1012 Wanaoamini na Wasioamini Hawalingani Kabisa
1 Kila mtu ana hatima inayofaa. Hatima hizi zinaamuliwa kulingana na asili ya kila mtu na hazihusiani kabisa. Hakuna uhusiano kati ya mume anayeamini na mke asiyeamini, na hakuna uhusiano kati ya watoto wanaoamini na wazazi wasioamini. Ni aina mbili zisizolingana. Kabla ya kuingia rahani, mtu ana jamaa wa kimwili, lakini baada ya mtu kuingia rahani, mtu hana jamaa wa kimwili tena wa kuzungumzia. Wanaofanya wajibu wao na wasiofanya ni adui, wanaompenda Mungu na wanaomchukia Mungu ni wapinzani. Wanaoingia rahani na wale ambao wameangamizwa ni aina mbili ya viumbe wasiolingana.
2 Viumbe wanaotimiza wajibu wao watasalimika, na viumbe wasiotimiza wajibu wao wataangamizwa; zaidi ya hayo, hii itadumu milele. Watu leo wana mahusiano ya kimwili miongoni mwao, na pia ushirikiano wa damu, lakini baadaye hii yote itavunjwa. Waumini na wasioamini hawalingani ila wanapingana. Walio rahani wanaamini kwamba kuna Mungu na wanamtii Mungu. Wasiomtii Mungu wote watakuwa wameangamizwa. Familia hazitakuwa tena duniani; kunawezaje kuwa na wazazi na watoto ama mahusiano kati ya waume na wake? Kutoambatana kati ya imani na kutoamini kutakuwa kumevunja haya mahusiano ya kimwili!
Umetoholewa kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili