512 Ni Msingi wa Maneno ya Mungu tu Unaotoa Njia ya Kutenda

1 Kwa kufuatilia ukweli tu ndipo mtu anaweza kutimiza mabadiliko katika tabia: Hili ni jambo ambalo watu wanafaa kufahamu na kulielewa vizuri kabisa. Usipokuwa na ufahamu wa kutosha wa ukweli, utateleza kwa urahisi na kupotoka. Ukitaka kukua katika maisha, lazima utafute ukweli katika kila kitu. Haijalishi kile unachokifanya, unapaswa utafute njia ya kutenda iliulingane na ukweli na utambue dosari zilizo ndani yako zinazoukiuka. Haijalishi kile unachokifanya, unapaswa kuzingatia iwapo kina thamani au la. Unaweza kufanya mambo yaliyo na maana, lakini lazima usifanye mambo yasiyo na maana. Kuhusu mambo ambayo ungeweza kuyafanya ama kutoyafanya, iwapo yanaweza kuachiliwa, basi yafaa uyaachilie. Vinginevyo, ukifanya mambo haya kwa muda fulani na baadaye utambue kwamba unapaswa uyaachilie, basi fanya uamuzi upesi na uyaachilie haraka. Hii ndiyo kanuni unayofaa kuifuata katika kila kitu unachofanya.

2 Wakati wa kutafuta kuingia, kila jambo lazima lichunguzwe. Mambo yote lazima yatafakiriwe kulingana na neno la Mungu na ukweli ili ujue jinsi ya kuyashughulikia kwa njia ambayo inalingana kikamilifu na mapenzi ya Mungu. Mambo yanayotokea kutoka kwa mapenzi yako kisha yanaweza kuachwa. Utajua jinsi ya kufanya mambo kulingana na mapenzi ya Mungu na basi utaenda uyafanye; itahisi kana kwamba kila kitu kinafuata mkondo wake, na itaonekana ikiwa rahisi kabisa. Hivi ndivyo watu walio na ukweli hufanya mambo. Kisha unaweza kuonyesha wengine kuwa tabia yako imebadilika, na wataona kuwa kwa hakika umetenda matendo mazuri, kwamba unafanya mambo kulingana na kanuni, na kwmba unafanya kila kitu sawa. Huyu ni mtu anayeelewa ukweli, na ambaye kwa kweli ana mfano fulani wa ubinadamu. Kwa hakika kabisa, neno la Mungu limevuna matokeo kwa watu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 511 Mshuhudie Mungu Katika Vitu Vyote ili Umridhisha Mungu

Inayofuata: 513 Tafuta Ukweli Katika Kila Kitu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp