Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Ufalme Wote Washangilia

I

Dunia nzima inaporudi kwa Mungu,

Kazi Yake ulimwenguni kote inafuata sauti Yake.

Watu watatumia njia nyingi kupokea maneno Yake.

Wote wakaribia na kumwabudu Mungu. Hizi zitakuwa kazi za Mungu.

Mungu hataanza tena kamwe mahali pengine.

Atawafanya watu wote waje mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani,

na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma,

na watu watalazimika kutafuta njia ya kweli.

Ufalme wote unaposhangilia, ni siku ya utukufu wa Mungu.

Mataifa na watu wanaopata habari njema ya Mungu

watabarikiwa na kutunzwa na Yeye.

II

Jumuiya nzima ya kidini inakabiliwa na njaa kali,

na ni Mungu wa leo pekee aliye chemchemi ya maji yaliyo hai,

Akimiliki chemchemi itiririkayo milele iliyotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu,

na watu watakuja na kumtegemea Yeye.

Wanaopata neno la Mungu wana njia ya kutembea.

Wanaoishi bila neno la Mungu wanapaswa kutafuta njia ya kweli.

Maneno ya Mungu yataenea kwa nyumba nyingi. Yatajulikana kwa wote.

Ni hapo tu ndipo kazi Yake itaenea ulimwenguni kote.

Ufalme wote unaposhangilia, ni siku ya utukufu wa Mungu.

Mataifa na watu wanaopata habari njema ya Mungu

watabarikiwa na kutunzwa na Yeye.

III

Kwa hivyo kama kazi ya Mungu itapanuka, maneno Yake ni lazima yaenee.

Maneno ya Mungu yanaonyesha mamlaka yayo mnamo siku ya utukufu Wake.

Maneno Yake yote, tangu kabla ya enzi hadi sasa yatatimia.

Utukufu wote utakuwa kwa Mungu. Maneno Yake yatatawala duniani.

Waovu wataadibiwa na maneno yaliyo katika kinywa cha Mungu,

na wenye haki watabarikiwa kwa maneno yaliyo katika kinywa Chake.

Wote wataasisiwa na kukamilishwa,

yote yatatimizwa na maneno Yake.

Ufalme wote unaposhangilia, ni siku ya utukufu wa Mungu.

Mataifa na watu wanaopata habari njema ya Mungu

watabarikiwa na kutunzwa na Yeye.

Ufalme wote unaposhangilia, ni siku ya utukufu wa Mungu.

Mataifa na watu wanaopata habari njema ya Mungu

watabarikiwa na kutunzwa na Yeye.

kutoka katika "Ufalme wa Milenia Umewasili" katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Njia ya Kutafuta Ukweli

Inayofuata:Kuwa Mtu Anayekubali Ukweli

Maudhui Yanayohusiana

 • Njia Yote Pamoja na Wewe

  I Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini. Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza. Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako, nina ama…

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  Ⅰ Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  Ⅰ Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…

 • Wewe Tu Unaweza Kuniokoa Mimi

  Ⅰ Mnyenyekevu na Uliyejificha, Wewe unaambatana na watu katika matatizo yao, Ukiwapa njia ya uzima wa milele. Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwe…