930 Vitu Vyote Huishi Chini ya Sheria na Amri Zilizowekwa na Mungu

1 Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia viumbe vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku zingali zinabadilishana nafasi zao bila kusita; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nao batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao.

2 Wadudu aina ya nyenje kwenye mchanga wanaimba kwelikweli kwenye siku za kiangazi; nyenje kwenye nyasi wanaimba kwa sauti ya polepole huku wakikaribisha msimu wa mapukutiko, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia pweke; fahari za simba wakijitosheleza wenyewe kwa kuwinda; nao kunguni wa kaskazini wa Ulaya hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni yanafanyika kwa muda wa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kusalia. Wanaishi katika ruzuku na kustawishwa na Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 929 Binadamu Bado ni Binadamu Wale Ambao Mungu Aliwaumba

Inayofuata: 931 Matendo ya Ajabu ya Mungu Katika Kusimamia Vitu Vyote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp