563 Kanuni za Msingi za Kutatua Asili ya Mtu
Kutatua asili ya mtu kunaanza na kuutelekeza mwili. Kuutelekeza mwili pia kunahitaji kanuni. Je, mtu anaweza kuutelekeza mwili kwa mtindo wa kipumbavu? Wakati utakapofika utakubali matakwa ya mwili. Kuna kanuni ambayo ni muhimu sana, ambayo ni kufikiria mara mbili kabla ya kutenda; ichunguze mbele ya Mungu. Zaidi ya hayo, kila jioni lazima uzichunguze hali zako mwenyewe. Hii ni kanuni moja. Chunguza tabia yako mwenyewe: matendo gani yalifanywa kulingana na ukweli na matendo gani yalikiuka kanuni. Hoja hizi mbili ndizo za muhimu sana! Moja ni kujichunguza wakati wa tendo na nyingine ni kujichunguza baada ya tendo. Kanuni ya tatu ni: Kuwa wazi kabisa na nini maana ya kuuweka ukweli katika matendo na kinachomaanishwa na kusema kushughulikia mambo kwa namna ya kufuata kanuni. Unapokuwa wazi kabisa kuhusu hili, utashughulikia mambo kwa usahihi. Kwa kufuata kanuni hizi tatu, basi utaweza kujizuia. Asili yako ya kwanza haitaweza kujifichua, haitaweza kujitokeza. Hii pia ni kanuni ya msingi ya kushughulikia asili ya binadamu.
Umetoholewa kutoka katika “Kutenda Ukweli na Kutatua Asili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo