacha vionyeshe kuwa yote Niliyosema ni ya ukweli, na kuwa ni yale ambayo mwanadamu lazima apewe, na, zaidi ya yote, yale ambayo mwanadamu anafaa akubali.

3 Nitawaruhusu wote wanaonifuata wajue ukweli huu: Wote wasioyakubali maneno Yangu kikamilifu, wale wasioyaweka maneno Yangu katika vitendo, wale wasiopata sababu ndani ya maneno Yangu, na wale wasiopata wokovu kwa sababu ya maneno Yangu, ni wale ambao wamehukumiwa na maneno Yangu na, zaidi ya hayo, wamepoteza wokovu Wangu, na fimbo Yangu haitaondoka kamwe miongoni mwao. Wacha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai.

Umetoholewa kutoka katika “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 470 Maneno ya Mungu: Kanuni Pekee ya Kuwepo kwa Mwanadamu

Inayofuata: 472 Ukweli Ni Methali ya Juu Zaidi ya Maisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp