852 Mungu Humtendea Mwanadamu kama Mpendwa Wake Mkuu

Mungu aliwaumba wanadamu; licha ya kama wamepotoka au kama wanamfuata Yeye, Mungu hushughulikia binadamu kama wapendwa Wake wanaothaminiwa zaidi—au kama vile binadamu wangesema, watu walio wapenzi Wake sana—na wala si kama vikaragosi Wake.

1 Ingawaje Mungu anasema Yeye ndiye muumba na kwamba binadamu ni uumbaji Wake, hali ambayo inaweza kuonekana ni kana kwamba kuna tofauti kiasi katika mpangilio wa cheo, uhalisia ni kwamba kila kitu ambacho Mungu amefanya kwa mwanadamu kinazidi kabisa uhusiano wa asili hii. Mungu anampenda mwanadamu, anamtunza mwanadamu, na anaonyesha kwamba anamjali mwanadamu, pamoja na kumkimu mwanadamu bila kuacha na bila ya kusita. Kamwe hahisi katika moyo Wake kwamba hii ni kazi ya ziada au ni kitu kinachostahili sifa nyingi.

2 Wala Hahisi kwamba kuokoa binadamu, kuwatosheleza, na kuwapatia kila kitu, ni kutoa mchango mkuu kwa binadamu. Anamkimu tu mwanadamu kimyakimya na kwa unyamavu, kwa njia Yake mwenyewe na kupitia kwa kiini Chake na kile Anacho na alicho. Haijalishi ni toleo kiasi kipi na ni msaada kiasi kipi ambao wanadamu wanapokea kutoka kwa Yeye, Mungu siku zote hajawahi kufikiri kuhusu au kujaribu kutaka sifa yoyote. Hii inaamuliwa na kiini cha Mungu, na pia hasa ni maonyesho ya kweli pia ya tabia ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 851 Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

Inayofuata: 853 Utunzi Kamili Wa Mungu Juu Ya Yote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp