653 Jinsi ya Kukubali Hukumu ya Maneno ya Mungu

1 Ili ujijue, ni lazima ujue maonyesho ya upotovu, udhaifu wako mkuu, tabia yako, na asili yako na kiini chako. Lazima pia ujue, maelezo yote kabisa, mambo hayo ambayo hufichuliwa katika maisha yako ya kila siku—nia zako, mitazamo yako, na msimamo wako kuhusu kila kitu—iwe uko nyumbani au nje, unapokuwa kwenye mikusanyiko, unapokuwa ukila na kunywa maneno ya Mungu, au katika kila suala unalokumbana nalo. Kupitia vitu hivi lazima uje kujijua. Ili kujijua kwa kina, lazima ujumuishe maneno ya Mungu; unaweza tu kupata matokeo kwa kujijua kulingana na maneno Yake.

2 Wakati ambapo tunapokea hukumu ya maneno ya Mungu, hatupaswi kuogopa mateso, wala hatupaswi kuogopa maumivu; na sembuse kuogopa kwamba maneno ya Mungu yataumiza mioyo yetu. Tunapaswa kusoma matamshi Yake zaidi kuhusu jinsi Anavyotuhukumu na kutuadibu na kufichua asili zetu potovu. Lazima tuyasome na kuyafuata na kujilinganisha kwayo mara kwa mara. Kamwe usiwalinganishe wengine nayo—tunafaa tujilinganishe wenyewe dhidi. Hatuna upungufu wowote katika vitu hivi vyote; sote tunaweza kulingana nao. Kabla ya kufanya chochote kingine, tunafaa kutambua kwamba tunafaa kukubali kila mojawapo ya neno lililonenwa na Mungu, iwe matamshi haya yanavutia kusikia au hayavutii na ikiwa yanatupatia hisia chungu au tamu. Huu ndio mtazamo tunaopaswa kuwa nao juu ya maneno ya Mungu.

3 Katika imani yetu, lazima tusisitize kwa uthabiti kwamba maneno ya Mungu ndiyo ukweli. Kwa kuwa kweli ndiyo ukweli, tunapaswa kuyakubali kwa busara. Bila kujali ikiwa tunaweza kutambua au kukubali au la, mtazamo wetu wa kwanza kuelekea maneno ya Mungu unapaswa kuwa ule wa kukubali kabisa. Maneno ya Mungu ni ya maana sana. Kila kitu ambacho Mungu husema, kila kitu ambacho hufichua kinahusu tabia potovu za watu, na vitu muhimu na vilivyokita mizizi ndani ya maisha yao. Hayo ni mambo muhimu, si mambo yanayoonekana nje, na haswa si tabia za nje. Kwa hvyo, huwezi kutegemea sura au kile unachoona kwa nje kulinganisha na maneno ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Umuhimu wa Kufuatilia Ukweli na Njia ya Kuufuatilia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 652 Ninyi Ndio Wale Watakaopokea Urithi wa Mungu

Inayofuata: 654 Jinsi ya Kukubali Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp