136 Kazi ya Mungu Haisimami

1 Madhumuni ya Mungu mara zote ni kuona kazi Yake ikiwa mpya na hai, si kongwe na iliyokufa, na kile Anachotaka mwanadamu ashikilie kwa nguvu kinabadilika kulingana na enzi na kipindi, na si cha kudumu milele na kisichobadilika. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu ambaye husababisha mwanadamu kuishi na kuwa mpya, tofauti na ibilisi anayemsababishia mwanadamu kufa na kuwa mzee. Je, bado hamlielewi hili? Una dhana kuhusu Mungu na umeshindwa kuziacha kwa kuwa hutafakari. Si kwa sababu kuna maana kidogo sana ndani ya kazi ya Mungu, wala kwa sababu kazi ya Mungu inatofautiana na matakwa ya binadamu, wala kwamba Mungu mara zote ni “mzembe katika wajibu Wake.” Huwezi kuacha dhana zako kwa kuwa umepungukiwa na utiifu, na huna sifa hata kidogo za kiumbe wa Mungu, na si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu. Yote haya umejisababishia na hayana uhusiano na Mungu; mateso na misukosuko yote husababishwa na mwanadamu.

2 Dhamira za Mungu mara zote huwa nzuri: hakusudii kukufanya uzitoe dhana, ila angependa ubadilike na uwe mpya kadiri enzi zinavyopita. Ila bado huwezi kutofautisha chokaa na jibini na kila mara ama unachunguza au unachanganua. Si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu, ila ni kuwa humheshimu Mungu na uasi wako umezidi. Kiumbe mdogo anathubutu kuchukua sehemu ndogo ya kile alichopewa mwanzo na Mungu, na kisha kubadilika na kukitumia kumvamia Mungu—je, huu si uasi wa mwanadamu? Ni haki kusema kuwa binadamu hawana sifa kabisa za kutoa maoni yao mbele za Mungu, na sembuse hawana sifa za kuonyesha hadharani maneno yao yasiyo na thamani, yanukayo, yaliyooza wapendavyo—bila kutaja chochote kuhusu hizo fikira zilizooza. Haina maana?

Umetoholewa kutoka katika “Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 135 Kazi ya Mungu ni Mpya Daima na si Nzee Kamwe

Inayofuata: 137 Kazi Yote ya Mungu ni ya Vitendo Kabisa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp