Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

201 Kuzinduka kwa Barakala

1

Nilikuwa barakala, nikifuatilia falsafa za maisha za Shetani,

nikithamini amani na uvumilivu kuliko vyote na kamwe kutobishana na mtu yeyote.

Nilipofanya mambo au kuingiliana na wengine, nililinda majivuno, kiburi na hadhi yangu.

Nilijifanya kutojua ukweli, na singesema kile nilichoona waziwazi sana.

Kama kitu hakikunihusu, basi niliacha kanuni zangu na kutokitilia maanani.

Nilijilinda, nikasaliti dhamiri yangu mwenyewe ili nisimkasirishe mtu yeyote.

Nilikubali shida bila kulalamika, niliishi maisha ya aibu na nikapoteza ubinadamu wangu.

Bila unyoofu au heshima, sikustahili kuwa mwanadamu.

2

Nilipopitia hukumu ya maneno ya Mungu, nilizinduka mara moja.

Nilipoelewa ukweli, niliona waziwazi ukweli wa uovu na upotovu wa wanadamu.

Nilianguka mbele za Mungu na nikahisi majuto makuu moyoni mwangu.

Nilichukia ubinafsi na ubahili wangu mwenyewe, na nikajichukia kwa kupoteza uaminifu na heshima yangu.

Huyu barakala alikuwa amefichuliwa mwishowe: Niliwaumiza wengine, nikajidhuru na Mungu alinichukia.

Mjanja, mdanganyifu, mnafiki, siwezi kuitoroka hukumu ya Mungu.

Maneno ya Mungu ni ukweli, kanuni za juu zaidi maishani.

Watu waaminifu humtii Mungu, wao hutenda kwa unyoofu na kwa moyo mkunjufu.

Wao hutenda ukweli na kupokea kibali cha Mungu, wakiishi katika nuru.

Ninaamua kuwa mtu mwaminifu, kuishi kwa kufuata maneno ya Mungu,

kuacha upotovu na udanganyifu wangu, na kumcha Mungu na kuepukana na maovu.

Nitatenda wajibu wangu kwa uaminifu na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu ili nimtukuze Mungu.

Iliyotangulia:Hukumu ya Mungu Imeniokoa

Inayofuata:Toba ya Dhati

Maudhui Yanayohusiana

 • Tilia Maanani Majaliwa ya Binadamu

  1 Mungu anawahimiza watu wa makabila yote, nchi zote na hata nyanja: Sikilizeni sauti ya Mungu na kuona kazi Yake; tilia maanani jaala ya binadamu; mf…

 • Furaha Katika Nchi ya Kanaani

  1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu kuingia kati…

 • Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

  Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena, hawamwiti baba tena. 1 …

 • Upendo Safi Bila Dosari

  1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vizuizi au ba…