875 Umuhimu wa Kupata Mwili kwa Mungu ili Ateseke kwa Niaba ya Mwanadamu

1 Mungu anapata mwili ili ateseke kwa niaba ya mwanadamu, na kwa kufanya hivyo atasababisha hatima iliyo ya ajabu ambayo itafuata kwa ajili ya mwanadamu. Hatua hiyo ya kazi iliyokamilishwa na Yesu ilikuwa tu kuwa Kwake mfano wa mwili wenye dhambi na kusulubiwa, kuhudumu Kwake kama sadaka ya dhambi na kuwakomboa wanadamu wote, na hii iliweka msingi wa kuingia kwa baadaye kwa mwanadamu katika hatima iliyo ya ajabu. Alizichukua dhambi zote za mwanadamu juu Yake na akawa mfano wa mwili wenye dhambi na akasulubiwa; Alisulubiwa kwa niaba ya wanadamu wote, na baada ya hapo wanadamu wote walikombolewa. Alitumia kusulibiwa Kwake na damu Yake ya thamani kuwakomboa wanadamu. Damu Yake ya thamani ilitumiwa kama sadaka ya dhambi, kumaanisha kwamba ilitumiwa kama ushuhuda kwamba mwanadamu anaweza kuwa bila dhambi na anaweza hatimaye kuja mbele za Mungu: Ilikuwa ni njia ya kumgeuzia Shetani mashambulizi katika vita dhidi ya Shetani.

2 Sasa katika hatua hii, Mungu atakamilisha kazi Yake na kuifanya enzi nzee kufika tamati. Atawaleta wale kati ya wanadamu walioachwa katika hatima yao iliyo ya ajabu. Hivyo Mungu kwa mara nyingine tena amekuwa mwili na, kama pamoja na kumshinda mwanadamu, Amekuja kustahimili mateso fulani kwa niaba ya mwanadamu ili kwamba mateso yao hatimaye yataondolewa kutoka kwao. Mateso yote ya mwanadamu yataondolewa kutoka kwao kwa njia ya ushuhuda, tendo hili, ambalo ni Mungu kujishuhudia Mwenyewe na kutumia ushuhuda huu na kushuhudia huku kumwangamiza Shetani, kumuaibisha ibilisi, na kuufichua hatima ya ajabu ya mwanadamu.

3 Kupata mwili kumekuja kufanya kazi Yake na kupitia uchungu wa dunia. Ni muhimu kwamba Mungu afanye kazi hii, na ni muhimu sana, kwa mwanadamu na kwa hatima ya baadaye ya mwanadamu. Yote ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, kwa ajili ya kupatikana kwa mwanadamu—matendo haya yanafanywa na juhudi hii inagharimika kwa sababu ya hatima wa ajabu wa mwanadamu. Baada ya kupitia kwa uchungu duniani kumrejesha mwanadamu, Shetani hatakuwa na mshiko tena kwa mwanadamu na mwanadamu atamgeukia Mungu kikamilifu. Hili tu ndilo linaloweza kuitwa binadamu kumilikiwa na Mungu kikamilifu.

Umetoholewa kutoka katika “Umuhimu wa Mungu Kuuonja Mateso ya Dunia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 874 Kila Kitu Ambacho Mungu Humfanyia Mwanadamu Ni Cha Kweli

Inayofuata: 876 Mungu Kupitia Maumivu ya Mwanadamu ni kwa Maana Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp