5 Mwili Mtakatifu wa Kiroho wa Mwenyezi Mungu Umeonekana

1

Mwenyezi Mungu amefichua mwili Wake mtukufu hadharani.

Mwili Wake mtakatifu umeonekana; ni Mungu Mwenyewe: Mungu hasa wa Kweli.

Dunia yote imebadilik, mwili pia umebadilika.

Kubadilishwa Kwake kwa umbo ni nafsi ya Mungu, taji la dhahabu juu ya kichwa Chake,

vazi jeupe juu ya mwili Wake, mkanda wa dhahabu kifuani Mwake.

Kila kitu duniani ni kiti cha miguu Yake, macho Yake ni kama miale ya moto,

upanga wenye makali kuwili mdomoni Mwake, nyota saba katika mkono Wake wa kulia.

Njia ya ufalme inang’aa na isiyo na mipaka, utukufu wa Mungu unainuka na kung’aa.

Milima inashangilia na maji kufurahia; jua, mwezi na nyota vyote vinazunguka

Katika mpangilio wao taratibu, ikimkaribisha Mungu mmoja wa kweli,

ambaye ametimiza mpango wa usimamizi wa miaka 6,000 kwa ushindi!

2

Wote wanacheza na kuruka kwa furaha, wakimshangilia Mungu.

Mwenyezi Mungu wa kweli! Mwenyezi Mungu anaketi katika kiti Chake cha enzi!

Hivyo imba sifa kwa jina Lake Takatifu!

Bango la ushindi la Mwenyezi limeinuka juu kwa fahari juu ya Mlima Zayuni!

3

Mataifa yanashangilia, watu wote kila mahali wanaimba kwa sauti inayosikika vizuri!

Mlima Zayuni unafurahia, utukufu wa Mungu unatokea!

Kamwe sikuota kwamba nitakutana na Yeye, lakini leo kweli nimekutana naye.

Uso kwa uso kila siku na Yeye, naongea na kuuweka moyo wangu wazi Kwake.

Yeye ni chanzo cha chakula changu na kinywaji, Yeye hunipa kila kitu.

Uzima, maneno, matendo, fikira na mawazo,

Utukufu Wake unang’aa juu yao anapoongoza kila hatua.

Kama moyo wowote utaasi, hukumu itakuja mara moja.

4

Kula na kuishi, kuwa na Mungu; kufurahia na kutembea na Mungu.

Kupokea utukufu na baraka pamoja, kutawala na Yeye ndani ya ufalme Wake.

Raha nyingi sana! Na utamu mwingi sana!

Uso kwa uso kila siku, Ananena nasi.

Tunazungumza na Yeye, tunapewa nuru kila siku,

na kuona kitu mpya kila siku mpya.

Tunafungua macho yetu ya kiroho, siri zetu za kiroho zimefunguliwa!

Kuishi maisha matakatifu ni bure. Njoo, usisimamishe miguu yako.

Endelea kusonga mbele ili uendelee, maisha yanayopendeza yako mbele.

Kupata tu kionjo kitamu hakutoshi, endelea kumkimbilia Mungu.

Yote pamoja na wingi, chochote tunachokosa kiko mikononi Mwake.

Shiriki kwa bidii, ingia ndani Yake, na hakuna kitakachokuwa vile tena.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 15” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 4 Mwana wa Adamu Ameonekana Kwa Utukufu

Inayofuata: 6 Mwenyezi Mungu Aonekana Kama Jua la Haki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki