568 Unapaswa Kukubali Uchunguzi wa Mungu Katika Vyote Ufanyayo

1 Leo, watu wengi wanaogopa sana kuyaleta matendo yao mbele za Mungu, na ingawa unaweza kuudanganya mwili wa Mungu, huwezi kumdanganya Roho wa Mungu. Yale yote ambayo hayawezi kustahimili uchunguzi wa Mungu hayakubaliani na ukweli nayo lazima yawekwe kando, ama unatenda dhambi dhidi ya Mungu. Kwa hivyo, haijalishi kama ni wakati unaomba, unaponena na kushiriki na ndugu na dada zako, ama unapofanya wajibu wako na kufanya biashara yako, lazima uuweke moyo wako mbele za Mungu. Unapoitimiza kazi yako, Mungu yuko nawe, na bora nia yako iwe sawa, nayo iwe kwa ajili ya kazi ya nyumba ya Mungu, Atakubali kila kitu ufanyacho, kwa hivyo ni lazima uweke bidii kwa dhati kujishughulisha na kuitimiza kazi yako.

2 Kila kitu unachofanya, kila tendo, kila nia, na kila jibu lazima kiletwe mbele za Mungu. Hata maisha yako ya kawaida ya kiroho—maombi yako, ukaribu wako kwa Mungu, jinsi unavyokula na kunywa maneno ya Mungu, ushirika wako na kina ndugu zako na maisha yako ndani ya kanisa—na huduma yako katika ushirikiano wako vinaweza kuletwa mbele za Mungu ili Yeye avichunguze. Ni matendo kama hayo ndiyo yatakayokusaidia kustawi katika maisha.

3 Mchakato wa kukubali uchunguzi wa Mungu ni mchakato wa kutakaswa. Kadri unavyoukubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyotakaswa zaidi na kadri unavyokubaliana na matakwa ya Mungu, ili kwamba hutajipata katika uasherati, na moyo wako utaishi katika uwepo wa Mungu; kadri unavyokubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyomuaibisha Shetani na kuutelekeza mwili. Kwa hivyo, kukubali uchunguzi wa Mungu ni njia ambayo watu wanafaa kutenda.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Anawakamilisha Wale Wanaoupendeza Moyo Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 567 Utukufu wa Mungu Unashikilia Umuhimu Mkubwa Kabisa Kati ya Wanadamu

Inayofuata: 569 Kudura Ya Mtu Itaishia Kuwaje Mwishowe?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp