181 Mamlaka na Umuhimu wa Kupata Mwili kwa Mungu

1 Kile ambacho mwanadamu amepata sasa—kimo cha mwanadamu leo, maarifa yao, upendo, uaminifu, utiifu, na pia kuona kwao—ni matokeo yanayopatikana kupitia hukumu ya neno. Hivi sasa mwanadamu anaona kuwa kazi ya Mungu kupata mwili ni ya ajabu kweli. Kuna mengi ambayo hayawezi kupatikana na mwanadamu, na kwamba ni mafumbo na maajabu. Kwa hivyo, wengi wamejiwasilisha. Wengine hawajawahi kujiwasilisha kwa mwanadamu yeyote kutoka siku za kuzaliwa kwao, ilhali wanapoyaona maneno ya Mungu siku hii, wanajiwasilisha kikamilifu bila kujua wamefanya vile, na hawajaribu kuchunguza au kusema chochote kingine. Binadamu wameanguka chini ya neno na wamesujudu chini ya hukumu ya neno.

2 Ni kwa kupata mwili pekee ndiyo Mungu ataweza kuwasilisha maneno Yake Mwenyewe kwa masikio ya wale wote ambao wana masikio waweze kuyasikia maneno Yake na kupokea kazi Yake ya hukumu kupitia kwa neno. Hayo tu ndio matokeo yanayopokewa na neno Lake, badala ya kutokea kwa Roho ikimtisha mwanadamu kuwasilisha. Ni kupitia tu kwa kazi ya vitendo na ya ajabu ndio tabia ya mwanadamu, iliyofichika ndani zaidi kwa enzi nyingi, ifichuliwe kabisa ili mwanadamu aitambue na kuibadilisha. Hili ndiyo kazi ya vitendo ya Mungu mwenye mwili; Ananena na kutekeleza hukumu kwa njia ya vitendo ili kupata matokeo ya hukumu juu ya mwanadamu kupitia kwa neno. Haya ndiyo mamlaka ya Mungu mwenye mwili na umuhimu wa Mungu kupata mwili.

3 Ingawa mwili Wake ni hali ya nje ya mwanadamu wa kawaida, ni matokeo ambayo neno Lake linapokea ndiyo yanamwonyesha mwanadamu kuwa Amejaa mamlaka, kwama ni Mungu Mwenyewe na kwamba maneno Yake ni maonyesho ya Mungu Mwenyewe. Hii inaonyesha wanadamu wote kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe, Mungu Mwenyewe Aliyekuwa mwili, kwamba hapaswi kukosewa na yeyote na kwamba hakuna anayeweza kuepuka hukumu Yake kupitia kwa neno, na hakuna nguvu ya giza inayoweza kutamalaki juu ya mamlaka Yake. Mwanadamu anamtii Yeye kabisa kwa sababu Yeye ni Neno aliyepata mwili, kwa sababu ya mamlaka Yake, na kwa sababu ya hukumu Yake kwa neno. Kazi iliyoletwa na mwili Wake uliokuwa mwili ni mamlaka ambayo Anamiliki.

Umetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 180 Kupata Mwili kwa Mungu ni Hasa ili Kuonyesha Neno Lake

Inayofuata: 182 Mamlaka ya Mungu Kupata Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp