581 Ni kwa Kutenda kwa Maadili Tu Ndiyo Mtu Anaweza Kufanya Wajibu Wake Vyema

1 Haijalishi ni wajibu upi unaotimiza, lazima utafute kushika mapenzi ya Mungu na kuelewa mahitaji Yake ni yapi kuhusiana na wajibu wako; ni hapo tu ndipo utaweza kushughulikia mambo kwa njia ya maadili. Katika kutekeleza wajibu wajo, huwezi kabisa kufuata upendeleo wako binafsi, kwa kufanya chochote ambacho ungependa kufanya, chochote ambacho unngefurahia na kuridhika unapokifanya au chochote ambacho kingekufanya uonekane kuwa mzuri. Ukimlazimishia kwa nguvu upendeleo wako kwa Mungu au kuutenda kama kwamba ni ukweli, ukiyafuata kana kwamba ni kanuni za ukweli, basi huko si kutekeleza wajibu wako, na kutekeleza wajibu wako kwa njia hakutakumbukwa na Mungu. Waliyaona yale waliyoyaamini kuwa sahihi, mema, na mazuri kuwa ukweli; haya ni makosa.

2 Hata ingawa wakati mwingine watu wanaweza kufikiri kuwa jambo fulani ni sahihi na kwamba linaambatana na ukweli, hilo halimaanishi kwamba lazima liwe linaambatana na mapenzi ya Mungu. Kadiri watu wanavyofikiri kwamba jambo fulani ni sahihi, ndivyo wanavyopaswa kuwa waangalifu zaidi na ndivyo wanavyopaswa kutafuta ukweli zaidi ili kuona iwapo kile wanachofikiria kinaridhisha matakwa ya Mungu. Ikiwa kinapingana na matakwa Yake na kinapingana na maneno Yake, basi umekosea kufikiria kwamba ni sahihi, ni wazo la binadamu tu, na si lazima kwamba kitaambatana na ukweli bila kujali jinsi unavyokifikiria kuwa sahihi. Uamuzi wako wa kilicho sahihi na chenye makosa unapaswa kutegemezwa kwa maneno ya Mungu pekee, na bila kujali jinsi unavyofikiria kwamba kitu fulani ni sahihi, ni lazima ukitupilie mbali isipokuwa iwapo kina msingi katika maneno ya Mungu. Wajibu ni nini? Ni agizo lililoaminiwa kwa watu na Mungu. Hivyo unapaswaje kutimiza wajibu wako? Kwa kutenda kwa mujibu wa matakwa na viwango vya Mungu, na kutegemeza tabia yako kwa kanuni za ukweli badala ya matamanio ya dhahania ya binadamu. Kwa njia hii, wewe kutimiza wajibu wako kutakuwa kumefikia kiwango kinachohitajika.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kutafuta Kanuni za Ukweli Tu Ndiyo Mtu Anaweza Kutekeleza Wajibu Wake Vizuri” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 580 Kutenda Maneno ya Mungu na Kumridhisha Mungu Huja Kwanza

Inayofuata: 582 Ni Waaminifu Tu Ndio Wanaoweza Kutekeleza Wajibu Wao kwa Kuridhisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp