89 Kazi ya Mungu Inatimizwa Kupitia Maneno

1 Iwapo, baada ya kipindi cha uzoefu, wewe unaweza kujua kazi inayofanywa na Mungu na kila hatua ya kazi ya Mungu, na unao ufahamu mkuu wa malengo ya maneno ya Mungu, na ni kwa nini maneno mengi yaliyozungumzwa na Yeye hayajatimika bado, basi unaweza kutulia na kuendelea katika safari iliyo mbele yako, ukiwa huru kutokana na wasiwasi na kusafishwa. Mnapaswa kuona kile Mungu anatumia wingi wa kazi Yake. Yeye hutumia maneno Anayozungumza, akimsafisha mwanadamu na kuyabadilisha mawazo ya mwanadamu kupitia maneno mengi tofauti.

2 Mateso yote ambayo mmestahimili, kusafishwa kote ambako mmepitia, kushughulikiwa ambako mmekukubali ndani yenu, kupata nuru ambako mmeona—yote yamefanikishwa kutumia maneno Aliyozungumza Mungu. Ni kwa sababu ya nini ndio mwanadamu anamfuata Mungu. Ni kwa sababu ya maneno ya Mungu! Maneno ya Mungu ni yenye mafumbo makuu, na yanaweza kuuguza moyo wa mwanadamu, kufunua vitu vilivyo ndani ya moyo wa mwanadamu, yanaweza kumfanya ajue vitu vilivyotendeka zamani, na kumruhusu kuona katika siku za usoni.

3 Na kwa hivyo mwanadamu anavumilia mateso kwa sababu ya maneno ya Mungu, na anafanywa mkamilifu kwa sababu ya maneno ya Mungu, na ni baada ya hapo tu ndipo mwanadamu anamfuata Mungu. Anachostahili kufanya mwanadamu katika hatua hii ni kukubali maneno ya Mungu, na haijalishi kama amefanywa mkamilifu, au kusafishwa, kilicho cha muhimu ni maneno ya Mungu; hii ni kazi ya Mungu, na ni maono ambayo mwanadamu lazima ayajue leo hii.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 88 Mungu Mwenye Mwili Katika Siku za Mwisho Anafanya Kazi Zaidi Kutumia Maneno

Inayofuata: 90 Neno la Mungu ni Mamlaka na Hukumu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp