Kwa Nini Umeme wa Mashariki Unaenda Mbele Kwa Mwendo Usioweza Kukomeshwa

17/01/2021

Bwana Yesu alisema, “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27). Tangu Umeme wa MasharikiMwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho—Aonekane Uchina kutekeleza kazi Yake, injili Yake ya ufalme imeenea pande zote katika bara zima la Uchina kwa zaidi ya miaka kumi tu. Sasa, imeenea hadi nchi na maeneo mengi ya ng’ambo, na imeyatikisa madhehebu mbalimbali sana na kuathiri dunia nzima. Hata hivyo, swali linalowakanganya zaidi viongozi wa dunia ya kidini ni: Mbona, ingawa wachungaji na wazee wa dini katika dunia ya dini wamefanya kila linalowezekana kupinga, kashifu na kushutumu Umeme wa Mashariki, kuzuia makanisa yao na hata kufika kiwango cha kushirikiana na serikali ya CCP kuwakamata na kuwatesa Wakristo katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, wale waumini kutoka madhehebu mbalimbali ambao wana ubinadamu mzuri na ambao kweli wanamwamini Bwana hukubali na kumfuata Mwenyezi Mungu mmoja baada ya mwingine? Mbona, ingawa umekabiliwa na upinzani na mateso yenye hasira kutoka sehemu mbili za nguvu za Shetani—serikali ya CCP na dunia ya dini—Umeme wa Mashariki haujakosa kuvunjwa au kuchoshwa tu, lakini kinyume chake umeendelea kusitawi na kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kama chipukizi kukua baada ya mvua, na umeendelea mbele bila kuzuilika na kukatalika?

Kwa kweli, si vigumu kupata sababu ya hili. Ingekuwa bora kuangalia kwanza kazi ya Bwana Yesu kabla ya kuchunguza swali hili, na bila shaka tutakuja kupata jibu. Wakati Bwana Yesu alionekana na kutekeleza kazi Yake, Alipitia upinzani na shutuma yenye hasira ya makuhani wakuu waandishi, na Mafarisayo wa Kiyahudi, hadi kiwango ambacho hata walishirikiana na wakuu wa Kirumi kumsulubisha Yesu msalabani, hivyo wakitumaini bure kupiga marufuku kazi ya Bwana Yesu. Kwa nini basi injili ya Bwana Yesu ilienea kotekote katika dunia ya Kiyahudi na hata Mataifa wakasikia? Wakuu wa Kirumi waliwatesa Wakristo kikatili na kuwauwa kinyama kwa miaka mia tatu, kwa hiyo mbona idadi ya Wakristo haikukosa kupungua tu, lakini kinyume chake ilikua na kuendelea wakati wa mateso haya, ikienea kwa kila pembe ya ufalme wa Kirumi na kotekote katika dunia nzima? Ilikuwa kwa sababu Bwana Yesu alikuwa Mungu aliyepata mwili, Alikuwa kuonekana kwa Mungu, na kazi na maneno ya Bwana Yesu yalikuwa kazi na maneno ya Mungu, kwa hiyo hakuna mtu angeweza kukomesha au kuharibu upanuzi wa injili ya Bwana Yesu. Biblia inasema, “Kwa maana kama ushauri huu ama kazi hii ni ya wanadamu, itakuwa bure: Lakini kama ni ya Mungu, hamuwezi kuiangamiza; ili msionekane kana kwamba huenda hata mnapigana dhidi ya Mungu” (Matendo 5:38-39). Yaani, chochote kitokacho kwa Mungu kitasitawi na chochote kitokacho kwa mwanadamu bila shaka kitaoza. Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema, “Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Vivyo hivyo, iwapo Umeme wa Mashariki haukuwa kuonekana na kazi ya Mungu mmoja tu na wa pekee, je, ungeweza kupenya safu baada ya safu ya vizuizi, upinzani na mateso yaliyotolewa na dunia ya kidini na serikali ya CCP inayomkana Mungu, kama ngome ya kuta za chuma, na kuenea kwa haraka kotekote Uchina na hata kotekote katika sehemu nyingine za dunia? Kama haukuwa umeongozwa na kazi ya Roho Mtakatifu, je, ungekuwa na mamlaka na uwezo wa kuyafanya mataifa yote yatiririke kwa mlima huu na dini zote kuungana? Kama haukuwa kuonekana na kazi ya Mungu, je, ungeweza kuuonyesha ukweli na kutekeleza hukumu ili kuwashinda waumini wengi sana wa kweli wa madhehebu mbalimbali, wale kondoo wazuri na kondoo viongozi, na kuwafanya wafuate kwa mioyo thabiti? Ukweli unatosha kuthibitisha kwamba Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu ambaye Umeme wa Mashariki unamshuhudia, ni Bwana Yesu aliyerudi, na kwa kweli ni Mungu ambaye Ameonekana na Hufanya kazi katika siku za mwisho. Kwa hiyo, Umeme wa Mashariki unaweza kusonga mbele kwa mwendo usioweza kukomeshwa huku ukikabiliwa na mateso ya hasira na ukandamizaji wa kikatili wa serikali ya CCP na dunia ya kidini!

Tunapaswa pia kuona kwamba wakati wa Enzi ya Neema wanafunzi waliweza kumfuata Bwana, huku wakiteswa kikatili na wakuu wa Uyahudi na wa Kirumi, kimsingi kwa sababu Bwana Yesu alikuwa Ameonyesha ukweli mwingi sana na alikuwa Amefichua siri za ufalme wa mbinguni, na kwamba watu walisikia sauti ya Mungu katika maneno Yake na kutambua kwamba Bwana Yesu alikuwa Kristo, Masiya aliyepaswa kuja, kwa hiyo waliweza kumfuata kwa mioyo thabiti na kueneza ushuhuda wao kumhusu, jinsi Petro alivyosema, “Bwana, tumwendee nani? Wewe una maneno ya uzima wa milele” (Yohana 6:68). Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli mzima ambao utawaruhusu watu kupata utakaso na kuokolewa, na Ametekeleza kazi Yake ya hukumu Akianzia nyumba ya Mungu. Maneno haya ndiyo ambayo Roho Mtakatifu husema kwa makanisa, na ndiyo kitabu na mihuri saba iliyofunguliwa na Mwanakondoo kama iliyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo (tazama Ufunuo 5:2-10). Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ametoa mamilioni ya maneno ambayo hayafichui tu siri zote za mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000, hayafichui kusudi la Mungu katika hatua Zake tatu za kazi ya kuwaokoa wanadamu, hayafichui usuli, maelezo ya kisirisiri, na kiini kinachoongoza kila hatua ya kazi Yake, pamoja na maelezo ya ndani ya Biblia na siri ya kupata mwili kwa Mungu, lakini pia yanajumuisha ukweli mwingi sana, kama vile jinsi Shetani huwapotosha wanadamu, jinsi Mungu huwaokoa wanadamu, jinsi Mungu hufanya kazi ya hukumu, jinsi watu wanavyoainishwa kila mmoja kulingana na aina yake, matokeo na hatima ya wanadamu, na jinsi ufalme wa Kristo unafanikishwa. Maneno hayafurahishi tu macho ya wanadamu na yanawaruhusu watu kupanua ujuzi wao, lakini pia yanawawezesha watu kuielewa kazi ya Mungu, tabia na asili ya Mungu. Aidha, maneno Yake yanatuwezesha kupata mabadiliko katika tabia na kutakaswa, na kweli maneno Yake yana ukweli wote ambao sisi watu wapotovu tunahitaji ili kuokolewa na kukamilishwa. Kondoo wa Mungu husikia sauti Yake na waumini wanaotii kwa unyenyekevu na kutamani kuonekana kwa Mungu wameshindwa kikamilifu na maneno ya Mwenyezi Mungu wanapotafuta na kuchunguza njia ya kweli; wamekuwa na hakika kwamba hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme ni kazi ya Mungu mmoja; wameona kwa kweli na kwa dhahiri kwamba kazi na maneno ya kweli ya Mungu hayawezi kufananisha na hayawezi kubadilishwa na dhahania au ujuzi wowote uliosababishwa na wanadamu. Maneno Yake ni maonyesho ya ukweli, na yanadhibitisha kwamba Mwenyezi Mungu mwenye mwili hasa ndiye Mwana wa Adamu akirudi katika siku za mwisho na kuonekana kwa Mungu mmoja wa kweli. Kwa hiyo, watu wote husujudu mbele ya Mwenyezi Mungu na kumkiri kama Baba yao, na wanaapa kumfuata hadi mwisho. Hii ndiyo sababu kuna watu zaidi na zaidi walio waaminifu kwa kweli ambao hawaogopi tena ugumu na taabu na wanaomfuata Mwenyezi Mungu.

Aidha, cha muhimu katika kuelewa mbona Umeme wa Mashariki unaweza kuendelea mbele kwa mwendo usioweza kukomeshwa licha ya mateso makali na ukandamizaji wa kikatili wa CCP na dunia ya kidini ni kumjua Mungu na kuijua kazi Yake. Ikiwa tunaweza kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu kwa mioyo mitulivu, na kusoma maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, na ikiwa tunaweza kuelewa hatua tatu za kazi katika mpango mzima wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000, basi ni rahisi kuona kwamba kazi ya hukumu inayotekelezwa na Kristo wa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu—imejengwa juu ya msingi wa kazi ya Yehova Mungu katika Enzi ya Sheria na kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema. Hakuna ukinzani na hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, lakini badala yake zinafuatana moja baada ya nyingine, kila moja ikiwa na jukumu lake, zikiwa zimeunganishwa bila kuchangulika na kuendelea mbele hatua kwa hatua. Hatua tatu za kazi ni kazi ya Mungu mmoja; Yehova, Yesu na Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja, Mungu Mwenyewe aliyeumba mbingu, ulimwengu na vitu vyote.

Fikiria Enzi ya Sheria kwa mfano: Mungu alimtumia Musa kutangaza sheria na amri Zake, kuongoza maisha ya mwanadamu duniani, na ili kwamba ajue dhambi ni nini na jinsi anavyopaswa kumwabudu Mungu. Katika kipindi cha baadaye cha Enzi ya Sheria, wanadamu walipotoshwa kwa kina zaidi na zaidi na Shetani, na bila kutaka wote waliendelea kutenda dhambi, na hawakuweza kufuata amri. Kadri dhambi za wanadamu zilivyoendelea kuongezeka kila siku, sadaka za dhambi zao zikawa chache zaidi na zaidi na waliingia katika mtego usioepukika wa dhambi. Polepole, wanadamu walikosa uchaji wao kwa Mungu na walifika kiwango cha kuwadhabihu mifugo wasioona na waliolemaa katika madhabahu takatifu ya Yehova Mungu, na hivyo hatari ya kufa chini ya laana ya sheria ikawapata. Ilikuwa kwa sababu ya hali hii ndiyo hatua mpya ya kazi ikawa muhimu ili Mungu amwokoe mwanadamu. Hii ni kwa sababu ni Mungu Mwenyewe pekee—Muumba—angeweza kuwaokoa wanadamu waliopotoshwa na walioharibika tabia na, kwa sababu hii, Mungu alipata mwili na kuonekana katika umbo la Bwana Yesu ili Aianze kazi ya ukombozi ya Enzi ya Neema. Alizibeba dhambi za wanadamu na kusulubiwa msalabani kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya wanadamu, hivyo kusamehe dhambi zote za wanadamu kabisa. Bwana Yesu aliwafunza wafuasi Wake kwamba wanapaswa kusamehe na kuwa wenye subira, kuwapenda majirani wao kama wajipendavyo, na kuchukua msalaba ili wamfuate. Pia Aliwafunza watu kufanya mambo kama kumega mkate, kunywa divai, kuosha miguu ya wengine, na kufunika vichwa vyao. Bwana Yesu aliwataka watu kuweka ukweli zaidi katika vitendo, Alihitaji zaidi kutoka kwa wanadamu kuliko ilivyohitajika wakati wa Enzi ya Sheria, na Alimletea mwanadamu mwelekeo wa kufuata katika enzi mpya. Alimradi watu walimwamini Bwana Yesu, kutubu na kukiri Kwake, basi wangeweza kufurahia neema ya kutosha ya Bwana na kutapa ukombozi Wake. Bwana Yesu alileta kazi katika Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria iliyoanza zaidi ya miaka 2,000. Ilikuwa kazi mpya zaidi na kuu zaidi iliyotekelezwa juu ya msingi wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria.

Baada ya sisi kumwamini Bwana, ingawa tunasamehewa dhambi zetu, kuthibitishwa kwa imani yetu, na kuokolewa, hili linamaanisha tu kwamba sisi si wa dhambi na kwamba Mungu hatuoni kama watenda dhambi. Lakini bado tunatenda dhambi mara nyingi na tunaishi katika mzunguko wa kutenda dhambi na kukiri na kutubu siku zote. Hatuzivunji pingu za dhambi kwa kweli na, punde hali zinazofaa zinapoibuka, tabia zetu potovu za kishetani zitafichuliwa bila sisi kutaka, kama vile ufidhuli na majivuno, kupigania umaarufu na mali, upotovu na ulaghai, na kudanganya na kusema uwongo. Hatuwezi kujizuia kutenda dhambi na kumkosea Bwana, jinsi Paulo alivyosema: “Kwa sababu kutaka kumo ndani yangu, lakini jinsi ya kutenda lililo jema sipati” (Warumi 7:18). Ni dhahiri kwamba sisi kumwamini Bwana Yesu na kusamehewa dhambi zetu hakuonyeshi kwamba tumepatwa kikamilifu na Mungu. Ni kwa sababu chanzo cha msingi cha dhambi hizi, yaani asili yetu ya kishetani inayompinga na kumsaliti Mungu, hakijatatuliwa. Kwa njia hii, hata kama Mungu hakumbuki dhambi zetu na Hatutendei kulingana na dhambi zetu, hata hivyo tunaishi katika mwili na hatuna njia ya kutupa asili yetu ya dhambi. Hata kama dhambi zetu zingesamehewa mara elfu moja au mara elfu kumi, na Enzi ya Neema ingeendelea kwa miaka mingine elfu mbili, bado tungetenda dhambi, na bado tungemwasi na kumsaliti Mungu, na tusiweze kuvunja pingu za asili yetu ya dhambi. Kwa hiyo ili wanadamu wapotovu waokolewe kikamilifu kutoka kwa ushawishi wa Shetani, lazima Mungu atekeleze hatua nyingine ya kazi binafsi, ile ambayo ni ya kina na kamilifu zaidi, kuwaokoa wanadamu, na ambayo itatatua kabisa tabia potovu za kishetani na asili ya dhambi ya mwanadamu, hivyo kumwezesha mwanadamu kutupa kabisa ushawishi wa Shetani na kupatwa kikamilifu na Mungu. Kwa hiyo, Bwana Yesu aliahidi kwamba Atarudi, na kutabiri kwamba Ataandaa wokovu kamili zaidi wa mwanadamu.

Kwa kweli, Biblia ina unabii kuhusu wokovu wa Mungu katika siku za mwisho ambapo Waraka wa Kwanza wa Petro sura ya 1 mstari wa 5 unasema, “Ninyi mnaohifadhiwa na nguvu zake Mungu kupitia imani hadi kwa wokovu ambao uko tayari kufichuliwa katika muda wa mwisho.” Mstari huu wa maandiko unatabiri wazi: Kwa kuwa sisi ambao humfuata Bwana Yesu, Mungu ametuandalia wokovu katika siku za mwisho. Kwa hiyo, huu wokovu katika siku za mwisho utakuwa nini kwa kweli? Biblia inasema: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). “Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:48). “Na nikamwona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, akiwa na injili ya daima kuwahubiria hao wanaoishi katika ulimwengu, na kwa kila taifa, na ukoo, na lugha, na watu, Akisema kwa sauti kuu, Mwogopeni Mungu, na kumpa utukufu; kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja(Ufunuo 14:6-7). Tunaweza kuona kutoka katika maandiko haya kwamba “injili ya milele” inahusu kazi ya hukumu ikianzia nyumba ya Mungu, ambapo Mungu hutumia maneno makali kama panga ili kumhukumu na kumtakasa mwanadamu. Hii hasa ndiyo hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe iliyotajwa katika Kitabu cha Ufunuo, na ndiyo kazi na kuwatenga kondoo kutoka kwa mbuzi na ngano kutoka kwa makapi, ya kutenga kila kulingana na aina yake, na ya kuamua hatima za watu. Mwenyezi Mungu anasema, “Ikifika kwa neno ‘hukumu,’ utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli). Tunaweza kuelewa kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba: Katika siku za mwisho, Mungu hufanya kazi ya hukumu na Huonyesha ukweli wote unaohukumu, kutakasa na kuwaokoa wanadamu, Anawajulisha watu wote kazi Yake, tabia Yake, na kile Anacho na alicho na aidha, Anafunua na kuhukumu tabia zote potovu za mwanadamu kutokana na yeye kupotoshwa na Shetani, na ukweli kuhusu upotovu wake, ili wanadamu waweze kuelewa mapenzi Yake vyema, wawe na maarifa ya kweli kumhusu Yeye, na kuelewa kweli chanzo na kiini cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani. Zaidi ya hayo, kazi ya hukumu pia huwaruhusu wanadamu kupata ukweli kwa hakika, njia na uzima uliotolewa na Kristo wa siku za mwisho kwa kweli, hivyo kubadili mawazo na tabia zao za zamani, ikitakasa kabisa asili yao ya dhambi, na kuwafanya kuwa watu walio na ukweli na ubinadamu, wanaomtii Mungu kweli, wanaoishi kwa kudhihirisha mfanano wa kweli wa binadamu na wanaoupata wokovu wa Mungu kikamilifu na kupatwa na Mungu. Kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu ni wokovu kamili zaidi inayojengwa juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, na pia ni hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu inayohitimisha mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000, ambayo ni kazi ya kumshinda na kumkamilisha mwanadamu; kwa kweli huu ndio wokovu kamili uliofichuliwa katika siku za mwisho, ambao Mungu ametuandalia.

Ndugu, huo ni ushirika wa kutosha kwa sasa, na ninatumai kwamba mmepata ufahamu kiasi kuhusu mbona Umeme wa Mashariki bado unaendelea mbele kwa mwendo usioweza kukomeshwa, licha ya mateso ya hasira kutoka kwa serikali ya CCP na dunia ya kidini. Hasa ni kwa sababu Umeme wa Mashariki ni kuonekana na kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Mwenyezi Mungu ndiko kuwasili kwa Mwokozi—Kristo wa siku za mwisho; kazi Yake ya hukumu ndio wokovu unaoonekana katika siku za mwisho ambao waumini wote wa kweli wametamani sana kwa muda mrefu sana. Kwa hiyo, injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu imeweza kuenea kwa kasi sana kotekote katika bara lote la Uchina, na hata kuenea kwa kila nchi na taifa la dunia. Ndugu wapendwa, mnapokabiliwa na kuonekana na kazi ya Mungu, mnapaswa kufanya uchaguzi upi? Bwana Yesu alisema, “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, nami nawajua wao, nao hunifuata(Yohana 10:27). Ikiwa mnaelewa, basi mnasubiri nini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp