510 Lazima Umshuhudie Mungu Katika Vitu Vyote

1 Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita.

2 Kwa mfano, ikiwa unawabagua ndugu na dada zako, utakuwa na maneno ambayo unataka kusema—maneno unayohisi huenda yasimpendeze Mungu—lakini usipoyasema, utahisi kutoridhika ndani, na kwa wakati huu vita vitazuka ndani yako. Kwa hivyo, katika kila jambo unalopitia kuna vita, na wakati kuna vita ndani yako, kutokana na ushirikiano wako na kuteseka kwako, Mungu anafanya kazi ndani yako. Hatimaye unaweza kuliweka kando jambo lenyewe na ghadhabu yako inazimika. Hiyo ndiyo athari ya ushirika wako na Mungu. Kila kitu wafanyacho watu kinawahitaji kulipa gharama fulani katika juhudi zao. Bila taabu ya kweli, hawawezi kumridhisha Mungu.

3 Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda. Kwa nje yataonekana kama mambo madogo; lakini haya mambo yakitendeka huonyesha kama unampenda Mungu au la. Ikiwa unampenda, utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako Kwake, na ikiwa hujaweka upendo Wake katika vitendo, hili linaonyesha kuwa wewe si Mtu ambaye anapenda kuuweka ukweli katika vitendo, kwamba huna ukweli, huna uzima, kuwa wewe ni makapi!

Umetoholewa kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 509 Watu Wanaopatwa na Mungu Wamemiliki Uhalisi

Inayofuata: 511 Mshuhudie Mungu Katika Vitu Vyote ili Umridhisha Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp