493 Ungependa Kuwa Tunda la Kufurahiwa na Mungu?

1 Nyakati zote, watu Wangu wanapaswa kujihadhari dhidi ya hila danganyifu za Shetani, walinde lango la nyumba Yangu kwa ajili Yangu, waweze kusaidiana na kupeana mahitaji, kitu ambacho kitawazuia kuingia katika mtego wa Shetani, wakati mtakapokuwa na majuto ya kuchelewa sana. Kwa nini Ninawafundisha kwa hali hiyo ya dharura? Kwa nini Ninawaelezea ukweli wa ulimwengu wa kiroho? Kwa nini Ninawakumbusha na kuwaonya mara kwa mara? Je, mmewahi kufikiri juu ya hili? Je, mmewahi kulielewa? Hivyo, hamhitaji tu kuweza kuwa wazoefu kwa kutegemeza juu ya msingi wa zamani, bali, zaidi, kuondoa uchafu ndani yenu chini ya uongozi wa maneno ya leo, mkiruhusu kila maneno Yangu kukita mzizi na kustawi ndani ya roho zenu, na muhimu zaidi, kuzaa matunda zaidi.

2 Hiyo ni kwa sababu kile Ninachokiomba si maua angavu yaliyostawi sana, bali matunda mengi—matunda, zaidi ya hayo, ambayo hayaharibiki. Je, mnaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu? Ingawa maua katika nyumba ya kioo ya kuhifadhi mimea ni yasiyohesabika kama nyota, na huwavuta watalii wote, mara yanaponyauka yanakuwa mabovu mabovu kama hila danganyifu za Shetani, na hakuna mtu anayevutiwa nayo. Lakini kwa wale ambao wamerushwa na upepo na kuchomwa na jua na kuwa na ushuhuda Kwangu, ingawa maua haya si mazuri, mara yanaponyauka, hapo panatokea tunda, maana haya ndiyo matakwa Yangu. Ninapozungumza maneno haya, mnaelewa kiwango kipi? Mara maua yanaponyauka na kuzaa matunda, na mara matunda haya yote yanaweza kutolewa kwa ajili ya furaha Yangu, Nitakamilisha kazi Yangu yote duniani, na Nitaanza kufurahia udhihirisho wa hekima Yangu!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 3” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 492 Ushauri wa Mungu kwa Mwanadamu

Inayofuata: 494 Uhalisi Huja tu kwa Kuyatenda Maneno ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp