Wale Wasiojifunza na Wanaosalia Wajinga: Je, Wao Sio Wanyama?

Unapoitembea njia ya leo, ufuatiliaji unaofaa zaidi ni wa aina gani? Katika ufuatiliaji wako, unapaswa kujiona kama mtu wa aina gani? Unafaa kujua jinsi unavyopaswa kukabili yote yanayokukumba leo, yawe majaribu ama taabu, ama kuadibu na laana isiyo ya huruma. Unapaswa kuyazingatia kwa uangalifu katika hali zote. Mbona Nasema hili? Nasema hili kwa sababu yanayokukumba leo hata hivyo ni majaribu mafupi yanayotokea tena na tena; huenda huyaoni kuwa yanayosumbua sana kiakili, na hivyo unayaacha mambo yaende mrama, na huyachukulii kuwa rasilmali ya thamani katika ufuatiliaji wa maendeleo. Wewe ni asiyejali kweli! Sana kiasi kwamba unaifikiria rasilmali kana kwamba ni wingu linaloelea machoni pako, na huyathamini haya mapigo makali yanayokuja mara kwa mara—mapigo ambayo ni ya muda mfupi na yanayoonekana kuwa dhaifu kwako—ila unayatazama kwa utulivu, usiyafikirie kwa dhati na kuyachukulia tu kama mapigo ya mara moja. Wewe ni mfidhuli sana! Kwa mashambulio haya makali, mashambulio yaliyo kama dhoruba na yanayokuja mara kwa mara unaonyesha kupuuza kwa dharau; wakati mwingine hata unatabasamu bila hisia, ukifichua jinsi usivyojali—kwani hujawahi kujiwazia mbona unashinda ukipitia “misiba” kama hii. Je, Namtendea mwanadamu bila haki kwa kiasi kikubwa? Je, Natafuta makosa kwako? Ingawa shida zako za akili huenda zisiwe nzito jinsi Nilivyoeleza, kupitia utulivu wako wa nje, tangu zamani umebuni taswira nzuri sana ya dunia yako ya ndani. Hakuna maana ya Mimi kukuambia kwamba jambo la pekee lililofichika katika vina vya moyo wako ni matusi yasiyo adilifu na athari dhaifu ya huzuni ambayo wengine hawayaoni. Kwa sababu unahisi kwamba si haki hata kidogo kupitia majaribu kama haya, unatoa matusi; majaribu hayo hukufanya uhisi ukiwa wa dunia, na kwa sababu ya hili, unajawa na ghamu. Badala ya kutazama nidhamu na mapigo haya yanayorudiwa kama ulinzi bora kabisa, unayaona kuwa uchokozi wa Mbinguni usio na sababu, ama vinginevyo kama adhabu inayokufaa. Wewe ni mpumbavu sana! Unazifungia nyakati nzuri gizani bila huruma; mara kwa mara unaona nidhamu na mapigo mazuri kuwa mashambulio kutoka kwa adui zako. Huwezi kubadilika kulingana na mazingira yako sembuse kutaka kufanya hivyo kwani huna hiari ya kupata chochote kutoka kwa kuadibu huku kunakorudiwa na unakoona kuwa katili. Hufanyi juhudi yoyote kutafuta au kuchunguza, na, unajikabidhi tu kwa yale majaaliwayako, kwenda pahali popote itakapokuelekeza. Yanayoonekana kwako kuwa marudio makali hayajaubadili moyo wako wala hayajatwaa udhibiti wa moyo wako; badala yake, yanakuchoma moyoni. Unaona “kuadibu huku katili” kuwa adui wako katika maisha haya tu na hujapata chochote. Wewe unajidai sana! Ni mara chache ambapo unaamini kwamba unapitia majaribu kama haya kwa sababu wewe ni duni sana; badala yake, unajiona aliye na bahati mbaya sana, na kusema kwamba Mimi daima hutafuta makosa kwako. Kufikia leo, kwa kweli una kiasi kipi cha maarifa ya kile Ninachosema na kufanya? Usifikiri kwamba una kipaji cha asili, uliye chini kidogo ya mbingu lakini juu sana ya dunia. Wewe si mwerevu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote—na hata inaweza kusemwa kwamba wewe ni mpumbavu zaidi kuliko watu wowote duniani walio na mantiki, kwani unajiona sana kuwa bora, na hujawahi kujiona kuwa mtu wa chini; inaonekana kwamba unayachunguza matendo Yangu kwa utondoti kabisa. Kwa kweli, wewe ni mtu ambaye kimsingi hana mantiki, kwa kuwa hufahamu kabisa Nitakachofanya sembuse kutambua Ninachofanya sasa. Kwa hivyo Nasema kwamba wewe hata hulingani na mkulima mzee anayefanya kazi kwa bidii shambani, mkulima ambaye hafahamu maisha ya binadamu hata kidogo na bado anategemeabaraka za Mbinguni wakati anapolima shamba. Huyafikirii maisha yako hata kidogo, hujui chochote chenye sifa sembuse kujijua. Wewe “una hadhi ya juu” sana! Kweli, Nawaonea ninyi walimbwende na ninyi wanawake wadogo wanaopendeza wasiwasi: Mtawezaje kustahimili shambulio kuu zaidi la dhoruba? Walimbwende hawajali hata kidogo mazingira wanamojipata. Kwao, linaonekana jambo lisilo la ya maana, wanalipuuza, wao si wabaya, wala hawajioni kuwa hafifu na duni; badala yake wanaendelea kutembea kwa majivuno mitaani wakipeperusha feni zao. Hawa “watu wakubwa” wapumbavu wasiojifunza kamwe hawajui kwa nini Nawaambia mambo kama haya; sura zao zikiwa zimejaa ghadhabu, wao hujaribu tu kujijua, na baadaye wanaendelea na tabia zao ovu; punde wanapotengana nami, wanaaza tena kuwa bila nidhamu duniani, wakifanya hila zao za zamani. Sura yako hubadilika haraka kweli. Kwa hivyo, unajaribu kunidanganya kwa njia hii tena—wewe ni jasiri kweli! Kinachochekesha hata zaidi ni wale wanawake wadogo warembo. Wanaposikia matamshi Yangu ya dharura na kuona mazingira waliomo, machozi yasiyo karibishwa yanatiririka usoni pao, wanajawa na vikweukweu, na wanaonekana kufanya vituko—jambo la kuchukiza kweli! Kwa sababu ya vimo vyao wenyewe, wanajitupa kwenye vitanda vyao na kulala hapo, wakilia bila kukoma, kana kwamba wako karibu kuishiwa na pumzi. Maneno haya yamewaonyesha utoto wao, upuuzi, uhafifu na uduni wao, na baadaye wanalemewa na uhasi, uchangamfu unawaondoka, machoni mwao na, wala kulalamika kunihusu Mimi au kunichukia Mimi, wanakuja kuwa wasiotikisika katikaubaridi wao na vilevile wao wanashindwa kujifunza na wanabaki wajinga. Baada ya kuniacha Mimi, wanafanya mzaha na kuchezacheza, vicheko vyao vinavyovuma vikiwa kama vya “kengele ya Binti wa Kifalme”. Kweli wao ni dhaifu na wasiojipenda! Ninyi nyote, wenye kasoro na kukataliwa ya wanadamu—jinsi gani mnavyokosa ubinadamu! Hamjui jinsi ya kujipenda au jinsi ya kujilinda, hamna akili, hamtafuti njia ya kweli, hampendi mwanga wa kweli na aidha, hamjui jinsi ya kujithamini. Mmeyapuuza mafundisho Yangu yaliyorudiwa tangu zamani. Hata mnayachukulia kuwa vitu vya kuchezea wakati hamna shughuli, na daima mnayafikiria kuwa “hirizi yenu wenyewe ya kujilinda.” Mnaposhutumiwa na Shetani, mnaomba; wakati ninyi ni hasi, mnalala; wakati mna furaha, mnakwenda huku na huko; Ninapowashutumu, mnanyenyekea mno; na mnapotengana nami, mnacheka kwa shauku. Ukiwa katika umati, hakuna mwingine mwenye hadhi kubwa kukuliko, lakini kamwe hujioni kuwa fidhuli zaidi kuwaliko wote. Daima wewe ni mwenye kiburi, aliyeridhika na mwenye maringo kukithiri. Je, inawezekanaje “waungwana na wasichana wadogo” na “mabwana na mabibi” ambao hawajifunzi na wanabaki kuwa wajinga wanawezaje kuyachukulia maneno Yangu kuwa hazina ya thamani? Sasa Nitaendelea kukuhoji: Umejifunza nini hasa kutoka kwa maneno na kazi Yangu katika muda mrefu kama huu? Je, hujakuwa mjanja zaidi katika udanganyifu wako? Mstaarabu zaidi katika mwili wako? Wa kawaida zaidi katika mtazamo wako Kwangu? Nakwambia waziwazi: Nimefanya kazi nyingi sana, lakini imeongeza ujasiri wako, ujasiri ambao awali ulikuwa kama ule wa panya. Hofu yako Kwangu inapunguka kila siku, kwani Mimi ni mkarimu sana, na kamwe sijawatilia vkwazo kwa mwili wako kwa njia ya ukatili; Labda unavyoona, Mimi Nasema maneno makali—lakini kwa mara nyingi huwa Nakutolea tabasamu, na ni nadra ambapo Nakukaripia ana kwa ana. Aidha, Mimi husamehe udhaifu wako kila wakati, na ni kwa sababu ya hili tu ndiyo unanitendea jinsi nyoka humtendea mkulima mzuri. Napendezwa na kiwango chajuu cha ujuzi na ustadi kwa uwezo wa mwanadamu kuchunguza sana! Acha nikwambie ukweli mmoja: Leo haijalishi hata kidogo iwapo una moyo wa uchaji au la; Mimi sina wasiwasi wala wahaka kuhusu hilo. Lakini pia ni lazima Nikuambie hili: Wewe, huyu “mtu mwenye kipaji,” asiyejifunza na anasalia mjinga, hatimaye utaangamizwa na ujanja wako wenye kiburi na kujioenda—ni wewe utakayeteseka na kuadibiwa. Siwezi kuwa mjinga sana kiasi cha kukuandama unapoendelea kuteseka kuzimuni, kwani Mimi silingani na wewe. Usisahau kwamba wewe ni kiumbe aliyelaaniwa na Mimi, na bado aliyefunzwa na kuokolewa na Mimi. Huna chochote Ninachoweza kutotaka kutengana nacho. Kila Nifanyapo kazi, Sizuiliwi na watu, matukio ama vitu vyovyote. Mitazamo na maoni Yangu kuwahusu wanadamu daima yamebaki yale yale. Mimi si mwenye tabia njema kwako hasa, kwa kuwa wewe ni nyongeza kwa usimamizi Wangu na hauko bora sana kuliko kiumbe mwingine. Nakushauri hivi: Kila wakati, kumbuka kwamba wewe ni kiumbe wa Mungu tu! Unaweza kuishi nami, lakini unapaswa kujua utambulisho wako; usijione kuwa wa hadhi ya juu sana. Hata Nisipokushutumu, ama kukushughulikia, na Nakutazama kwa tabasamu, hili halithibitishi kwamba wewe unalingana na Mimi; unapaswa kujua kwamba wewe ni mmoja wa wale wanaofuatilia ukweli, sio ukweli wenyewe! Hupaswi kamwe kukoma kubadili kwa kuambatana na maneno Yangu. Huwezi kuepuka hili. Nakushauri ujaribu kujifunza jambo wakati huu muhimu, fursa hii adimu ikujapo. Usinipumbaze; Sikutaki utumie ubembelezaji kujaribu kunidanganya. Unaponitafuta, yote siyo kwa ajili Yangu, bali kwa ajili yako mwenyewe!

Iliyotangulia: Utambulisho wa Asili wa Mwanadamu na Thamani Yake: Je, Viko Namna Gani?

Inayofuata: Watu Waliochaguliwa wa China Hawana Uwezo wa Kuwakilisha Kabila Lolote la Israeli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp