379 Kumsaliti Mungu ni Asili ya Binadamu

1 Asili ya wanadamu inatoka kwa roho zao; haitoki kwa miili yao. Roho ya kila mtu ndiyo tu inajua jinsi imepitia majaribu, mateso na uovu wa shetani. Mwili wa mwanadamu hauwezi kulifahamu hili. Vivyo hivyo, pasipo kujua mwanadamu anaendelea kuwa mchafu, mwovu na mbaya zaidi na zaidi, ilhali umbali baina Yangu na mwanadamu unaendelea kuongezeka hata zaidi, na siku za mwanadamu zinaendelea kuwa za giza hata zaidi. Roho za wanadamu zote ziko karibu na mikono ya Shetani. Kwa hivyo, ni dhahiri kuwa mwili wa mwanadamu pia umemilikiwa na Shetani. Ingekuwaje miili kama hii na wanadamu kama hawa wasimuasi Mungu na kupatana naye kiasili? Nilimtupa chini Shetani kwa sababu alinisaliti, basi wanadamu wangejinasua vipi kutoka katika matokeo ya hili? Hii ndiyo sababu asili ya mwanadamu ni usaliti.

2 Haijalishi umekuwa mfuasi wake kwa muda gani—asili yako bado ni kumsaliti Mungu. Yaani, ni asili ya watu kumsaliti Mungu kwa sababu watu hawana ukomavu kamili katika maisha yao, wana mabadiliko yanayohusiana tu katika tabia. kupitia kwa sura hizi mbili Mungu anawakumbusha watu wote kwamba haijalishi vile maisha yako yalivyo mapevu, jinsi uzoefu wako ulivyo mkubwa, jinsi imani yako ilivyo, na haijalishi ulikozaliwa na unakokwenda, asili yako ya kumsaliti Mungu inaweza kutokea wakati wowote na mahali popote. Kile Mungu anataka kumwambia kila mtu ni hiki: Kumsaliti Mungu ni asili ya binadamu. Bila shaka kusudi la Mungu katika kuonyesha sura hizi mbili sio kupata visingizio vya kuwaondosha au kuwashutumu wanadamu, lakini ni kuwafanya wawe na ufahamu zaidi kuhusu asili yao wenyewe na hivyo waishi kwa makini zaidi mbele ya Mungu wakati wote ili kupata uongozi Wake, wakiepuka kupoteza uwepo Wake na kuingia kwenye njia isiyoweza kurudi nyuma tena.

Umetoholewa kutoka katika “Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 378 Sababu Ambayo Asili ya Mwanadamu ni Usaliti

Inayofuata: 380 Matokeo Hatari ya Kumsaliti Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

1Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu,kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu.Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa...

125 Nimeuona Upendo wa Mungu

1Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda.Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi!Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

137 Nitampenda Mungu Milele

1Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako.Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku.Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki