Sababu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu Kusemekana Linamwamini Mungu Mwenye Mwili

19/07/2020

Dini mbili kubwa zaidi duniani—Ukristo na Ukatoliki—zote zinamwamini Bwana Yesu na zinakiri kwamba Yeye alikuwa Mungu aliyepata mwili. Kutoka kwa nje, Bwana Yesu alionekana kuwa mwana wa kawaida wa Adamu, lakini Alikuwa na kiini kitakatifu, Alionyesha ukweli na kumpa mwanadamu njia ya toba, Alisulubiwa kwa sababu ya wanadamu, Alitekeleza kazi ya ukombozi, Akahitimisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema, hivyo kutimiza unabii wa Masihi katika Agano la Kale. Bwana Yesu alikuwa Mungu aliyepata mwili; Alikuwa Mwokozi wa wanadamu. Sasa, katika siku za mwisho, Bwana Yesu amerudi katika mwili kama Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Mwenyezi Mungu ni sawa na Bwana Yesu: Kwa nje, Anaonekana kuwa mwana wa kawaida wa Adamu aliye na ubinadamu wa kawaida, lakini zaidi ya hayo, Ana utakatifu kamili. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli wote ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, Akatekeleza kazi ya hukumu katika siku za mwisho, Akahitimisha Enzi ya Neema na kuanzisha Enzi ya Ufalme. Mwenyezi Mungu ni Mungu aliyepata mwili—Mungu mwenye haki anayewahukumu wanadamu.

Mwenyezi Mungu anasema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu). “Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu, inaweza kuonekana kwamba kupata mwili huku ni Roho wa Mungu aliyekuja duniani, akivalia mwili wa mtu wa kawaida. Yeye ana ubinadamu wa kawaida lakini pia ana utakatifu kamili. Kutoka nje, Kristo anaonekana kuwa wa kawaida, lakini Ana kiini Chake kitakatifu na anaweza kuonyesha tabia ya Mungu na kile Mungu anacho na alicho. Aidha, Anaweza kuonyesha ukweli ili kufanya kazi ya kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, na hili si jambo ambalo mtu yeyote tu anaweza kutimiza. Kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu vinafanikisha kikamilifu unabii katika Biblia kuhusu kurudi kwa Bwana Yesu: “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27). “Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu(Mathayo 24:44). “Tazama, Naja upesi; na Nina thawabu Yangu, kumpa kila mwanadamu kulingana na vile matendo yake yatakuwa(Ufunuo 22:12). “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Mwenyezi Mungu ndiye mwana wa Adamu kama ilivyotabiriwa katika Biblia. Yaani, Yeye ni Mungu mwenye mwili, ambaye ameonyesha ukweli wote ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu na Alitekeleza kazi Yake ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Matamshi haya mengi yamekusanywa katika kitabu, Neno Laonekana Katika Mwili. Maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu yanafichua ukweli na siri zote za mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita wa kumwokoa mwanadamu, kusudi la hatua Zake tatu za kazi, siri ya kupata mwili Kwake, jinsi Shetani anavyowapotosha wanadamu, jinsi Mungu kisha anavyomtakasa, kumwokoa na kumkamilisha mwanadamu, hatima za baadaye ya watu na kadhalika, yote ambayo yanathibitisha kikamilifu kwamba Kristo ndiye ukweli, njia na uzima, na kwamba ni Mungu pekee anayeweza kuonyesha ukweli na kufunua siri. Wanadamu hawana ukweli, sembuse wao kuweza kutekeleza kazi ya kuwaokoa wanadamu. Ukweli wote ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu unafanya iwe dhahiri kwetu kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu aliyepata mwili na kwamba Yeye ndiye kuonekana kwa Kristo katika siku za mwisho.

Zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita, wakati Bwana Yesu mwenye mwili alionekana na kutekeleza kazi Yake, Alishutumiwa na makuhani wakuu, walimu na Mafarisayo wa Uyahudi kuwa mtu tu—kuwa mwana wa seremala (rejelea Mathayo 13:55). Hata hivyo, miaka elfu mbili baadaye, injili ya Bwana Yesu imeenea katika ulimwengu mzima na kwa miisho ya dunia. Mungu aliyepata mwili kwa mara ya pili sasa ameonekana na anatekeleza kazi Yake, na wachungaji na wazee wa dunia ya dini wanamshutumu Mwenyezi Mungu vikali kuwa mtu tu. Hata hivyo, waumini wa Mungu husikia sauti Yake, na watu wengi kutoka dini zote na madhehebu yote, wanaomwamini Bwana kwa kweli na wanaotamani sana Mungu aonekane na kufanya kazi, husikia sauti Yake ndani ya maneno ya Mwenyezi Mungu. Wamekiri kwamba Mwenyezi Mungu kweli ndiye Bwana Yesu aliyerudi, na mmoja baada ya mwingine, wamekuja mbele za Mungu. Yote yanayotoka kwa Mungu yatasitawi. Katika muda wa zaidi ya miaka ishirini mifupi tu, injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho imeenea katika bara nzima la China, na sasa inaenda hadi kwa mataifa yote na kila mahali duniani. Idadi inayoongezeka ya watu wanamgeukia Mwenyezi Mungu; hili linaamuliwa na mamlaka na amri Yake ya pekee, na zaidi ya hayo, ni mfano halisi wa uweza na hekima ya Mungu. Mambo haya ya hakika ni thibitisho tosha kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ndiyo ukweli, njia na uzima; Mwenyezi Mungu ndiye Kristo aliyepata mwili, na Yeye ndiye kuonekana kwa mwokozi katika siku za mwisho. Hili halipingiki!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp