Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?

10/11/2017

Watu wengi hawaelewi ni kwa nini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu katika siku za mwisho, Bwana Yesu anaitwa Mwenyezi Mungu wakati Anapokuja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa nini haendelei kuitwa Bwana Yesu? Kwa kweli, Mungu ana jina jipya kila wakati Anapofanya hatua moja ya kazi Yake. Jina hili jipya linachukuliwa na Mungu Mwenyewe kama inavyofaa kazi hii—siyo kitu ambacho watu humuita Yeye kama wanavyotaka. Jina la Bwana Yesu aliyerejea wa siku za mwisho lilitabiriwa zamani katika Biblia. Katika Kitabu cha Ufunuo, ilisemwa pia kuwa, “Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu Wangu, na hatatoka nje tena: na nitaandika kwake jina lake Mungu wangu, na jina la mji wake Mungu Wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ambao hukuja chini kutoka kwa Mungu Wangu mbinguni: na nitaandika kwake jina langu jipya(Ufunuo 3:12). “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi(Ufunuo 1:8). “Na nikaisikia sauti kana kwamba ilikuwa sauti ya umati mkubwa, na kana kwamba sauti ya maji mengi, na kana kwamba radi kuu, ikisema, Haleluya: kwani Bwana Mungu mwenye uenzi hutawala(Ufunuo 19:6). Jina la Mwenyezi Mungu wa Enzi ya Ufalme ni utimizaji kamili waunabii wa kitabu cha Ufunuo. Jina ambalo Mungu huchukua katika kila enzi lina umuhimi mkubwa na limeshikamana kwa undani na kazi ya Mungu wakati wa enzi hiyo. Mwenyezi Mungu alifichua mafumbo yanayohusiana na hili Aliposema,

Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni mmoja, lakini wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu Wake? Hili likiwa hivyo, Mungu lazima aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, na lazima Atumie jina hilo kubadilisha enzi na kuwakilisha enzi. Kwani hakuna jina moja linaloweza kumwakilisha Mungu Mwenyewe kikamilifu, na kila jina linaweza tu kuwakilisha tabia ya Mungu bainifu ya enzi fulani; kile tu linalohitaji kufanya ni kuwakilisha kazi Yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia Yake kuwakilisha enzi nzima. Bila kujali iwapo ni enzi ya Yehova, au ni enzi ya Yesu, kila enzi inawakilishwa kwa jina(Neno, Vol. 1. Kuonekana kwa Mungu na Kazi Yake. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

‘Yehova’ ndilo jina ambalo Nilichukua wakati wa kazi Yangu katika Israeli, na linamaanisha kwamba Mungu wa Waisraeli (watu wateule wa Mungu) Anayeweza kumwonyesha mwanadamu rehema, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu; Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. ‘Yesu’ ni Imanueli, linalomaanisha sadaka ya dhambi iliyojaa upendo, iliyojaa rehema, na inayomkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, na Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya kazi ya mpango wa usimamizi. Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Israeli, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa watu wote wa Israeli. Na hivyo, katika enzi ya sasa, Waisraeli wote, isipokuwa Wayahudi, wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu na kumtumikia hekaluni wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu, na Yeye ndiye sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka dhambini. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema na lilikuja kuwepo kwa ajili ya kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuja kuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema wazaliwe upya na kuokolewa, nalo ni jina mahususi la ukombozi wa binadamu wote. Hivyo, jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi walilomwita Waisraeli walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina maana wakilishi wa kuwa muhimu: Kila jina linawakilisha enzi moja. ‘Yehova’ linawakilisha Enzi ya Sheria nalo ni jina la heshima ambalo watu wa Israeli walimwita Mungu waliyemwabudu. ‘Yesu’ linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Yudea, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekomea katika Enzi ya Ukombozi, nao haungeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hii ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nilichukua jina la Yesu kwa ajili tu ya wenye dhambi wote katika Enzi ya Neema, lakini si jina ambalo kwalo Nitawafikisha wanadamu wote mwisho. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti za mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kumaliza kwa ukamilifu tabia Yangu nzima na kila kitu Nilicho. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya tamati—enzi ya mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi—Nitaitwa Mungu Mwenyewe mwenye nguvu na mwenyezi, na chini ya jina hili Nitaitamatisha enzi nzima. Niliitwa Yehova wakati mmoja, Nilijulika na watu pia kama Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa upendo na heshima. Leo hii, Mimi si yule Yehova au Yesu tena ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita. Badala yake, Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataitamatisha enzi; Mimi ndiye Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka miisho ya dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu(Neno, Vol. 1. Kuonekana kwa Mungu na Kazi Yake. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”).

Mwenyezi Mungu alisema kwa dhahiri kwamba kuna umuhimu mwakilishi kwa jina ambalo Mungu huchukua katika kila enzi: Kila moja huwakilisha kazi ya Mungu na tabia Anayoonyesha katika enzi hiyo. Wakati wa Enzi ya Sheria, Mungu alitumia jina la Yehova kutangaza sheria na amri Zake na kuyaongoza maisha ya wanadamu duniani; wakati wa Enzi ya Neema, Mungu alitumia jina la Yesu kufanya kazi ya ukombozi wa wanadamu; na wakati wa Enzi ya Ufalme, Mungu anaitwa Mwenyezi Mungu, Yeye hufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu kumtakasa, kumbadilisha, na kumwokoa mwanadamu. Mungu hubadilisha enzi akitumia jina Lake, na hutumia jina hili kuwakilisha kazi ya enzi. Wakati Yehova Mungu alifanya kazi ya Enzi ya Sheria, ni kwa kuomba tu kwa jina la Yehova na kutii sheria na amri Zake ndipo watu wangeweza kubarikiwa na kulindwa na Mungu. Kwa kuwasili kwa Enzi ya Neema, Mungu alitumia jina la Yesu kufanya kazi ya ukombozi, na watu hawakuwa na budi ila kumkubali Bwana Yesu kama Mwokozi, na kuombea toba kwa jina la Bwana, kusamehewa dhambi zao na kufurahia ukweli na neema iliyotolewa na Bwana Yesu. Ikiwa watu bado walishikilia jina la Bwana na kukataa kumkubali Bwana Yesu, basi walipoteza utunzaji na ulinzi wa Mungu, na walianguka katika giza, wakilaaniwa na kuadhibiwa na Mungu kama Mafarisayo Wayahudi. Pamoja na ujio wa siku za mwisho, Mungu hutumia jina la Mwenyezi Mungu kutekeleza kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Ni kwa kukubali jina la Mwenyezi Mungu tu, kwenda sambamba na hatua za kazi ya Mungu, na kufanyiwa hukumu na kuadibiwa kwa Mwenyezi Mungu, ndipo watu wanaweza kuelewa na kupata ukweli, kujitenga na dhambi, kutakaswa, na kupokea wokovu wa Mungu. Wote wanaokataa kulikubali jina la Mwenyezi Mungu na kukataa kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho hawawezi kujitoa wenyewe kutoka kwa utumwa wa dhambi, na milele hawatakuwa na sifa kamili kuingia katika ufalme wa mbinguni.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp