955 Malengo na Kanuni za Matendo ya Mungu ni Wazi

1 Mungu kubadilisha nia Zake kwa watu wa Ninawi hakukuhusisha kusitasita au kutoeleweka kokote. Badala yake kulikuwa ni mabadiliko kutoka kwa hasira tupu hadi uvumilivu mtupu. Huu ni ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Mungu kamwe si wa kusitasita au asiye na uamuzi katika vitendo Vyake; kanuni na makusudio yaliyo katika matendo Yake yote ni wazi na dhahiri, yasiyo na dosari wala doa, yasiyo kabisa na hila ama njama zozote zilizochanganywa ndani. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu hakina giza wala maovu.

2 Mungu alikasirikia Waninawi kwa sababu vitendo vyao viovu vilikuwa vimefikia macho Yake; wakati ule hasira Yake ilitokana na kiini Chake. Hata hivyo, wakati hasira ya Mungu ilitoweka na akatoa uvumilivu Wake kwa watu wa Ninawi kwa mara nyingine tena, kila kitu Alichofichua kilikuwa bado ni kiini Chake. Uzima wa badiliko hili ulitokana na badiliko katika mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu. Katika kipindi hiki chote cha muda, tabia ya Mungu isiyokosewa haikubadilika; kiini cha Mungu cha uvumilivu hakikubadilika; kiini cha Mungu cha upendo na huruma hakikubadilika.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 954 Maafa Yafikapo

Inayofuata: 956 Mtazamo wa Mungu kwa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp