Mtu Anayepata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Tayari Kutenda Ukweli

Umuhimu wa kuwa na maisha sahihi ya kanisa unatajwa mara kwa mara katika mahubiri. Kwa hivyo ni kwa nini maisha ya kanisa hayajaboreka bado, na bado ni yale yale ya zamani? Mbona hakuna njia mpya na tofauti kabisa ya maisha? Je, inaweza kuwa kawaida kwa mtu wa miaka ya tisini kuishi kama mfalme wa enzi iliyopita? Ingawa vitu ambavyo watu wanakula na kunywa sasa ni vyakula vitamu vilivyoonjwa mara chache katika enzi zilizopita, hakujakuwa na mabadiliko makubwa katika maisha ya kanisa. Imekuwa kama kutia divai ya kale ndani ya viriba vipya. Je, kuna haja gani basi ya Mungu kusema mengi sana? Makanisa katika maeneo mengi hayajabadilika hata kidogo. Mimi nimeona hili kwa macho Yangu Mwenyewe na ni wazi katika moyo Wangu; hata ingawa sijapitia maisha ya kanisa Mimi Mwenyewe, Nazijua hali za mikusanyiko ya kanisa vizuri sana. Hawajafanya maendeleo mengi. Inarejelea msemo huo—ni kama kutia divai ya kale ndani ya viriba vipya. Hakuna kilichobadilika! Wakati mtu anapowachunga, wao huwaka kama moto, lakini wakati ambapo hakuna mtu wa kuwafadhili, wao ni kama pande kubwa la barafu. Si wengi wanaoweza kuzungumza juu ya mambo ya vitendo, na ni mara chache ambapo mtu yeyote anaweza kushika usukani. Ingawa mahubiri ni ya juu, imekuwa nadra kwa mtu yeyote kupata kuingia. Watu wachache huthamini neno la Mungu. Wao hujawa na machozi wanapolikubali neno la Mungu wanachangamka wanapoliweka kando; na kukosa shauku na uhai wanapoliondokea. Kusema ukweli, nyinyi hamlithamini neno la Mungu hata kidogo, na kamwe hamyaoni maneno kutoka kinywa Chake Mwenyewe sasa kama hazina. Nyinyi huwa na wasiwasi tu mnapolisoma neno Lake, na kuhisi kuchoka mnapolikariri, na inapofika kuliweka neno la Mungu katika matendo, ni kama kujaribu kuzungusha mkono wa pampu ya kisima kwa kuuvuta na unywele kutoka katika mkia wa farasi—haijalishi jinsi utakavyojaribu, huwezi tu kutia nguvu ya kutosha. Nyinyi daima huwa mnachangamka mnaposoma neno la Mungu, lakini mnasahau mnapolitenda. Kwa hakika, maneno haya si lazima yazungumzwe kwa jitihada sana na kurudiwa kwa uvumilivu sana; lakini ukweli kwamba watu husikiliza tu bila kutia neno la Mungu katika vitendo umekuwa kizuizi kwa kazi Yake. Mimi siwezi kukosa kulitaja jambo hili, Mimi siwezi kukosa kulizungumzia. Mimi ninalazimika kufanya hivyo; siyo kwamba Mimi hufurahia kufunua udhaifu wa wengine. Mnafikiri kwamba matendo yenu kadiri yanatosha—kwamba wakati ambapo ufunuo uko kileleni, kuingia kwenu pia kumefikia kilele chake? Je, ni jambo rahisi sana hivyo? Kamwe hamchunguzi msingi ambao hatimaye hujenga uzoefu wenu! Kwa wakati huu, mikusanyiko yenu haiwezi kuitwa maisha yanayofaa ya kanisa hata kidogo, wala haijumuishi maisha yanayofaa ya kiroho kamwe. Ni mkusanyiko tu wa kundi la watu ambao hufurahia kuzungumza na kuimba. Kusema kweli, hakuna uhalisi mwingi ndani yake. Kueleza bayana, kama hutendi ukweli, uhalisi uko wapi? Je, huko siko kujigamba kusema kwamba una uhalisi? Wale ambao daima hufanya kazi ni wenye majivuno na wanaojipenda, wakati ambapo wale ambao hutii daima hutulia na kuinamisha vichwa vyao, bila nafasi yoyote ya kujifunza. Watu ambao hufanya kazi huwa hawafanyi chochote ila kuzungumza, wakizidi na mazungumzo yao yenye kuvutia, na wafuasi husikiliza tu. Hakuna mabadiliko ya kuzungumzia; Hizi zote ni njia za zamani tu! Leo, kuweza kwako kunyenyekea na kutothubutu kuingilia au kutenda jinsi unavyotaka ni kutokana na kuwasili kwa amri za kiutawala za Mungu; siyo mabadiliko uliyoyapata kupitia uzoefu. Ukweli kwamba huthubutu tena kufanya mambo fulani ambayo yanakiuka amri za kiutawala leo ni kwa sababu kazi ya Mungu ya maneno imekuwa na matokeo dhahiri na imewashinda watu. Acha Nimuulize mtu mmoja: Ni kiasi kipi cha mafanikio yako leo kilichopatikana kwa jasho la jitihada yako mwenyewe? Ni kiasi kipi ulichoambiwa moja kwa moja na Mungu? Ungejibu vipi? Je, ungepigwa na bumbuwazi na kutoweza kunena? Ni kwa nini wengine wanaweza kuzungumza juu ya uzoefu wao mwingi halisi ili kukuruzuku, wakati ambapo unafurahia tu chakula ambacho wengine wamepika? Je, huoni haya? Mnaweza kutekeleza uchunguzi wa kutafuta ukweli, mkiwachunguza wale ambao kwa kulinganisha ni wazuri: Unaelewa ukweli kiasi kipi? Je, ni kiasi kipi ambacho wewe hatimaye huweka katika vitendo? Ni nani unayempenda zaidi, Mungu au wewe mwenyewe? Je, wewe hutoa mara nyingi zaidi, au hupokea mara nyingi zaidi? Je, ni mara ngapi umetelekeza nafsi yako ya zamani na kuyaridhisha mapenzi ya Mungu wakati lengo lako lilikuwa lenye kosa? Maswali haya machache tu yatawakanganya watu wengi. Kwa watu wengi, hata wakitambua kuwa nia yao si sahihi, bado wao hufanya makosa makusudi, nao hata hawajakaribia kuikana miili yao wenyewe. Watu wengi huruhusu dhambi kuenea kote ndani yao, wakiruhusu dhambi kuongoza kila tendo lao. Hawawezi kushinda dhambi zao, na wao huendelea kuishi katika dhambi. Baada ya kufika katika hatua hii ya sasa, ni nani asiyejua ni matendo mangapi mabaya ambayo ameyafanya? Ukisema kwamba hujui, basi unasema uongo kabisa. Kusema ukweli, yote ni kutotaka kutelekeza nafsi yako ya zamani. Je, kuna maana gani ya kusema “maneno ya dhati” yaliyo mengi sana ya kutubu ambayo ni bure? Je, hili linakusaidia kukua katika maisha yako? Inaweza kusemwa kwamba kujijua ni kazi yako ya kudumu. Mimi huwakamilisha watu kupitia utii wao na kutenda kwao maneno ya Mungu. Ukivaa tu neno la Mungu jinsi ambavyo ungevaa nguo zako, ili kuwa tu nadhifu na kupendeza, je, hujidanganyi mwenyewe na kuwadanganya wengine? Ikiwa yote uliyo nayo ni mazungumzo na kamwe huyaweki katika matendo, ni kitu gani utakachokipata?

Watu wengi wanaweza kuzungumza kidogo juu ya matendo na wanaweza kuzungumza kuhusu fikira zao za kibinafsi, lakini mengi ya hayo ni mwanga kutoka kwa maneno ya wengine. Hayajumuishi chochote kutoka kwa matendo yao binafsi hata kidogo, wala kujumuisha kile wanachokiona kutokana na uzoefu wao. Nimechambua suala hili mapema; usifikiri kwamba Sijui chochote. Wewe ni tishio la bure tu, lakini unazungumza juu ya kumshinda Shetani, juu ya kutoa ushuhuda wa ushindi, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa Mungu? Huu wote ni upuuzi! Je, unadhani kwamba maneno yote ambayo Mungu amenena leo ni ya wewe kupendezwa nayo? Kinywa chako hunena juu ya kutelekeza nafsi yako ya zamani na kuweka ukweli katika matendo, lakini mikono yako inafanya vitendo vingine na moyo wako unapanga hila zingine—wewe ni mtu wa aina gani? Kwa nini moyo wako na mikono yako si kitu kimoja? Kuhubiri kwingi sana kumekuwa maneno matupu; si hili ni jambo la kuvunja moyo? Ikiwa huwezi kuweka neno la Mungu katika matendo, inathibitisha kuwa bado hujaingia katika njia ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi, bado hujapata kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani yako, na bado hujapata mwongozo Wake. Ukisema kuwa unaweza tu kuelewa neno la Mungu lakini huwezi kuliweka katika matendo, basi wewe ni mtu asiyependa ukweli. Mungu haji kumwokoa mtu wa aina hii. Yesu alipatwa na maumivu makubwa wakati Aliposulubiwa ili kuwaokoa wenye dhambi, kuwaokoa maskini, na kuwaokoa wale watu wote wanyenyekevu. Kusulubiwa Kwake kulitumika kama sadaka ya dhambi. Ikiwa huwezi kutenda neno la Mungu, basi ni heri uondoke haraka iwezekanavyo; usikawie katika nyumba ya Mungu kama mdoezi. Watu wengi hata huona vigumu kujizuia kufanya mambo ambayo humpinga Mungu kwa dhahiri. Je, si wanaalika kifo? Wanawezaje kuzungumza juu ya kuingia katika ufalme wa Mungu? Je, wataweza kuwa na ujasiri wa kuuona uso wa Mungu? Kula chakula ambacho Mungu hukupa, kufanya mambo ya uhalifu ambayo humpinga Mungu, kuwa mwenye nia mbaya, mwenye kudhuru kwa siri, na mwenye kufanya hila, hata wakati ambapo Mungu anakuruhusu ufurahie baraka ambazo Yeye amekupa—je, huzihisi zikiichoma mikono yako unapozipokea? Je, huhisi aibu? Baada ya kufanya kitu kinachompinga Mungu, baada ya kufanya hila ili “kuwa laghai,” je, huhisi hofu? Kama huhisi chochote, unawezaje kuzungumza juu ya wakati wowote ujao? Tayari kulikuwa hakuna wakati ujao kwako zamani za kale, kwa hiyo ni matarajio yapi makubwa zaidi unayoweza kuwa nayo bado? Ukisema kitu bila haya lakini huhisi lawama, na moyo wako hauna ufahamu, basi haimaanishi kwamba tayari umeachwa na Mungu? Kuzungumza na kutenda kwa kujiachilia na bila kuzuiwa kumekuwa asili yako; je, unawezaje kukamilishwa na Mungu hivi? Je, unaweza kutembea ulimwenguni kote? Ni nani anayeweza kushawishiwa na wewe? Wale ambao wanaijua asili yako ya kweli watakaa mbali nawe. Je, si hii ni adhabu ya Mungu? Kwa jumla, ikiwa kuna mazungumzo tu bila matendo, hakuna ukuaji. Ingawa Roho Mtakatifu anaweza kuwa akifanya kazi ndani yako unapozungumza, kama hutendi, Roho Mtakatifu ataacha kufanya kazi. Ukizidi kuendelea kwa njia hii, kunawezaje kuwa na majadiliano yoyote ya wakati ujao au kutoa nafsi yako yote kwa kazi ya Mungu? Unaweza tu kuzungumza juu ya kutoa nafsi yako yote, lakini hujampa Mungu upendo wako wa kweli. Yote Anayopata kutoka kwako ni upendo wa maneno tu; Yeye hapewi kusudi lako la kutenda ukweli. Je, hiki kinaweza kuwa ndicho kimo chako halisi? Ikiwa utaendelea kwa jinsi hii, utakamilishwa na Mungu lini? Je, huhisi wasiwasi juu ya kesho yako ya giza na majonzi? Je, huhisi kwamba Mungu amepoteza tumaini kwako? Je, hujui kwamba Mungu anatamani kuwakamilisha watu wengi zaidi na wapya zaidi? Je, vitu vya zamani vinaweza kudumu? Wewe huyazingatii maneno ya Mungu leo: Je, unasubiri kesho?

Iliyotangulia: Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo

Inayofuata: Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp