881 Mungu Apitia Maumivu Makubwa Kumwokoa Mwanadamu
1 Mungu alikuwa mwili na Amefanya kazi kwa miaka kadhaa na Amesema mambo yasiyoweza kuhesabika. Mungu anaanza kwa kutoa hukumu ya wafanya huduma, na baadaye Husema unabii na Huanza kazi ya hukumu na kurudi, kisha Hutumia kifo kuwatakasa watu. Baada ya hapo, Huwaongoza watu katika njia sahihi ya kumwamini Mungu, Akizungumza na kuwapatia watu ukweli wote na kupambana na dhana mbalimbali za mwanadamu. Baadaye, Humpatia mwanadamu tumaini dogo kumruhusu kuona kuna tumaini mbele yake; yaani, Mungu na watu wanaingia katika mwisho mzuri wa safari kwa pamoja.
2 Ingawa kazi hii inafanywa kulingana na mipango ya Mungu, yote inafanywa kulingana na mahitaji ya binadamu. Haifanywi kiholela na Yeye; Hutumia hekima Yake kufanya kazi yote hii. Kwa kuwa ana upendo, Anaweza kutumia hekima na kwa bidii kushughulika na watu hawa walioharibika. Hachezi na watu hata kidogo. Hebu angalia toni ya sauti na namna ya kutamka maneno katika maneno ya Mungu; wakati fulani inawapatia watu majaribu, wakati fulani maneno Yake huwafanya watu kutahayari, wakati fulani huwapatia watu maneno ambayo huwaokoa na hufanya wawe watulivu. Kwa kweli Anawafikiria sana na kuwajali watu.
3 Ingawa watu ni viumbe wa Mungu, na wote wamepata uharibifu kutoka kwa Shetani, na ingawa watu hawana thamani, ni wazururaji, na asili zao ziko namna hii, Hashughuliki na watu kulingana na hulka zao, na Hashughuliki nao kulingana na adhabu ambayo wangestahili kuipata. Ingawa maneno Yake ni makali, siku zote Anashughulika na watu kwa ustahimilivu, uvumilivu, na huruma. Tafakari hili kwa taratibu na kwa makini! Ikiwa Mungu hakushughulika na watu kwa uvumilivu, huruma na neema, je, Angeweza kusema mambo haya yote ili kuwaokoa watu?
Umetoholewa kutoka katika “Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo