511 Mshuhudie Mungu Katika Vitu Vyote ili Umridhisha Mungu

1 Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. Mambo huwatokea watu wakati Mungu anawataka wasimame imara katika ushuhuda wao Kwake. Hakuna kubwa lililokutendekea kwa sasa, na huna ushuhuda mkubwa, lakini kila chembe ya maisha yako ya kila siku inahusiana na ushuhuda kwa Mungu. Ikiwa utawavutia ndugu na dada zako, wanafamilia, na kila aliye karibu nawe; ikiwa siku moja wasioamini watakuja na wavutiwe na yote unenayo na utendayo, na kuona kuwa yote afanyayo Mungu ni ya ajabu, basi utakuwa umekuwa na ushuhuda.

2 Ijapokuwa huna ufahamu na wewe si mwerevu sasa, kupitia kwa kufanywa mkamilifu na Mungu, unaweza kumridhisha na kuzingatia mapenzi Yake, ukiwaoshyesha wengine kazi kubwa Aliyofanya miongoni mwa watu wenye ubora duni wa tabia. Watu wanapokuja kumjua Mungu na kuwa washindi mbele ya Shetani, waaminifu kwa Mungu kwa kiwango kikubwa, basi hakuna aliye na uthabiti kuliko hili kundi la watu, na huu ndio ushuhuda mkubwa zaidi. Ijapokuwa huwezi kufanya kazi kubwa, unaweza kumridhisha Mungu. Wengine hawawezi kuyaacha mawazo yao, ila wewe unaweza; wengine hawawezi kuwa na ushuhuda kwa Mungu wakati wa mapito yao ya kweli, ila unaweza kutumia hadhi na matendo yako ya kweli kulipia mapenzi ya Mungu na kuwa na ushuhuda mkubwa Kwake. Hili ndilo huhesabika kama mapenzi ya kweli kwa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 510 Lazima Umshuhudie Mungu Katika Vitu Vyote

Inayofuata: 512 Ni Msingi wa Maneno ya Mungu tu Unaotoa Njia ya Kutenda

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp