973 Yote Asemayo na Kutenda Mungu ni Ukweli

1 Na kwa Mungu kuhusu asili ovu ya Shetani na tabia potovu ya mwanadamu, Hagombani kamwe wala kubishana na watu, na kamwe Halalamiki wakati watu wanatenda kutokana na ujinga. Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno ambalo amesema na kila kitendo amefanya kinahusiana na ukweli.

2 Ukweli huu sio tu ndoto isiyo na msingi; ukweli huu na maneno haya yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake. Kwa sababu maneno haya na kiini cha kila kitu Mungu amefanya ni ukweli, tunaweza kusema kwamba kiini cha Mungu ni kitakatifu. Kwa maneno mengine, kila kitu ambacho Mungu anasema na kufanya kinaleta uzima na mwangaza kwa watu, kinawaruhusu watu kuona vitu vizuri na uhalisi wa vitu hivyo vizuri, na kinaashiria wanadamu njia ili watembelee njia njema. Vitu hivi vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha Mungu na vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha utakatifu Wake.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 972 Mungu Huongoza Maisha ya Mwanadamu Daima

Inayofuata: 974 Amri za Enzi Mpya

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp