68 Mungu Anataka Kumwokoa Mwanadamu kwa Kiasi Kikubwa Mno Iwezekanavyo

I

Wakati wa kazi ya Mungu ya wokovu,

Atawaokoa wale wote Anaoweza kuwaokoa

kwa kiasi kikubwa mno iwezekanavyo, na Hatamwacha yeyote.

Lakini wale wote wasioweza kubadilisha tabia yao,

au kumtii Mungu kabisa watakuwa walengwa wa adhabu.

Wote ambao wanakubali kushinda kwa maneno

watakuwa na nafasi nyingi za wokovu.

Wokovu wa Mungu utawaonyesha

huruma Yake kubwa sana na uvumilivu.

Watu wakirudi kutoka kwa njia mbaya,

wakitubu, Mungu atawapa fursa kupata wokovu Wake.

II

Hatua hii ya kazi, kazi ya maneno, inafungua tu kwa watu

njia zote na mafumbo ambayo hawayaelewi.

Hili humsaidia mwanadamu kuyajua mapenzi ya Mungu

na matakwa ya Mungu kwa mwanadamu.

Kwa hiyo wanaweza kutenda maneno ya Mungu

na kubadilisha tabia yao.

Wote ambao wanakubali kushinda kwa maneno

watakuwa na nafasi nyingi za wokovu.

Wokovu wa Mungu utawaonyesha

huruma Yake kubwa sana na uvumilivu.

Watu wakirudi kutoka kwa njia mbaya,

wakitubu, Mungu atawapa fursa kupata wokovu Wake.

III

Mungu anatumia maneno tu kufanya kazi Yake.

Huwa hawaadhibu watu kwa sababu ya uasi wao mdogo,

kwani sasa ni wakati wa wokovu.

Wote wanaoasi wangeadhibiwa,

hakuna ambaye angekuwa na fursa ya kuokolewa.

Wote wangeadhibiwa na wangeanguka Kuzimu.

Maneno yanayomhukumu mwanadamu humruhusu

kujijua na kumtii Mungu,

si kwa yeye kuadhibiwa kwa hukumu ya maneno haya.

Wote ambao wanakubali kushinda kwa maneno

watakuwa na nafasi nyingi za wokovu.

Wokovu wa Mungu utawaonyesha

huruma Yake kubwa sana na uvumilivu.

Watu wakirudi kutoka kwa njia mbaya,

wakitubu, Mungu atawapa fursa kupata wokovu Wake.

IV

Watu wanapomwasi Mungu kwanza,

Yeye hana shauku ya kuwaua,

lakini badala yake Yeye hufanya analoweza kuwaokoa.

Kama mtu hana nafasi ya wokovu, Mungu atamtelekeza.

Hana haraka ya kuadhibu kwani Anataka kuwaokoa

wote ambao wanaweza kuokolewa.

Wote ambao wanakubali kushinda kwa maneno

watakuwa na nafasi nyingi za wokovu.

Wokovu wa Mungu utawaonyesha

huruma Yake kubwa sana na uvumilivu.

Watu wakirudi kutoka kwa njia mbaya,

wakitubu, Mungu atawapa fursa kupata wokovu Wake.


Yeye huwahukumu, huwatia nuru,

huwaongoza watu Akitumia maneno tu,

sio kuwapiga kwa fimbo.

Kutumia maneno kuokoa ndilo kusudi,

maana ya hatua hii ya mwisho ya kazi.

Umetoholewa kutoka katika “Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu Kuleta Wokovu kwa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 67 Mungu Anautafuta Moyo Wako na Roho Yako

Inayofuata: 69 Kuwa Mtu Anayekubali Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki