428 Jinsi ya Kutulia Mbele za Mungu

1 Ikiwa mnataka kweli kuifanya mioyo yenu kuwa na amani mbele za Mungu, lazima mfanye kazi ya ushirikiano kwa makusudi. Hiyo ni kusema, kila mmoja wenu lazima achukue muda kuwa mbali na kila mtu, jambo, na chombo kwa ajili ya ibada zenu binafsi za kiroho, ambapo mtaweza kuleta amani kwa mioyo yenu na kujituliza mbele za Mungu. Mnapaswa kuwa na muhtasari wenu binafsi wa ibada ambapo mnaweza kurekodi ufahamu wenu wa neno la Mungu na jinsi roho zenu zimesisimuliwa, haijalishi kama mnachoandika ni cha kina au ni cha juujuu. Tulizeni mioyo yenu mbele za Mungu kwa kusudi.

2 Ikiwa unaweza kutoa saa moja au mbili kwa maisha ya kiroho ya kweli wakati wa mchana, basi maisha yako siku hiyo yatahisi kusitawishwa na moyo wako utakuwa mchangamfu na bila hatia. Ikiwa unaishi maisha haya ya kiroho kila siku, basi utaweza kumpa Mungu moyo wako zaidi na zaidi, roho yako itakuwa imara zaidi na zaidi, hali yako itakuwa bora zaidi na zaidi, utakuwa na uwezo zaidi wa kutembea katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu, na Mungu atakupa baraka zaidi na zaidi. Mwanzoni, huenda usiweze kutimiza mengi katika suala hili, lakini usijiruhusu kurudi nyuma au kugaagaa katika ukanaji—lazima uendelee kufanya kazi kwa bidii!

3 Kadri unavyoishi maisha ya kiroho, ndivyo moyo wako utakavyomilikiwa zaidi na maneno ya Mungu, ukishughulika na mambo haya daima na kuubeba mzigo huu daima. Baada ya hiyo, unaweza kufichua ukweli wako wa ndani kabisa kwa Mungu kupitia maisha yako ya kiroho, mwambie unachotaka kufanya, kile ambacho umekuwa ukifikiri, ufahamu wako na maoni yako mwenyewe ya neno la Mungu. Usizuie chochote, hata kidogo! Jizoeze kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, mwambie ukweli, na usisite kuzungumza yaliyo moyoni mwako.

4 Kadri unavyofanya hivi, ndivyo utakavyohisi zaidi upendo wa Mungu, na moyo wako utavutiwa zaidi na zaidi kumwelekea Mungu. Wakati ambapo hili litafanyika, utahisi kwamba Mungu ni mpenzi zaidi kwako kuliko mtu mwingine yeyote. Hutawahi kumwacha Mungu kamwe, lolote liwalo. Ikiwa utafanya aina hii ya ibada ya kiroho kila siku na usiiondoe akilini mwako, bali uichukulie kama wito wako katika maisha, basi neno la Mungu litaumiliki moyo wako. Hii ndiyo maana ya kuguswa na Roho Mtakatifu. Itakuwa kana kwamba moyo wako daima umetawaliwa na Mungu, kana kwamba kumekuwa na upendo ndani ya moyo wako daima. Hakuna anayeweza kuliondoa hilo kutoka kwako. Wakati hili litatokea, Mungu ataishi ndani yako kweli na kuwa na nafasi ndani ya moyo wako.

Umetoholewa kutoka katika “Maisha ya Kawaida ya Kiroho Huwaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 427 Mungu Awatuza Mara Mbili Zaidi Wale Wanaoshirikiana Naye

Inayofuata: 429 Jinsi ya Kuutuliza Moyo Wako Mbele za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp