454 Roho Mtakatifu Afanya Kazi Zaidi kwa Wale Wanaotamani Kukamilishwa

1 Kwa hiyo sasa mnapaswa kufuatilia mabadiliko katika tabia yenu ya maisha ili muwe kweli thibitisho la Mungu kupata utukufu kupitia kwa kazi Yake katika siku za baadaye, na kufanywa kuwa vielelezo vya kazi Yake ya siku za baadaye. Kazi yote ya leo inaweka msingi kwa ajili ya kazi ya siku za baadaye; ni kwa wewe kutumiwa na Mungu na ili uweze kuwa na ushuhuda Wake. Ikiwa hii ni chombo cha kazi yako, utaweza kupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Kadri chombo cha kazi yako kilivyo juu, ndivyo itawezekana kwako wewe kukamilishwa zaidi. Kadri unavyofuatilia ukweli, ndivyo Roho Mtakatifu atafanya kazi zaidi. Kadri unavyokuwa na nguvu zaidi kwa kazi, ndivyo utakavyopata zaidi. Roho Mtakatifu huwakamilisha watu kulingana na hali yao ya ndani. Ukilenga moyo wako katika kufuatilia lengo moja, Mungu bila shaka atakukamilisha. Hii ni njia ya Roho Mtakatifu. Njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu inapatikana kupitia kwa kutafuta kwa watu.

2 Kadri unavyotamani kukamilishwa na kupatwa na Mungu, ndivyo Roho Mtakatifu atafanya kazi zaidi ndani yako. Kadri usivyotafuta, na kadri unavyokuwa mbaya na kukimbia, ndivyo zaidi Roho Mtakatifu anakosa nafasi za kufanya kazi. Roho Mtakatifu atakuacha polepole. Mnapaswa kufuatilia kufanya kila kitu kwa ajili ya kukamilishwa, kupatwa, na kutumiwa na Mungu, kuruhusu kila kitu katika ulimwengu kuona matendo ya Mungu yakifichuliwa ndani yenu. Miongoni mwa mambo yote, nyinyi ni watawala wa hayo, na miongoni mwa yote yaliyopo, mtamruhusu Mungu kupata ushuhuda Wake na utukufu Wake kwa sababu yenu—hii inaonyesha kwamba nyinyi ni kizazi kilichobarikiwa zaidi.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 453 Kazi ya Roho Mtakatifu ina Kanuni Zake

Inayofuata: 455 Mungu Awakamilisha Wale Walio na Kazi ya Roho Mtakatifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp