598 Unapaswa Kukubali Uchunguzi wa Mungu Katika Kila Kitu

1 Wale ambao wanaweza kutia ukweli katika vitendo wanaweza kukubali uchunguzi makini wa Mungu katika matendo yao. Unapokubali uchunguzi makini wa Mungu, moyo wako unawekwa kuwa sawa. Ikiwa daima unafanya tu mambo kwa ajili ya wengine kuona na hukubali uchunguzi makini wa Mungu, je, una Mungu moyoni mwako? Watu kama hawa hawana moyo unaomcha Mungu. Usifanye mambo kwa ajili yako daima na usiyafikirie masilahi, hadhi na sifa yako mwenyewe kila wakati. Lazima kwanza uyafikirie masilahi ya nyumba ya Mungu, na uyape kipaumbele. Unapaswa kuyafikiria mapenzi ya Mungu na uanze kwa kutafakari kama umekuwa mwenye najisi katika utimizaji wa wajibu wako au la, kama umefanya kila uwezalo kuwa mwaminifu, kama umefanya kila uwezalo kutimiza majukumu yako, na kufanya kadiri uwezavyo au la, na vile vile kama umefikiria wajibu wako na kazi ya nyumba ya Mungu kwa moyo wote au la. Lazima uyazingatie mambo haya.

2 Yafikirie mara kwa mara, na itakuwa rahisi kwako kutekeleza wajibu wako. Iwapo wewe ni mwenye ubora duni wa tabia, uzoefu wako ni wa juu juu, au wewe hujabobeba katika kazi yako ya kitaalamu, basi kunaweza kuwa na makosa au upungufu katika kazi yako, na matokeo huenda yasiwe mazuri sana—lakini utakuwa umetiajuhudi zako zote. Wakati hufikirii tamaa zako za binafsi ama kufikiria maslahi yako mwenyewe katika mambo unayoyafanya, na badala yake unafikiria kila wakati kuhusu kazi ya nyumba ya Mungu, ukifikiria maslahi yake, na kutimiza wajibu wako vizuri, basi utakuwa ukikusanya matendo mema mbele za Mungu. Watu wanaotenda matendo haya mema ndio wale walio na uhalisi wa ukweli; hivyo, wamekuwa na ushuhuda.

Umetoholewa kutoka katika “Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 597 Timiza Wajibu Wako na Utakuwa Shahidi

Inayofuata: 599 Kuishi kwa ajili ya Kutimiza Wajibu Wako Kuna Maana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp