1003 Baada ya Mungu Kurudi Sayuni

1 Baada Yangu kurudi Sayuni, wale walio duniani wataendelea kunisifu Mimi kama zamani. Wale watendaji huduma waaminifu wanabaki wakisubiri kutoa huduma Kwangu lakini kazi yao itakuwa imefika mwisho. Jambo bora zaidi wanaloweza kufanya ni kutafakari hali Yangu kuwa duniani. Wakati huo, Nitaanza kushusha maafa juu ya wale ambao watakabiliwa na maafa makubwa; ilhali kila mtu anaamini kwamba Mimi ni Mungu mwenye haki. Bila shaka Sitawaadhibu wale watendaji-huduma waaminifu, bali nitawaruhusu tu wapokee neema Yangu. Maana Nimesema kuwa nitawaadhibu watenda dhambi wote, na kwamba wale wanaotekeleza matendo mema watapata starehe yakinifu iliyokirimiwa nami, huu ni ufunuo kwamba Mimi ni Mungu wa haki na uaminifu Mwenyewe.

2 Nitakaporudi Sayuni, Nitaanza kugeuka kuelekea kila taifa duniani; Nitawaleta Waisraeli kwa wokovu na kuwaadibu Wamisri. Hii ni hatua inayofuata katika kazi Yangu. Kazi Yangu wakati huo haitakuwa sawa kama siku hizi: Haitakuwa kazi katika mwili lakini itauzidi mwili kabisa, na kwa kuwa Nimenena, itafanyika, na kama Nilivyoagiza, itasimama imara. Mradi imesemwa nami, itatimizwa mara moja katika hali halisi, na hii ndiyo maana ya kweli ya neno Langu kunenwa na kutimizwa kwake kufanyika kwa wakati mmoja, kwa sababu Ninachosema ni mamlaka yenyewe. Sasa Ninanena kuhusu baadhi ya mambo ya jumla ili kuwasaidia watu duniani kuwa na dalili chache bali si kufahamu ovyo ovyo. Wakati huo utakapofika, kila kitu kitapangwa nami na hakuna anayepaswa kutenda kimakusudi ili kuepuka kuangushwa kwa mkono Wangu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 120” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1002 Mungu Arudipo Sayuni

Inayofuata: 1004 Matakwa ya Mungu kwa Wafuasi Wake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp