219 Amkeni Karibuni, Ninyi Mlio Werevu

1 Kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu kwa kweli ni ngumu kwa watu kuwaza na yote huingia katika uhalisi; kwa kweli haitakufaa kuwa mzembe. Kama moyo wako na mawazo si sahihi, basi hutakuwa na njia. Kutoka mwanzo hadi mwisho ni lazima uwe macho wakati wote na kuhakikisha kuwa umejikinga dhidi ya uzembe. Heri wale ambao daima huwa macho na kusubiri na ambao wako kimya mbele Yangu! Heri wale ambao daima hunitegemea Mimi kwa mioyo yao, ambao huhakikisha wameisikiliza kwa karibu sauti Yangu, ambao huzingatia matendo Yangu na ambao huweka maneno Yangu katika matendo! Wakati kweli hauwezi kuvumilia taahira; mabaa ya kila namna yataenea, yakifungua midomo yao mikali, yenye damu kuwala nyinyi nyote kama mafuriko. Wakati umefika! Hakuna nafasi zaidi ya kuwaza. Njia pekee itakayowaleta chini ya ulinzi Wangu ni kurudi Kwangu.

2 Wale ambao ni werevu lazima kwa haraka wauelewe ukweli! Achilia mambo yote ambayo huna nia ya kuyaacha. Mambo haya kwa kweli ni hatari kwa maisha yako na yasiyokuwa na manufaa! Natumaini unaweza kunitegemea Mimi katika matendo yako, vinginevyo njia tu iliyo mbele itakuwa njia ya kifo, na ni wapi basi utakakokwenda kutafuta njia ya maisha? Uondoe moyo wako ambao unapenda kujishughulisha na mambo ya nje! Uondoe moyo wako ambao huwakaidi watu wengine! Kazi ya Roho Mtakatifu sasa si kama wewe unavyofikiria. Kama huwezi kuziachilia dhana zako basi utapata hasara kubwa. Kama kazi ingekuwa ni kwa kuambatana na dhana za mtu, je, asili yako ya zamani na dhana zingeweza kufichuka? Je, ungeweza kuwa na uwezo wa kujijua mwenyewe? Labda bado unadhani kuwa huna dhana, lakini wakati huu bado pande zako zote mbalimbali mbaya zitafichuka.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 14” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 218 Itii Kazi ya Roho ili Kufuata Hadi Mwisho

Inayofuata: 220 Waumini Lazima Wafuate Nyayo za Mungu kwa Karibu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp