Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

10/11/2017

Wanadamu walipopotoshwa na Shetani, Mungu alianza mpango Wake wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria na kuyaongoza maisha ya wanadamu, Akiwafanya watu kujua kwamba wanapaswa kumwabudu Mungu, na kuwafanya wajue dhambi ni nini. Lakini kutokana na ujio wa hatua za mwisho za Enzi ya Sheria, upotovu wa wanadamu ukawa hata wa kina zaidi, na watu mara nyingi walikiuka sheria na kutenda dhambi dhidi ya Yehova. Walikabiliwa na hatari ya kuhukumiwa na kuuawa kwa sababu ya ukiukaji wao. Hivyo, kwa kujibu mahitaji ya wanadamu, wakati wa Enzi ya Neema Mungu alichukua umbo la kibinadamu na akawa Bwana Yesu. Yeye, Alitundikwa msalabani kwa ajili ya wanadamu, na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi, kuwawezesha watu kuja mbele ya Mungu na kuomba kwa Mungu, kukiri dhambi na kutubu, kusamehewa dhambi zao, na kuishi chini ya utajiri wa neema na baraka za Mungu. Lakini kwa sababu asili ya dhambi ya watu ilikuwa bado haijatatuliwa, na bado mara nyingi walitenda dhambi na kumuasi Mungu, katika Enzi ya Ufalme Mungu mara nyingine akawa mwili, kwa kutumia jina la Mwenyezi Mungu kuonyesha ukweli wote kwa ajili ya wokovu na utakaso wa wanadamu juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, kufuta asili ya dhambi ya wanadamu, kusababisha wanadamu kusitisha uasi wake kwa Mungu na kumpinga Mungu, kuwaruhusu watu kwa hakika kumtii Mungu na kumwabudu Mungu, na hatimaye kuwaongoza wanadamu kwenye hatima nzuri. Ingawa kazi ambayo Mungu amefanya katika Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme imekuwa tofauti, na majina Aliyoyachukua na tabia ambayo Ameonyesha yamekuwa tofauti, kiini na malengo ya kazi Yake ni sawa–yote ni ili kuwaokoa wanadamu, na kazi yote inafanywa na Mungu Mwenyewe. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema, “Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

Kwa maelfu ya miaka, watu wachache wamejua kwa hakika kwamba Bwana Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe, kwamba Yeye ni kuonekana kwa Mungu, na kwamba Yeye ni Mungu aliyepata mwili. Kwa kweli, Biblia tayari imetabiri kwa dhahiri kitambo. Bwana Yesu alisema, “yule ambaye ameniona mimi amemwona Baba(Yohana 14:9). “Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake(Yohana 10:38). “Mimi na Baba yangu tu mmoja(Yohana 10:30). Wakati Bwana Yesu alisema kwamba “Mimi na Baba yangu tu mmoja.” Alikuwa akisema kwamba Yeye na Yehova ni roho mmoja naye. Maneno yanayosemwa na Bwana Yesu na yale yanayosemwa na Yehova ni sawa–wote wawili ni ukweli, ni matamshi ya Roho mmoja, na chanzo ni sawa; yaani, Bwana Yesu na Yehova ni Mungu mmoja. Vivyo hivyo, chanzo cha maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho na yale ya Bwana Yesu ni sawa, ni matamshi ya Roho Mtakatifu, ni ukweli, na ni sauti ya Mungu. Wale wanaomwamini Bwana wote wanajua kwamba idadi kubwa ya unabii katika Biblia inahusu kurudi kwa Bwana na kazi ya hukumu ya Mungu wa siku za mwisho. Kama Bwana Yesu alivyosema, “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo(Yohana 14:3). “Na tazama, ninakuja upesi(Ufunuo. 22:12). “Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija katika wingu akiwa na nguvu na utukufu mwingi(Luk 21:27). “Tazama, nitakuja kama mwizi(Ufunuo 16:15). “Yeye anikataaye mimi, na hayakubali maneno yangu, anaye amhukumuye: neno hilo nililolinena, ndilo hilo litakalomhukumu siku ya mwisho(Yohana 12:48). Katika Waraka wa Kwanza wa Petro pia ilisemwa kuwa, “Kwa maana wakati umefika ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1Pet 4:17). Ilizungumzwa kwa dhahiri sana katika maandiko haya kwamba Bwana Yesu angerejea wakati wa siku za mwisho, na angeonyesha maneno na kufanya kazi ya hukumu. Wakati Mwenyezi Mungu anapokuja wakati wa siku za mwisho, Yeye hufanya kazi ya hukumu akianza kwa nyumba ya Mungu juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, na huonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu. Ingawa kazi ya Mwenyezi Mungu na ile ya Bwana Yesu ni tofauti, chanzo chao ni sawa–Mungu Aliye mmoja! Hili hutimiza kikamilifu unabii wa Bwana Yesu: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambia, lakini hivi sasa hamwezi kuyastahimili. Hata hivyo, yeye, Roho wa kweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwa ukweli wote: kwa maana hatanena juu yake mwenyewe; bali yote atakayoyasikia, hayo ndiyo atakayoyanena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16: 12-13). Mwenyezi Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho ni mfano halisi wa Roho wa kweli; Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Umeme wa Mashariki Unatoka Wapi?

Sasa tuko katika siku za mwisho, unabii wa kurudi kwa Bwana umetimizwa kimsingi, na waumini wengi sana wanaomcha Mungu wanatumai kurudi kwa...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp