140 Mungu Huchukua Majina Tofauti Kuwakilisha Enzi Tofauti

1 Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima Atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha kipengele cha wakati cha tabia ya Mungu katika enzi fulani; yote linahitaji kufanya ni kuwakilisha kazi Yake.

2 Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima. Bila kujali iwapo ni enzi ya Yehova, au ni enzi ya Yesu, kila enzi inawakilishwa kwa jina. Baada ya Enzi ya Neema, enzi ya mwisho imewadia na Yesu Amekwisha kuja. Itakuwaje awe bado anaitwa Yesu? Itakuwaje awe bado anachukua umbo la Yesu miongoni mwa watu? Je, umesahau kuwa Yesu Alikuwa tu mkombozi wa wanadamu? Itakuwaje achukue kazi ya kushinda na kurekebisha mwanadamu katika siku za mwisho?

3 Katika siku za mwisho, mwanadamu ameshuka kwenye kiasi hicho cha upotovu mpaka kazi ya hatua hii inaweza kutelezwa tu kupitia hukumu na kuadibu. Ni kwa njia hii tu ndiyo kazi inaweza kufanikishwa. Hii imekuwa kazi ya enzi kadhaa. Kwa maneno mengine, Mungu hutumia jina Lake, kazi Yake, na taswira tofauti za Mungu kugawanya na kuhamisha enzi; jina la Mungu na kazi Yake vinawakilisha enzi Yake na kuwakilisha kazi Yake katika kila enzi. Kwa hivyo, kazi ambayo Mungu hufanya katika kila enzi, jina ambalo Yeye huitwa, na mfano ambao Yeye hutwaa—kazi ambayo Yeye hufanya katika kila hatua mpaka leo—hivi havifuati kanuni hata moja, na hayakabiliwi na kikwazo chochote.

Yeye ni Yehova lakini pia ni Yesu, na vile vile ni Masihi, na Mwenyezi Mungu. Kazi yake inaweza kubadilika polepole, na kuna mabadiliko sambamba katika jina lake. Hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Yeye kikamilifu, lakini majina yote ambayo Yeye huitwa yanaweza kumwakilisha Yeye, na kazi ambayo Amefanya katika kila enzi inawakilisha tabia yake.

Umetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 139 Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Inayofuata: 141 Tabia ya Mungu Inaonekana Katika Kila Hatua ya Kazi Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp