821 Jinsi ya Kumshuhudia Mungu Katika Imani Yako

1 Umepitia kazi nyingi sana ya Mungu, umeiona kwa macho yako mwenyewe na kuipitia wewe binafsi; wakati umefika mwisho kabisa, ni lazima uweze kutenda kazi inayokupasa uifanye. Litakuwa jambo la kusikitisha kweli usipoweza! Katika siku zijazo, wakati injili inaenezwa, unapaswa kuweza kuzungumzia maarifa yako mwenyewe, ushuhudie yote uliyoyapata moyoni mwako na utumie jitihada yote. Kiumbe aliyeumbwa anapaswa kufanikisha hili. Umuhimu wa kweli wa hatua hii ya kazi ya Mungu ni upi? Athari yake ni ipi? Na ni kiwango chake kipi kinatekelezwa ndani ya mwanadamu? Watu wanapaswa kufanya nini? Unapoweza kuzungumza kwa uwazi kuhusu kazi yote ambayo Mungu mwenye mwili amefanya tangu aje duniani, basi ushuhuda wako utakuwa kamili.

2 Unapoweza kuzungumza kwa uwazi kuhusu vitu hivi vitano: umuhimu wa kazi Yake; maudhui yake; kiini chake; tabia inayowakilisha; na kanuni zake, basi hili litathibitisha kwamba unaweza kumshuhudia Mungu, kwamba kweli una maarifa. Mahitaji yangu kwenu si ya juu sana, na yanaweza kutimizwa na wale wote wanaofuatilia kwa kweli. Ikiwa umeazimia kuwa mmoja wa mashahidi wa Mungu, ni lazima uelewe kile Mungu anachochukia sana na kile Mungu Anachopenda. Umepitia kazi Yake nyingi; kupitia kazi hii, ni lazima upate kujua tabia Yake, uelewe mapenzi Yake na mahitaji Yake kwa wanadamu, na utumie maarifa haya kumshuhudia na kutenda wajibu wako.

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 820 Ushuhuda Anaopaswa Kuwa Nao Mwanadamu

Inayofuata: 822 Jinsi ya Kushuhudia kwa Mungu ili Upate Matokeo ya Vitendo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp