946 Hasira ya Mungu ni Onyesho la Tabia Yake ya Haki

1 Ingawaje kumwagwa kwa hasira ya Mungu ni dhana ya maonyesho ya tabia ya haki Yake, hasira ya Mungu kwa vyovyote vile haibagui walengwa wake au haina kanuni. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu si mwepesi wa ghadhabu, wala Hakimbilii kufichua hasira Yake na adhama Yake. Aidha, hasira ya Mungu inadhibitiwa na kupimwa kwa kiwango fulani; hailinganishwi kamwe na namna ambavyo binadamu atakavyowaka kwa hasira kali au kutoa ghadhabu zake. Kushushwa kwa hasira ya Mungu si kwa vyovyote vile maonyesho au hali ya kutoa nje hali Yake ya moyo. Hasira ya Mungu si mlipuko mkubwa wa hasira kali kama vile binadamu anavyoielewa. Mungu hawachilii hasira Yake kwa sababu hawezi kuidhibiti hali ya moyo Wake binafsi au kwa sababu ghadhabu Yake imefikia kilele na lazima itolewe. Kinyume cha mambo ni kwamba, hasira Yake ni maonyesho ya tabia ya haki Yake na maonyesho halisi ya tabia ya haki Yake; ni ufunuo wa ishara ya hali Yake halisi takatifu.

2 Mungu ni hasira, asiyevumilia kosa—hivi si kusema kwamba ghadhabu ya Mungu haitofautishi sababu za kufanya hivyo au haifuati kanuni; ni binadamu uliopotoka ambao unafuata mkondo wa kipekee wa kutokuwa na kanuni, mlipuko wa hasira kali bila mpango usiotofautisha hali hii miongoni mwa sababu mbalimbali. Binadamu atalipuka kwa ghadhabu na kutoa nje hisia zake ili kutetea na kushikilia uwepo wa dhambi, na matendo haya ndiyo njia ambayo kwayo binadamu anaonyesha kutotosheka kwake; yamejaa dosari, mifumo na mbinu mbalimbali, kupotoka na maovu ya binadamu, na zaidi ya chochote kingine, yanajaa kwa malengo na matamanio ya binadamu. Wakati haki inaposhindana na maovu, binadamu hataruka juu kwa ghadhabu ili kutetea uwepo wa haki; kinyume ni kwamba, wakati nguvu za haki zinatishwa, zinateswa na kushambuliwa, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutotilia maanani, kukwepa, au kushtuka. Hata hivyo, wakati anapokabiliwa na nguvu za maovu, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutunza, na kunyenyekea mno. Hivyo basi, kutoa nje ghadhabu kwa binadamu ni kimbilio la nguvu za maovu, maonyesho ya mwenendo wa maovu uliokithiri na usiositishwa wa binadamu wa kimwili.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 945 Ishara ya Hasira ya Mungu

Inayofuata: 947 Onyo la Maangamizi ya Mungu ya Sodoma kwa Wanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp