5 Mwana wa Adamu Ameonekana Kwa Utukufu

1 Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiye anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, aliyevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti Yake kama sauti ya maji mengi. Ana nyota saba katika mkono Wake wa kuume, upanga mkali wenye makali kuwili uko katika kinywa Chake na uso Wake ni kama jua liking’aa kwa nguvu zake!

2 Mwana wa Adamu Ameshuhudiwa, na Mungu Mwenyewe amefichuliwa waziwazi. Utukufu wa Mungu umekuja, uking’aa vikali kama jua lichomalo! Uso Wake mtukufu unawaka kwa mwanga ung’aao; ni macho ya nani yatathubutu kumtendea kwa upinzani? Upinzani husababisha kifo! Hakuna hata chembe ya rehema kwa kitu chochote unachofikiri katika moyo wako, neno lolote usemalo au chochote ufanyacho. Nyinyi nyote mtakuja kuelewa na kuja kuona ni nini ambacho mmekipata—hakuna chochote ila hukumu Yangu!

3 Mwenyezi Mungu hudhihirika katika mwili wa kiroho, bila hata chembe ya mwili au damu ikiunganisha mwili mzima. Yeye huvuka mipaka ya ulimwengu dunia, kama Ameketi kwenye kiti kitukufu cha enzi katika mbingu ya tatu, Akisimamia mambo yote! Ulimwengu na vitu vyote vimo mikononi Mwangu. Kama Nikisema, itakuwa. Kama Nikiliamua, ndivyo litakavyokuwa. Shetani yu chini ya miguu Yangu, yu katika kuzimu! Sauti Yangu itakapotoka, mbingu na nchi zitapita na kuwa bure! Mambo yote yatafanywa upya na huu ni ukweli wa kweli sana usiobadilika. Nimeushinda ulimwengu, kuwashinda waovu wote. Naketi hapa nikizungumza nanyi; wale wote ambao wana masikio wanapaswa kusikiliza na wale wote wanaoishi wanapaswa kukubali.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 15” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 4 Njooni Zayuni Kwa Sifa

Inayofuata: 6 Mwenyezi Mungu Aonekana Kama Jua la Haki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp