878 Kila Hatua ya Kazi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Uzima wa Mwanadamu

1 Mungu amefanyika kuwa mwili wakati huu kufanya kazi hii, kukamilisha kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kuifunga enzi hii, kuihukumu enzi hii, kuwaokoa waliozama kabisa dhambini kutoka katika ulimwengu wa bahari ya mateso na kuwabadilisha kabisa. Mungu amevumilia sana kulala bila kupata usingizi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi kupitisha siku Zake na mwanadamu, hajawahi kulalamikia uchakavu walionao wanadamu, hajawahi kumlaumu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha Yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na Aliingia mwenyewe “jahanamu” na “kuzimu,” katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu amestahili vipi kumpinga Mungu? Ana sababu gani tena ya kumlaumu Mungu? Anawezaje kuwa na ujasiri wa kumwangalia Mungu tena?

2 Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung’uniko au malalamiko Yake kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi na ukandamizaji wa mwanadamu. Kamwe Hajawahi kujibu matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, hajawahi kutaka mambo mengi yanayomuelemea mwanadamu, na hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi ambazo mwanadamu alitakiwa kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia mwanga, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni hatua gani Alizozichukua ambazo si kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haijakuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso haya na kunyanyaswa na nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye mapenzi? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu wenye shauku?

Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 877 Mungu Huvumilia Aibu Kubwa Kuwaokoa Wanadamu

Inayofuata: 879 Ni Mungu tu Ampendaye Mwanadamu Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp