1029 Mto wa Maji ya Uzima

1 Mto wa maji ya uzima, safi sana, unatiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo. Katika kila upande wa mto kuna mti wa uzima, unaozaa aina kumi na mbili za matunda, na unazaa matunda yake kila mwezi. Majani ya mti huo ni ya kuyaponya mataifa. Hakutakuwa na laana tena. Kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo atakuwa jijini. Watumishi Wake watamtumikia, na watauona uso Wake, watauona uso Wake. Jina Lake litakuwa kwenye mapaji ya nyuso zao. Na hakutakuwa na usiku; hakutakuwa na haja ya mshumaa, hakuna mshumaa, wala mwanga wa jua; kwa kuwa Bwana Mungu anawapa mwangaza. Watatawala milele na milele.

2 Mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, unakuja chini kutoka kwa Mungu mbinguni, kutoka mbinguni. Tazama, tabenakulo la Mungu liko na wanadamu, Ataishi pamoja nao. Watakuwa watu Wake. Mungu Mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao. Mungu atafuta machozi yao yote kutoka machoni mwao; hakutakuwa na kifo tena, wala huzuni au kulia, hakuna uchungu tena, kwa kuwa mambo ya zamani yamepita. Atampa yule aliye na kiu maji ya chemichemi ya maji ya uzima bure, atampa bure. Yeye anayeshinda atarithi vitu vyote. Mungu atakuwa Mungu Wake, na yeye atakuwa mwana Wake.

3 Maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwanakondoo ni hekalu lake. Na mji haukuwa na haja ya jua, wala mwezi, kuumulika: maana utukufu wake Mungu uliuangaza, na Mwanakondoo ndiye mwanga hapo. Na mataifa ambayo yameokolewa yatatembea katika mwanga wake: nao wafalme wa dunia wanaleta utukufu na heshima yao ndani hapo. Nayo milango yake kamwe haitafungwa mchana: maana hakutakuwa na usiku huko. Na hakutaingia kabisa ndani yake chochote kinachonajisi, wala yeyote atendaye kirihi, ama asemaye uongo: bali wale ambao wameandikwa katika kitabu cha Mwanakondoo cha uzima.

4 Umeme unatoka Mashariki na kuangaza mpaka Magharibi. Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, amekuja miongoni mwa wanadamu. Anaonyesha ukweli: Neno likionekana katika mwili. Mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, watu wote wanakubali mazoezi na usafishaji wa ufalme. Kristo wa siku za mwisho ameleta njia ya milele wa uzima. Watu wa Mungu wako uso kwa uso na Mungu kila siku na kufurahia neno la Mungu, tamu lisilo na kifani. Neno, upanga wa kukata pande mbili, linahukumu kumtakasa na kumwokoa mwanadamu. Hukumu imeanza na nyumba ya Mungu. Pazia imeinuka kwa hukumu ya siku za mwisho. Watu wote wa Mungu wanalitukuza jina la Mwenyezi Mungu. Katika ufalme Wake, Mwenyezi Mungu amekuja. Kazi ya Mungu imekamilishwa. Amepata utukufu wote. Amepata utukufu wote.

Imetolewa kutoka kwa Kitabu cha Ufunuo katika Biblia

Iliyotangulia: 1028 Maisha Mapumzikoni

Inayofuata: 1030 Binadamu Waingiapo Hatima ya Milele

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp