1001 Matamshi ya Mungu ni Ushawishi Bora kwa Mwanadamu

1 Leo, kazi Nifanyayo ndani yenu inakusudiwa kuwaongoza hadi katika maisha ya ubinadamu wa kawaida; ni kazi ya kukaribisha enzi mpya na ya kuwaongoza wanadamu katika maisha ya enzi mpya. Kazi hii inatekelezwa na kukuzwa miongoni mwenu hatua kwa hatua na moja kwa moja: Nawafunza ana kwa ana; Nawaongoza moja kwa moja; Nawaambia chochote msichokielewa, Nawapa chochote msicho nacho. Inaweza kusemekana kwamba, kwenu, hii kazi yote ni kwa ajili ya ruzuku yenu ya maisha, kuwaongoza pia katika maisha ya ubinadamu wa kawaida; inakusudiwa hasa kuruzuku maisha ya kundi hili la watu wakati wa siku za mwisho.

2 Kazi Nifanyayo miongoni mwenu sasa ni ruzuku yenu ya leo na wokovu wenu wa wakati mzuri, lakini katika miaka hii michache mifupi, Nitawaambia ukweli wote, njia nzima ya maisha, na hata kazi ya siku zijazo; hili litatosha kuwawezesha mpitie mambo kwa njia ya kawaida katika siku zijazo. Nimewaaminia maneno Yangu yote pekee. Sitoi ushawishi mwingine wowote; leo, maneno yote Ninayowazungumzia ni ushawishi Wangu kwenu. Maneno haya ni maono yenu ya leo, na ndiyo mtakayotegemea katika siku zijazo; ni ruzuku ya maisha leo na ushawishi wa siku zijazo, na hakuna ushawishi unaoweza kuwa bora zaidi.

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 1000 Wakati wa Kuachana

Inayofuata: 1002 Mungu Arudipo Sayuni

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp