362 Mungu Hamruhusu Kiumbe Yeyote Kumdanganya

1 Kwa kuwa tayari umeweka uamuzi wako kunitumikia Mimi, sitakuacha uende. Mimi ni Mungu anayechukia uovu, na Mimi ni Mungu ambaye ana wivu kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umewekelea maneno yako juu ya madhabahu, Sitakuvumilia wewe kuhudumia mabwana wawili. Je, ulifikiri ungepata upendo mwingine baada ya kuweka maneno yako juu ya madhabahu Yangu, baada ya kuyaweka mbele ya macho Yangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo? Je, ulidhani kwamba ungeweza kuweka nadhiri kikawaida, kula kiapo Kwangu Mimi na ulimi wako?

2 Je, ungewezaje kula kiapo kwa kiti Changu cha enzi, Aliye Juu Zaidi? Je, ulifikiri kwamba viapo vyako vilikuwa tayari vimekufa? Hata kama miili yenu ikifa, viapo vyenu haviwezi kufa. Hatimaye, Nitawahukumu kwa msingi wa viapo vyenu. Lakini mnadhani kwamba mnaweza kuweka maneno yenu mbele Yangu ili kunivumilia Mimi na kwamba mioyo yenu inaweza kuwatumikia pepo wachafu na pepo wabaya. Je, hasira Yangu ingewezaje kuwavumilia hao watu mithili ya mbwa na nguruwe wanaonidanganya?

3 Lazima Nitekeleze amri Zangu za kiutawala, na kuwapokonya kutoka kwa mikono ya pepo wachafu wale wote wenye fukuto, “wacha Mungu” ambao wanaamini katika Mimi “kunitumikia” Mimi kwa njia ya mpango, kuwa ng’ombe Wangu, kuwa farasi Wangu na kudhibitiwa na Mimi. Nitakufanya ushike uamuzi wako wa awali na kunitumikia Mimi tena. Siwezi kuvumilia kiumbe yeyote kunidanganya Mimi. Je, ulifikiria kwamba ungeweza kufanya maombi tu kiutukutu na kudanganya kiutukutu mbele Yangu? Je, ulifikiri kwamba Mimi sikuwa nimesikia au kuona maneno na matendo yako? Je, maneno yako na matendo yako yangekosaje kuwa katika mtazamo Wangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo?

Umetoholewa kutoka katika “Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 361 Udanganyifu wa Mwanadamu kwa Mungu Huenea Katika Matendo Yao

Inayofuata: 363 Watu Hawajui Jinsi Walivyo Duni

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp