Kazi na Kuonekana kwa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 46)

Sifa zimekuja Sayuni na makazi ya Mungu yameonekana. Jina tukufu takatifu linasifiwa na watu wote, na linaenea. Ah, Mwenyezi Mungu! Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—Yeye ni Jua linalong’aa, na Ameinuka juu ya Mlima Sayuni ulio na uadhimu na mzuri kabisa katika ulimwengu mzima …

Mwenyezi Mungu! Sisi tunakushangilia; tunacheza ngoma na kuimba. Kweli Wewe ni Mkombozi wetu, Mfalme mkubwa wa ulimwengu! Umetengeneza kundi la washindi, na kutimiza mpango wa usimamizi wa Mungu. Watu wote wataelekea kwa mlima huu. Watu wote watapiga magoti mbele ya kiti cha enzi! Wewe ndiye Mungu mmoja wa kweli na wa pekee na Unastahili utukufu na heshima. Utukufu wote, sifa, na mamlaka yawe kwa kiti cha enzi! Chemchemi ya maisha hutiririka kutoka kwenye kiti cha enzi, ikinyunyizia na kuwalisha watu wa Mungu. Maisha hubadilika kila siku; nuru mpya na ufunuo hutufuata sisi, daima vikitupatia utambuzi mpya wa Mungu. Kuwa yakini kwa Mungu kupitia uzoefu; maneno Yake daima huonekana, yakionekana kwa wale ambao ni waadilifu. Kwa kweli sisi tumebarikiwa kupita kiasi! Kuwa ana kwa ana na Mungu kila siku, kuwasiliana na Mungu katika kila kitu, na kumpa Mungu mamlaka katika kila kitu. Kwa umakini sisi tunatafakari neno la Mungu, mioyo yetu ni mitulivu katika Mungu, na hivyo sisi tunakuja mbele za Mungu ambapo tunapokea nuru Yake. Katika maisha yetu ya kila siku, matendo, maneno, mawazo, na fikira, tunaishi ndani ya neno la Mungu, na daima tunao utambuzi. Neno la Mungu linapenya; mambo yaliyofichwa ndani kwa ghafula huonekana moja baada ya nyingine. Ushirika na Mungu hauwezi kucheleweshwa; mawazo na fikira huonyeshwa kwa uwazi na Mungu. Kwa kila muda tunaishi mbele ya kiti cha Kristo ambapo sisi hupitia hukumu. Kila eneo la miili yetu linamilikiwa na Shetani. Leo, hekalu la Mungu lazima litakaswe ili Apate ukuu Wake tena. Ili kumilikiwa kabisa na Mungu, ni lazima tupitie vita vya kufa kupona. Ni wakati tu nafsi zetu za zamani zimesulubiwa ndipo maisha ya kufufuliwa ya Kristo yatatawala kwa ukuu.

Sasa Roho Mtakatifu Anafanya shambulio katika kila pembe yetu ili kuzindua vita vya kurudisha! Mradi tuko tayari kujinyima wenyewe na radhi kushirikiana na Mungu, Mungu kwa wakati wowote Ataangaza na kututakasa ndani zetu, na kurudisha upya yale ambayo Shetani amemiliki, ili tuweze kukamilishwa na Mungu haraka iwezekanavyo. Usipoteze muda, na daima uishi ndani ya neno la Mungu. Jengwa pamoja na watakatifu, letwa katika ufalme, na uingie katika utukufu na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 1

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 47)

Kanisa la Filadelfia limechukua umbo, na hili limesababishwa kabisa na neema na rehema za Mungu. Watakatifu wameleta upendo wao wa Mungu mbele na kamwe hawakuyumbayumba kutoka kwa njia yao ya kiroho. Kuwa imara katika imani kwamba Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, ya kwamba Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote—hii imethibitishwa na Roho Mtakatifu na ni ushahidi thabiti! Kamwe hauwezi kubadilika!

Eh, Mwenyezi Mungu! Leo Umefungua macho yetu ya kiroho, kuwaruhusu vipofu kuona, viwete kutembea, wenye ukoma kuponywa. Umefungua dirisha la mbinguni na tumeona siri za dunia ya kiroho. Maneno Yako matakatifu yametujaza sisi, na Umetuokoa kutoka kwa ubinadamu potovu uletwao na Shetani. Hii ni kazi Yako kuu na rehema Yako kubwa sana. Sisi ni mashahidi Wako!

Umekuwa mnyenyekevu na kufichika katika kimya kwa muda mrefu. Wewe umepitia ufufuo na mateso ya msalaba; Wewe umejua furaha na huzuni ya maisha ya binadamu pamoja na mateso na dhiki. Wewe umepitia na kuonja maumivu ya dunia ya binadamu, na Wewe umetelekezwa na enzi. Mungu mwenye mwili ni Mungu Mwenyewe. Wewe umetuokoa kutoka kwa lundo la samadi kwa ajili ya mapenzi ya Mungu na umetushikilia kwa mkono Wako wa kulia; neema Yako imepeanwa huru kwetu sisi. Unafanya juhudi za ukarimu kuingiza maisha Yako ndani yetu; gharama Ulilolipa kwa damu Yako, jasho, na machozi imekuwa katika watakatifu. Sisi ndio matokeo ya[a] juhudi Zako zenye bidii, sisi ndio gharama Unayolipa.

Eh, Mwenyezi Mungu! Ni kwa sababu ya upendo Wako na rehema, haki Yako na uadhama, utakatifu Wako na unyenyekevu kwamba watu wote wanapaswa kutii mbele Yako na kukuabudu Wewe daima dawamu.

Leo Umefanya kamili makanisa yote—kanisa la Filadelfia—ambayo ni matunda ya miaka 6,000 ya mpango Wako wa usimamizi. Sasa watakatifu kwa unyenyekevu wanaweza kuwa watiifu mbele Yako; wao wameunganishwa pamoja katika roho na kuandama pamoja katika upendo. Wao wameunganishwa kwa chanzo cha chemchemi ya maji. Maji ya uhai ya maisha huenda bila mwisho na husafisha na kutakasa uchafu wote na taka katika kanisa, kwa mara nyingine tena yakitakasa hekalu Lako. Tumemjua Mungu wa ukweli wa vitendo, tumetembea ndani ya maneno Yake, tumetambua shughuli zetu na wajibu wetu wenyewe, na kufanya kila kitu tunachoweza kutumia kila rasilmali yetu kwa ajili ya kanisa. Tunapaswa kuchukua kila muda kuwa kimya mbele Yako na kutilia maanani kazi ya Roho Mtakatifu ili mapenzi Yako yasizuiwe ndani yetu. Miongoni mwa watakatifu kuna upendano, na nguvu za wengine zitafidia dosari za wengine. Tembea katika roho kila muda na upate nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu; fahamu ukweli na uuweke katika vitendo mara moja; kuwa sawa na nuru mpya na kufuata nyayo za Mungu.

Shirikiana kwa utendaji na Mungu; kumruhusu Yeye Achukue uongozi ni kutembea pamoja naye. Mawazo yetu yote wenyewe, fikira na maoni, mitego yetu yote ya kimwili, hutokomea kama moshi. Tunamruhusu Mungu Atawale katika roho zetu, kutembea naye na kupata uwezo unaozidi sana wa mwanadamu, kushinda ulimwengu, na roho zetu huruka kwa uhuru na kufikia ufunguliwaji; haya ni matokeo ya Mwenyezi Mungu kuwa Mfalme. Tunawezaje kukosa kucheza ngoma na kuimba sifa, kutoa sifa zetu, na kutoa nyimbo mpya?

Kweli kuna njia nyingi za kumsifu Mungu: kuliita jina Lake, kukaribia karibu na Yeye, kumfikiria Yeye, kuomba kwa kusoma, na kuwa na ushirika, kuzingatia, kutafakari, na sala, na pia kuna nyimbo za sifa. Katika aina hizi za sifa kuna raha, na kuna kupakwa mafuta; kuna nguvu katika sifa na pia kuna mzigo. Kuna imani katika sifa, na kuna utambuzi mpya.

Shirikiana na Mungu kwa utendaji, tumikia kwa uratibu na kuwa moja, yakidhi mapenzi ya Mwenyezi Mungu, harakisha kuwa mwili mtakatifu wa kiroho, kanyaga Shetani, na kumaliza hatima yake. Kanisa la Filadelfia limechukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu na linajidhihirisha katika utukufu wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 2

Tanbihi:

a. Maandishi ya awali hayana maneno “matokeo ya.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 48)

Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Sayuni na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai ndani yao, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi. Kwa hakika Mungu atawahukumu hao, na kwa hakika Atakuwa mwenye hasira nao na mle uadhama wa Mungu utafichuliwa. Hukumu ya aina hiyo itakuwa papo hapo na kuwasilishwa bila kuchelewa. Moto ya ghadhabu ya Mungu itachoma makosa yao ya kuchukiza na janga litawafikia wakati wowote; wao hawatajua njia ya kutoroka na hawatakuwa na mahali pa kujificha, wao watalia na kusaga meno yao, na watajiletea maangamizi.

Wana wa ushindi wapendwa wa Mungu kwa hakika watakaa katika Uyahudi, kamwe wasiiache. Umati utasikiliza sauti Yake kwa makini, watatilia maanani kwa uangalifu matendo Yake, na sauti zao za sifa Kwake kamwe hazitakoma. Mungu mmoja wa kweli Ameonekana! Tutakuwa na uhakika juu Yake katika roho na kumfuata kwa karibu na kukazana kusonga mbele bila kusita. Mwisho wa dunia unajitokeza mbele yetu; maisha sahihi ya kanisa pamoja na watu, shughuli, na mambo ambayo yanatuzunguka sasa hata yanayafanya mafunzo yetu yawe makali zaidi. Acha tufanye hima kuchukua tena mioyo yetu ambayo inapenda dunia sana! Acha tufanye hima kuchukua tena maono yetu yaliyozibwa! Hatutasonga mbele zaidi tusije tukazidi mipaka na tutashikilia ndimi zetu ili tuweze kuishi kwa kufuata neno la Mungu, na tena hatutazozana juu ya faida zetu wenyewe na hasara. Acha upendo wako wa dunia ya kawaida na utajiri! Ah, jiwekeni huru kutoka kwake—upendo wenu wa kuning’nia kwa waume zenu na mabinti na wana wenu! Acha maoni yako na upendeleo! Amka, kwa sababu muda ni mfupi! Iruhusu roho yako iangalie juu, angalia juu na umruhusu Mungu Achukue uongozi. Usijiruhusu kuwa kama mke wa Lutu. Kutelekezwa ni jambo la kusikitisha sana! Ni la kusikitisha kweli! Amka!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 3

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 49)

Milima na mito huenda ikibadilika, vijito hutiririka kwenye mikondo yao, na maisha ya mwanadamu ni yenye uvumilivu mdogo kuliko ardhi na anga. Mwenyezi Mungu pekee ndiye maisha ya milele yaliyofufuka milele, katika vizazi hai milele! Vitu vyote na matukio viko katika mikono Yake, Shetani yuko chini ya miguu Yake.

Leo hii ni kwa sababu ya uteuzi wa Mungu ulioamuliwa kabla kwamba Ametuokoa kutoka kukamatwa na Shetani. Yeye kweli ni Mkombozi wetu. Maisha ya kufufuliwa ya Kristo milele yametugusa ndani yetu, hivi sisi tumejaliwa kuhusiana na maisha ya Mungu, tunaweza kuwa naye ana kwa ana, kumla Yeye, kumnywa Yeye, na kumfurahia Yeye. Huku ni kujitolea kwa Mungu kwa bidi na kusio na ubinafsi.

Majira yanakuja na ku kuenda, yakipitia upepo na jalidi, yakikumbana na taabu, mateso na majonzi mengi sana ya maisha, kukataliwa na kukashifiwa duniani, serikali kusingizia mashtaka, hakuna upungufu wa imani ya Mungu wala kusudi. Kwa ukamilifu kwa ajili ya mapenzi ya Mungu, ili usimamizi wa Mungu na mpango utimizwe, Yeye huweka maisha Yake Mwenyewe kando. Kwa ajili ya watu Wake wote, huwa Hapuri juhudi yoyote, kwa uangalifu Akilisha na kunyunyizia. Haidhuru kiasi cha ujinga, tu wagumu kiasi kipi, tunahitaji tu kutii mbele Yake, na maisha ya kufufuka kwa Kristo yatabadilisha asili yetu ya zamani…. Kwa wana hawa wazaliwa wa kwanza, Yeye hufanya kazi bila kuchoka, huachilia chakula na usingizi. Ni mchana na usiku ngapi, ni kupitia joto ngapi kali, na baridi ya kuganda, Yeye hutazama kwa moyo mmoja katika Sayuni.

Ulimwengu, nyumba, kazi vimeachiliwa kabisa, bila kusita, bila raha za kidunia kumgusa…. Maneno kutoka kinywa Chake yanatupiga kwa ndani, yakifunua mambo yaliofichwa kwenye kina cha mioyo yetu. Ni vipi haturidhishwi? Kila sentensi inayotoka katika kinywa Chake inatendeka wakati wowote kwetu. Kila kitendo chetu, hadharani na faraghani, hakuna ambacho Yeye hakijui, hakuna Asichokijua. Kwa kweli vyote vitafichuliwa mbele Yake, licha ya mipango yetu wenyewe na matayarisho.

Tukiwa tumeketi mbele Yake, roho zetu hufurahia, kustareheshwa na tulivu, daima kuhisi tupu ndani, kwa kweli kuwiwa kwa Mungu. Hili ni jambo la ajabu lisilofikirika na lisiloweza kufanikishwa. Roho Mtakatifu anathibitisha vya kutosha kwamba Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli! Asiyepingika! Sisi, kundi hili la watu, kwa kweli tumebarikiwa! Kama si kwa neema ya Mungu na rehema, lazima tuangamie milele na kumfuata Shetani. Ni Mungu Mwenyezi pekee Anayeweza kutuokoa!

Ah! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo! Ni Wewe ambaye Umefungua macho yetu ya kiroho, kwamba tumeweza kuona siri za dunia ya kiroho. Taswira za ufalme hazina na mwisho. Kuweni waangalifu na wenye kusubiri. Siku haiwezi kuwa mbali sana.

Mioto ya vita huzunguka, moshi wa bunduki huelekea, hali ya hewa huwa vuguvugu, tabia ya nchi hubadilika, tauni litaenea, na watu lazima wafariki, na tumaini ndogo la kuishi.

Ah! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo! Wewe ni mnara wetu imara. Wewe ni kimbilio letu. Sisi tunakusanyika chini ya mabawa Yako, na janga haliwezi kutufikia. Huu ni utunzaji Wako mtakatifu.

Sisi sote tunainua sauti zetu, kuimba sifa, sifa ambazo zinavuma kote Uyahudi! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo ameandaa hatima hio tukufu kwa ajili yetu. Kuwa mwangalifu—mwangalifu! Wakati hauwezi kuwa mbali sana.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 5

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 50)

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu.

Lugha za mataifa mbalimbali ni tofauti na kila nyingine lakini kuna Roho mmoja tu. Huyu Roho huunganisha makanisa kote ulimwenguni na ni mmoja na Mungu, bila tofauti hata kidogo, na hili ni jambo ambalo halina shaka kabisa. Roho Mtakatifu sasa anawapaazia sauti na sauti Yake yawaamsha. Hii ni sauti ya huruma ya Mungu. Wanaliita kwa sauti jina takatifu la Mwenyezi Mungu! Wao pia wanatoa sifa na kuimba. Hakuwezi kuwa na mkengeuko wowote katika kazi ya Roho Mtakatifu, na watu hawa hufanya linalowezekana ili kuendelea kwenye njia sahihi, huwa hawajitoi na maajabu yake hulundikana juu ya maajabu. Ni kitu ambacho watu huona ugumu kufikiria na kisichowezekana kukikisia.

Mwenyezi Mungu ndiye Mfalme wa maisha katika ulimwengu! Yeye huketi juu ya kiti kitukufu cha enzi na huihukumu dunia, huwatawala wote, huyaongoza mataifa yote; watu wote hupiga magoti Kwake, humwomba, huja karibu naye na kuwasiliana na Yeye. Bila kujali muda gani mmemwamini Mungu, jinsi hadhi yenu ilivyo ya juu au jinsi ukubwa wenu wa vyeo ulivyo, kama nyinyi humpinga Mungu katika mioyo yenu basi ni lazima mhukumiwe na lazima msujudu mbele Yake, mkitoa sauti chungu ya kusihi kwenu; huku kweli ni kuvuna matunda ya matendo yenu wenyewe. Sauti hii ya kupiga mayowe ni sauti ya kuteswa katika ziwa la moto na kiberiti, na ni kilio cha kuadibiwa na fimbo ya chuma ya Mungu; hii ndiyo hukumu mbele ya kiti cha Kristo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 8

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 51)

Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiye anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, aliyevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti Yake kama sauti ya maji mengi. Ana nyota saba katika mkono Wake wa kuume, upanga mkali wenye makali kuwili uko katika kinywa Chake na uso Wake ni kama jua liking’aa kwa nguvu zake!

Mwana wa Adamu Ameshuhudiwa, na Mungu Mwenyewe amefichuliwa waziwazi. Utukufu wa Mungu umekuja, uking’aa vikali kama jua lichomalo! Uso Wake mtukufu unawaka kwa mwanga ung’aao; ni macho ya nani yatathubutu kumtendea kwa upinzani? Upinzani husababisha kifo! Hakuna hata chembe ya rehema kwa kitu chochote unachofikiri katika moyo wako, neno lolote usemalo au chochote ufanyacho. Nyinyi nyote mtakuja kuelewa na kuja kuona ni nini ambacho mmekipata—hakuna chochote ila hukumu Yangu! Naweza kukistahimili wakati nyinyi hamuweki juhudi zenu katika kula na kunywa maneno yangu, lakini hudakiza kiholela na kuharibu ujenzi Wangu? Mimi sitamhurumia mtu wa aina hii! Mengine makubwa zaidi na utaangamizwa katika moto! Mwenyezi Mungu hudhihirika katika mwili wa kiroho, bila hata chembe ya mwili au damu ikiunganisha mwili mzima. Yeye huvuka mipaka ya ulimwengu dunia, kama Ameketi kwenye kiti kitukufu cha enzi katika mbingu ya tatu, Akisimamia mambo yote! Ulimwengu na vitu vyote vimo mikononi Mwangu. Kama Nikisema, itakuwa. Kama Nikiliamua, ndivyo litakavyokuwa. Shetani yu chini ya miguu Yangu, yu katika kuzimu! Sauti Yangu itakapotoka, mbingu na nchi zitapita na kuwa bure! Mambo yote yatafanywa upya na huu ni ukweli wa kweli sana usiobadilika. Nimeushinda ulimwengu, kuwashinda waovu wote. Naketi hapa nikizungumza nanyi; wale wote ambao wana masikio wanapaswa kusikiliza na wale wote wanaoishi wanapaswa kukubali.

Siku zitafika mwisho; mambo yote katika dunia yatakuwa bure, na mambo yote yatazaliwa upya. Kumbuka hili! Kumbuka hili! Hapawezi kuwa na utata! Mbingu na nchi zitapita lakini maneno Yangu hayatapita! Acha Niwasihi kwa mara nyingine tena: Msikimbie bure! Amkeni! Tubuni na wokovu umekaribia! Tayari Nimeonekana miongoni mwenu na sauti Yangu imetokea. Sauti yangu imetokea mbele yenu, uso kwa uso na nyinyi kila siku, safi na mpya kila siku. Unaniona Mimi na Ninakuona wewe, Ninasema na wewe mara kwa mara, uso kwa uso na wewe. Na, bado unanikataa Mimi, hunijui Mimi; Kondoo Wangu wasikia sauti Yangu na bado mnasita! Mnasita! Mioyo yenu imepumbaa, macho yenu yamepofushwa na Shetani na hamuwezi kuuona uso Wangu mtukufu—ni kusikitisha kulikoje! Kusikitisha kulikoje!

Roho saba mbele ya kiti Changu cha enzi watumwa kwa kila pembe ya dunia na Mimi Nitamtuma Mjumbe Wangu kuzungumza kwa makanisa. Mimi ni mwenye haki na mwaminifu, Mimi ni Mungu achunguzaye sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mtu. Roho anaongea na makanisa na ni maneno Yangu yanayotiririka kutoka ndani ya Mwanangu; wale wote ambao wana masikio wanapaswa kusikiliza! Wale wote ambao wanaishi wanapaswa kukubali! Yaleni tu na kuyanywa, na msitilie shaka. Wale wote ambao huyatii na kuyasikiza maneno Yangu watapokea baraka kuu! Wale wote wautafutao uso Wangu kwa kweli watapata mwanga mpya kwa hakika, nuru mpya na ufahamu mpya; wote watakuwa wasafi na wapya. Maneno Yangu yataonekana kwako wakati wowote na yatafungua macho ya roho yako ili uweze kuona siri zote za ulimwengu wa kiroho na kwamba ufalme uko miongoni mwa binadamu. Ingia katika hifadhi na neema yote na baraka zitakuwa juu yako, njaa na baa hazitaweza kukugusa, mbwa mwitu, nyoka, chui wakubwa na chui hawataweza kukudhuru. Utaenda na Mimi, utembee na Mimi, na uingie katika utukufu pamoja na Mimi!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 15

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 52)

Mwenyezi Mungu! Mwili Wake mtukufu waonekana wazi wazi, mwili mtakatifu wa kiroho watokea na Yeye ndiye Mungu Mwenyewe kamili! Dunia na mwili vyote vimegeuzwa na mabadiliko Yake juu ya mlima ambaye ni nafsi ya Mungu. Amevaa taji la dhahabu kichwani, mavazi Yake ni meupe kabisa, kifuani ana ukanda wa dhahabu na vitu vyote katika dunia ni mahali pa kuweka miguu yake. Macho Yake ni kama mwale wa moto, na upanga mkali wenye makali kuwili uko ndani ya kinywa Chake na Ana nyota saba katika mkono Wake wa kuume. Njia ya kwenda kwa ufalme ni ng’avu bila kikomo na utukufu Wake watokea na kuangaza; milima huwa na furaha na maji hucheka, jua, mwezi na nyota zote zazunguka kwa mpango wao wa taratibu, ukimkaribisha Mungu wa kweli na wa kipekee, ambaye kurudi kwake kwa ushindi kunaashiria ukamilisho wa miaka elfu sita ya mpango Wake wa usimamizi. Zote zaruka na kucheza kwa furaha! Shangilia! Mwenyezi Mungu amekaa juu ya kiti Chake kitukufu cha enzi! Imbeni! Bendera ya ushindi ya Mwenyezi inainuliwa juu ya mlima mwadhimu, mtukufu wa Sayuni! Mataifa yote yanashangilia, watu wote wa mataifa wanaimba, Mlima Sayuni unacheka kwa furaha, utukufu wa Mungu umetokea! Hata katika ndoto Sijawahi kufikiri kwamba Ningeuona uso wa Mungu lakini leo Nimeuona. Uso kwa uso na Yeye kila siku, nauweka wazi moyo wangu Kwake. Yeye kwa ukarimu hutoa vyote vinavyoliwa na kunywewa. Maisha, maneno, matendo, mawazo, nia—mwanga Wake mtukufu huwatia nuru wote. Yeye huongoza kila hatua ya njia, na kama moyo wowote ni muasi basi hukumu Yake itatokea mara moja.

Kula pamoja na Mungu, kukaa pamoja, kuishi pamoja, kuwa pamoja na Yeye, kutembea pamoja, kufurahia pamoja, kupata utukufu na baraka pamoja, kushiriki ufalme na Mungu, na kuwa pamoja katika ufalme—oo, ni furaha iliyoje! Oo, ni utamu ulioje! Uso kwa uso kila siku, kuzungumza kila siku, kuzungumza mara kwa mara, kupata nuru upya na ufahamu mpya kila siku. Macho yetu ya kiroho yanafunguliwa na tunaona kila kitu, siri zote za kiroho zinafichuliwa kwetu. Maisha matakatifu si ya kujali. Kimbia kwa haraka na usisite, songa mbele mfululizo, kuna maisha ya ajabu zaidi mbele. Usiridhike tu na ladha tamu lakini siku zote tafuta kuingia ndani ya Mungu. Yeye anajumuisha yote na mkarimu, na Ana kila aina ya vitu ambavyo tumekosa. Shirikiana kwa vitendo, ingia ndani Yake na hakuna kitu kitakachokuwa kama awali tena. Maisha yetu yatakuwa ya uvukaji mipaka na hakuna mtu, jambo, au kitu kitakachoweza kutuvuruga.

Uvukaji mipaka! Uvukaji mipaka! Uvukaji mipaka wa kweli! Maisha ya Mungu ya uvukaji mipaka yako karibu na vitu vyote kwa kweli vinakuwa na pumziko! Tunavuka mipaka ya dunia na mambo ya kidunia, hatuhisi upendo kwa waume au watoto. Tunavuka mipaka ya udhibiti wa ugonjwa na mazingira. Shetani hatothubutu kutuvuruga. Kuvuka kabisa mipaka ya maafa yote—hii ni kumruhusu Mungu kuuchukua ufalme! Tunamkanyaga Shetani chini ya miguu, kuwa shahidi kwa ajili ya kanisa na kuifunua kikamilifu sura mbovu ya Shetani. Ujenzi wa kanisa u katika Kristo, mwili mtukufu umetokea—huku ni kuishi katika hali ya kuchukuliwa kuenda mbinguni!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 15

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 53)

Mwenyezi Mungu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani, Mungu wetu Anatawala! Mwenyezi Mungu anaweka miguu Yake kwenye Mlima wa Mizeituni. Uzuri ulioje! Sikiliza! Sisi walinzi tunapaza sauti zetu: tunaimba kwa pamoja kwa sauti zetu, kwa kuwa Mungu amerudi Sayuni. Tunaona kwa macho yetu wenyewe ukiwa wa Yerusalemu. Furahieni na kuimba kwa sauti kwa pamoja, kwa kuwa Mungu ametufariji na Ameukomboa Yerusalemu. Mungu ameweka wazi mkono Wake mtakatifu machoni pa mataifa yote, mtu halisi wa Mungu amejitokeza! Miisho yote ya dunia imeona wokovu wa Mungu wetu.

Ee, Mwenyezi Mungu! Roho saba wametumwa kutoka kwa kiti Chako cha enzi kwa makanisa yote ili kufichua siri Zako zote. Unaketi kwenye kiti Chako cha enzi cha utukufu na Umesimamia ufalme Wako na kuuimarisha na kuushikilia kwa haki; Umeyadhibiti mataifa yote mbele Yako. Ee, Mwenyezi Mungu! Umeilegeza mikanda ya wafalme, Umeyafungua wazi malango ya mji mbele Yako, yasifungike tena. Kwa maana nuru Yako imefika na utukufu Wako unajitokeza na kuangaza uzuri wake. Giza linaifunika dunia na giza totoro imewafunika watu. Ee, Mungu! Hata hivyo, Wewe, umeonekana na kutuangazia mwanga Wako, na utukufu Wako utaonekana kwetu; mataifa yote yatakuja kwa nuru Yako na wafalme kwa upendo Wako. Unayainua macho Yako na kuangalia kila mahali: Wana Wako wanakusanyika mbele Yako, na wanatoka mbali; Mabinti Zako wanabebwa mikononi. Ee, Mwenyezi Mungu! Upendo Wako mkubwa umetushika; ni Wewe unayetuongoza mbele kwenye njia inayouelekea ufalme Wako na ni maneno Yako matakatifu yanayopenya na kuenea ndani mwetu.

Ee, Mwenyezi Mungu! Tunakushukuru na kukusifu! Hebu tukuheshimu, tukushuhudie, tukusifu, na kukuimbia kwa mioyo safi, yenye utulivu, na thabiti. Hebu tuwe na akili moja na kujengwa pamoja, na Utufanye tuwe wanaoupendeza moyo Wako hivi karibuni, wanaotumika na Wewe. Tunatamani kwamba mapenzi Yako yatekelezwe katika nchi yote bila kuzuiwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 25

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 54)

Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu zote, mwenye kutimiliza yote na Mungu wa kweli mkamilifu! Habebi tu nyota saba, ana Roho saba, ana macho saba, anafungua mihuri saba na kufungua hati ya kukunja yenye maandishi, lakini zaidi ya hayo Yeye anaendesha mapigo saba na vitasa saba na kufungua radi saba; zamani za kale Yeye alipiga vinumbi saba! Vitu vyote vilivyoumbwa na kufanywa kuwa kamili na Yeye vinapaswa kumsifu, kumpa adhama na kutukuza kiti Chake cha enzi. Ee, Mwenyezi Mungu! Wewe ni kila kitu, Wewe umetimiza kila kitu, na kila kitu kinakamilika na Wewe, vyote vinang’aa, vyote vimekombolewa, vyote viko huru, vyote viko imara na vyenye nguvu! Hakuna chochote kilichofichwa wala kufungwa, na Wewe mafumbo yote yanafumbuliwa. Aidha, Wewe unahukumu halaiki za adui Zako, unaonyesha uadhama Wako, unaonyesha moto Wako unaoendelea vikali, unaonyesha ghadhabu Yako, na hata zaidi Unaonyesha utukufu Wako ambao haujawahi kuonekana awali, wa milele na usio na mwisho! Watu wote wanapaswa kuamka na wanapaswa kushangilia na kuimba bila kusita, wakihimidi mwenye Uweza, yule wa kweli, anayeishi, mkarimu, adhimu na Mungu wa kweli aliye kutoka milele hadi milele. Kiti Chake cha enzi kinapasa kutukuzwa kila wakati, jina Lake takatifu kusifiwa na kutukuzwa. Haya ni mapenzi Yangu—ya Mungu—ya milele na ni baraka zisizo na mwisho ambazo Yeye hutufichulia na kutukarimia! Je, ni nani kati yetu ambaye hairithi? Ili kurithi baraka za Mungu, mtu lazima alitukuze jina takatifu la Mungu na kuja kumwabudu kwa kuzunguka kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wanaenda mbele Yake wakiwa na nia nyingine na dhamira nyingine wanayeyushwa na moto Wake wenye ghadhabu. Leo ni siku ambayo adui Zake watahukumiwa, na pia wataangamia katika siku hii. Hata zaidi ni siku ambayo Mimi, Mwenyezi Mungu, nitafunuliwa na Nitapokea utukufu na heshima. Enyi, watu wote! Inukeni haraka ili mhimidi na kumkaribisha Mwenyezi Mungu ambaye milele na milele hutupa wema wenye upendo, wokovu, na kutupa baraka, huwafanya wana Wake kuwa wakamilifu na kufikia ufalme Wake kwa mafanikio! Hili ni tendo la ajabu la Mungu! Haya ni majaaliwa na mipango ya milele ya Mungu, kwamba Yeye Mwenyewe aje kutuokoa, kutufanya tuwe wakamilifu na kutuleta kwenye utukufu.

Wale wote ambao hawainuki na kuwa na ushuhuda ni wahenga wa vipofu, wafalme wa wasiojua na watakuwa daima wasiojua, wajinga wa milele na vipofu waliokufa daima. Kwa hivyo nafsi zetu zinapasa kuamka! Watu wote wanapaswa kuinuka! Mshangilie, msifu na kumhimidi Mfalme wa utukufu, Baba wa huruma, Mwana wa ukombozi bila kikomo, Roho saba zenye ukarimu, na Mwenyezi Mungu anayeleta moto adhimu wenye ghadhabu na hukumu yenye haki, anayejitosheleza, mkarimu, mwenye Uweza, na mkamilifu. Kiti Chake cha enzi kitatukuzwa milele! Watu wote wanafaa kuona kwamba hii ni hekima ya Mungu, ni njia Yake ya shani ya wokovu, na utimilifu wa mapenzi Yake yenye utukufu. Tusipoinuka na kuwa na ushuhuda, wakati muda utakapokwisha basi hakutakuwa na kurudi nyuma. Iwapo tunapokea baraka au balaa inaamuliwa katika hatua hii iliopo ya safari yetu, kulingana na tunayotenda, kufikiria au kuishi wakati huu. Basi mnapaswa kutenda yapi? Mshuhudieni na kumtukuza Mungu milele; mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho—Mungu wa kweli, wa kipekee, na wa milele!

Kuanzia sasa kuendelea unapaswa kuona wazi kuwa wale wote wasiokuwa na ushuhuda kwa Mungu, wasiokuwa na ushuhuda kwa wale wa kipekee, waaminifu kwa Mungu, wale walio na tashwishi kumhusu, wote ni wagonjwa, wafu na wenye kumuasi Mungu! Maneno ya Mungu yamehakikishwa kutoka nyakati za kale: Wale wote ambao hawakusanyiki na Mimi wanatawanyika, na wale wasio upande Wangu wako dhidi Yangu; huu ni ukweli usioweza kubadilishwa uliochongwa jiweni! Wale wasiokuwa na ushuhuda kwa Mungu ni vikaragosi wa Shetani. Watu hawa huja kuwasumbua na kuwadanganya watoto wa Mungu, kukatiza usimamizi wa Mungu, na sharti wawekwe kwenye upanga! Yeyote anayewaonyesha nia nzuri anatafuta maangamizi yake mwenyewe. Unapaswa kusikiza na kuamini tamko la Roho wa Mungu, kutembea kwenye njia ya Roho wa Mungu na kuishi kwa maneno ya Roho wa Mungu, na hata zaidi kusifu kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu milele!

Mwenyezi Mungu ni Mungu wa Roho saba! Yule wa macho saba na nyota saba ndiye Yeye pia; Yeye hufungua mihuri saba, na hati nzima ya kukunja imekunjuliwa na Yeye! Amepiga baragumu saba, na vitasa saba na mapigo saba yako mikononi Mwake, yatakayofunguliwa kwa mapenzi Yake. Ee, ngurumo saba ambazo daima zimefungwa! Wakati wa kuzifungua umewadia! Yule atakayezifungua ngurumo saba tayari ameshaonekana mbele ya macho yetu!

Mwenyezi Mungu! Kila kitu kimekombolewa na kuwa huru na Wewe, hapana ugumu, na kila kitu kinakwenda vizuri! Hakuna kinachothubutu kukupinga au kukuzuia Wewe, vyote hukutii. Chochote kisichotii hufa!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye macho saba! Vyote viko wazi vikamilifu, vyote ni ng’avu na wazi, vyote vimefunuliwa na kuwekwa wazi. Vyote ni dhahiri kabisa na Yeye, na si tu kuwa Mungu Mwenyewe yuko hivi, lakini pia wana Wake wako hivi vilevile. Hapana yeyote, hakuna kitu chochote, na hakuna hoja yoyote inayoweza kufichwa mbele Yake na wana Wake!

Nyota saba za Mwenyezi Mungu ni ng’avu bashashi! Kanisa limefanywa kuwa kamili na Yeye, Yeye huweka imara mitume wa kanisa Lake na kanisa lote liko ndani ya utoaji Wake. Yeye anafungua mihuri yote saba, na Yeye Mwenyewe analeta mpango wa usimamizi Wake na mapenzi Yake hadi tamati. Hati ndiyo kunga ya lugha ya kiroho ya usimamizi Wake na Amekifungua na kukifunua!

Watu wote wanapaswa kusikiliza baragumu Zake saba zinazopigwa kwa sauti. Kwake, vyote vinajulishwa, kamwe visifichike tena, na hakuna huzuni tena. Vyote vinafunuliwa, na vyote vinashinda!

Baragumu saba za Mwenyezi Mungu ziko wazi, baragumu adhimu na zenye ushindi! Pia ni baragumu zinazowahukumu adui Zake! Katikati ya ushindi Wake, baragumu Yake inatukuzwa! Yeye hutawala ulimwengu mzima!

Yeye amevitayarisha vitasa saba vya mapigo na vyote vinafunguliwa kwa nguvu kabisa kwa adui Zake kwa kiwango cha juu, na watateketea kwa miale ya moto Wake wenye ghadhabu. Mwenyezi Mungu huonyesha uwezo wa mamlaka Yake na adui Zake wote wanaangamia. Ngurumo saba za mwisho hazitafichwa tena mbele ya Mwenyezi Mungu, zote ziko wazi! Zote ziko wazi! Yeye huwaua adui Zake kwa ngurumo saba, Akiimarisha dunia, Akiifanya imtolee huduma, kamwe kutokuwa isiyofaa!

Mwenyezi Mungu mwenye haki! Tunakutukuza milele! Unastahili sifa zisizoisha, kuhimidiwa kusikoisha na kutukuzwa! Ngurumo Zako saba si tu za hukumu Yako, bali zaidi ni kwa ajili ya utukufu na mamlaka Yako, ili kukamilisha vitu vyote!

Watu wote wanasherehekea mbele ya kiti cha enzi, wakimtukuza na kumsifu Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho! Sauti zao zinautikisa ulimwengu mzima kama radi! Bila shaka vitu vyote vinakuwepo kwa ajili Yake, na kuinuka kwa ajili Yake. Je, ni nani anayethubutu kutoona utukufu, heshima, mamlaka, hekima, utakatifu, ushindi na ufunuo kuwa sio Zake? Huu ndio utimizaji wa mapenzi Yake na ndio ukamilishaji wa mwisho wa ujenzi wa usimamizi Wake!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 34

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 55)

Ngurumo saba zinatoka katika kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinazipindua mbingu na dunia, na zinaenea kote angani! Sauti hiyo inapenya sana kiasi kwamba watu hawawezi kuepuka wala kujificha kutoka kwayo. Nuru za umeme na ngurumo zinatolewa, mbingu na nchi zinabadilishwa mara moja, na watu wako karibu kufa. Kisha, dhoruba kali sana ya mvua inaufagilia mbali ulimwengu wote kwa haraka sana, ikinyesha kutoka angani! Katika pembe za mwisho kabisa za dunia, kama mvua inayopita katika kila pembe, hakuna waa hata moja linalobaki, na inapofagia vitu vyote toka utosini hadi kidoleni, hakuna kitu kinachofichwa kutoka kwayo wala hakuna mtu yeyote anayeweza kuiepuka. Kama kiasi kidogo chenye baridi cha nuru za umeme, ngurumo zinawafanya watu kutetemeka kwa hofu! Upanga mkali wa kukata kuwili unawaangamiza wana wa uasi, naye adui anakabiliwa na janga, pasipo na popote pa kujificha; wanachanganyikiwa wanapokumbwa na upepo na mvua mkali, na huku wakishtushwa na pigo, wanakufa mara moja ndani ya maji yanayotiririka na kufagiliwa na maji. Wanakufa tu bila namna yoyote ya kuyaokoa maisha yao. Ngurumo saba zinatoka Kwangu nazo zinawasilisha nia Yangu, ambayo ni kuwaangamiza wana wakubwa wa Misri, kuwaadhibu waovu na kuyasafisha makanisa Yangu, ili wote wapendane sana, wafikirie na kutenda kwa njia sawa, na wawe na nia moja nami, na ili makanisa yote katika ulimwengu yaweze kujengwa na kuwa kanisa moja. Hili ni kusudi Langu.

Ngurumo inaposikika, sauti za kuomboleza zinatokea ghafla. Wengine wanaamka kutoka katika usingizi wao, na, wakiwa wameshtuka sana, wao wanachunguza nafsi zao na kukimbia mara moja mbele ya kiti cha enzi. Wanakoma kufanya hila na kudanganya na kufanya uhalifu, nami Sijachelewa sana kuwaamsha watu kama hao. Naangalia kutoka katika kiti cha enzi. Natazama ndani ya mioyo ya watu. Nawaokoa wale ambao wanitamani sana kwa dhati na kwa ari, nami Ninawahurumia. Nitawaokoa milele wale wanaonipenda mioyoni mwao zaidi ya vingine vyote, wale wanaoyaelewa mapenzi Yangu, na ambao wananifuata hadi mwisho. Mkono Wangu utawashikilia salama ili wasiweze kukabiliana na mandhari haya na hawatapatwa na madhara yoyote. Baadhi, wanapouona umeme huu wenye nuru, wana taabu isiyoelezeka mioyoni mwao na wanajuta kupindukia. Wakiendelea kutenda kwa njia hii, watakuwa wamechelewa sana kusaidika. Ee, yote na kila kitu! Yote yatafanyika. Hii pia ni moja ya njia Zangu za wokovu. Nawaokoa wale wanaonipenda na kuwaangamiza waovu. Kwa hiyo ufalme Wangu utakuwa thabiti na imara duniani na mataifa yote na watu wote, wote ulimwenguni na katika miisho ya dunia, wanajua kwamba Mimi ni uadhama, Mimi ni moto wenye ghadhabu, Mimi ni Mungu anayeutafuta moyo wa ndani kabisa wa kila mtu. Kutoka wakati huu na kuendelea, hukumu ya kiti cha enzi cheupe kikuu imefunuliwa waziwazi kwa raia na imetangazwa kwa watu wote kuwa hukumu imeanza! Bila shaka, wote ambao hawaneni yaliyo mioyoni mwao, wale wanaohisi kuwa na wasiwasi na hawathubutu kuwa na hakika, wale ambao hupoteza wakati, ambao wanayaelewa mapenzi Yangu lakini hawako radhi kuyatenda, sharti wahukumiwe. Lazima mchunguze kwa makini makusudi na nia zenu wenyewe, na mchukue nafasi yenu inayofaa, fanyieni mazoezi kabisa kile Ninachosema, kazieni umuhimu uzoefu wenu wa maisha, msitende kwa shauku kwa nje, lakini yafanyeni maisha yenu yakue, yakomae, yawe imara na yenye uzoefu, na kwa njia hiyo tu ndipo mtaupendeza moyo Wangu.

Wakane vikaragosi wa Shetani na pepo wabaya ambao wanavuruga na kuharibu yale ambayo Ninaunda fursa za kutumia vitu kwa manufaa yao. Lazima wakomeshwe na kuzuiwa kwa ukali na wanaweza tu kushughulikiwa kupitia matumizi ya mapanga makali. Wale walio wabaya zaidi lazima waangamizwe mara moja ili wasiwe tishio katika siku zijazo. Nalo kanisa litakamilishwa, litaondolewa ulemavu wote, nalo litakuwa na afya nzuri, lililojaa uhai na nguvu. Baada ya umeme wenye nuru, radi zinavuma. Hampaswi kupuuza, hampaswi kukata tamaa lakini mfanye kila mwezalo ili mfikie, na hakika mtaweza kuona kile mkono Wangu unachofanya, kile Ninachopata, kile Ninachoacha, kile Ninachokamilisha, kile Ninachoondoa kabisa, kile Ninachoangamiza. Yote haya yatatokea mbele ya macho yenu ili mweze kuona wazi kabisa uweza Wangu.

Kutoka katika kiti cha enzi hadi ulimwengu na miisho ya dunia, ngurumo saba zinasikika. Kikundi kikubwa cha watu kitaokolewa na kutii mbele ya kiti Changu cha enzi. Baada ya huu mwanga wa uzima, watu wanatafuta njia ya kuishi nao hawana budi kuja Kwangu, kupiga magoti katika ibada, midomo yao inaliita jina la Mwenyezi Mungu wa kweli, na kueleza kusihi kwao. Lakini kwa wale wanaonipinga Mimi, watu wanaoishupaza mioyo yao, radi inavuma masikioni mwao na bila shaka sharti waangamie. Haya hasa ni matokeo ya mwisho kwao. Wana Wangu wapendwa ambao ni washindi watakaa Sayuni na watu wote wataona kile watakachokipata, na utukufu mkubwa utatokea mbele yenu. Kwa kweli, hii ni baraka kubwa sana, na ni uzuri ambao ni mgumu kusimulia.

Wakati ambapo sauti za ngurumo saba zinatoka, kuna wokovu wa wale wanaonipenda Mimi, wanaonitamani kwa mioyo ya kweli. Wale wote ambao ni Wangu na ambao Nimewajaalia na kuwachagua wanaweza kuja chini ya jina Langu. Wanaweza kusikia sauti Yangu, ambayo ni wito wa Mungu. Acha wale walio katika miisho ya dunia waone kwamba Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ni upendo, Mimi ni huruma, Mimi ni uadhama, Mimi ni moto wenye ghadhabu, na hatimaye Mimi ni hukumu isiyo na huruma.

Acha wote ulimwenguni waone kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe halisi na kamili. Watu wote wanaamini kabisa na hakuna mtu anayethubutu kunipinga tena, kunihukumu au kunikashifu tena. Vinginevyo, watakumbana na laana mara moja na msiba utawafika. Watalia na kusaga meno yao tu na watasababisha uharibifu wao wenyewe.

Wacha watu wote wajue, wacha ijulikane katika ulimwengu mzima na katika miisho ya dunia, katika kila nyumba na kwa watu wote: Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli. Kila mmoja atapiga magoti ili kumwabudu Yeye na hata watoto ambao wamejifunza tu kuzungumza wataita “Mwenyezi Mungu”! Maofisa hao wenye mamlaka watamwona kwa macho yao wenyewe Mungu wa kweli akiwa mbele yao na pia watasujudu katika ibada, wakiomba huruma na msamaha, lakini kweli wamechelewa sana kusaidika, kwani muda wao wa kufa umefika. Wanaweza tu kuangamizwa na kuhukumiwa kuelekea kwenye lindi la kina kirefu sana. Nitaikomesha enzi yote, na kuimarisha ufalme Wangu zaidi. Mataifa na watu wote watatii mbele Yangu milele yote!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 35

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 56)

Mwenyezi Mungu wa kweli, Mfalme katika kiti cha enzi, hutawala ulimwengu mzima, Anakabiliana na mataifa yote na watu wote, na kila kitu chini ya mbingu hung'aa kwa utukufu wa Mungu. Viumbe vyote hai katika ulimwengu na hadi miisho ya dunia vitaona. Milima, mito, maziwa, ardhi, bahari, na viumbe vyote viishivyo, katika nuru ya uso wa Mungu wa kweli, na wamesisimka kana kwamba wameamka kutoka ndotoni, kana kwamba wao ni chipuko zinazochipuka kutoka mchangani!

Ah! Mungu mmoja wa kweli, Huonekana mbele ya dunia. Je, nani anathubutu kumtendea kwa upinzani? Kila mmoja hutetemeka kwa hofu. Hakuna ambao hawajaridhishwa kabisa, mara kwa mara kuomba msamaha, wote kwa magoti yao mbele Yake, vinywa vyote vikimuabudu! Mabara na bahari, milima, mito, vitu vyote kumsifu bila kikomo! Vuguvugu la upepo mwanana wa masika huja na masika kuleta mvua mzuri wa masika. Kama watu wote, mikondo ya mito hutiririka kwa huzuni na furaha, ikitoa machozi ya kuwiwa na kujilaumu. Mito, maziwa, chafuko na mawimbi, yote yanaimba, yakihimidi jina takatifu la Mungu Wa kweli! Sifa hizi zinavuma kwa wazi sana! Mambo yote ya zamani ambayo kwa wakati mmoja yalikuwa yamepotoshwa na Shetani, kila mmoja atafanyia upya, atabadilika, na kuingia katika hali mpya kabisa …

Hili ni tarumbeta takatifu linasikika! Sikiliza. Sauti hiyo, tamu sana, ni kiti cha enzi kinatoa mlio, kutangaza kwa mataifa yote na watu, wakati umefika, hatima ya mwisho imefika. Mpango Wangu wa usimamizi umemalizika. Ufalme Wangu huonekana hadharani duniani. Falme za duniani zimekuwa ufalme—wa Mungu—Wangu. Matarumbeta Yangu saba yanasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, na ni maajabu gani yatatokea! Watu katika miisho ya dunia watakurupuka pamoja kutoka kila upande kwa nguvu ya lundo na uwezo wa radi. …

Hufurahia kuona watu Wangu, ambao husikia sauti Yangu, na kukusanyika kutoka kila taifa na nchi. Watu wote, uhifadhi Mungu wa kweli daima katika midomo yao, kusifu na kuruka kwa furaha bila kukoma! Wao huushuhudia kwa ulimwengu, na sauti ya ushuhuda wao kwa Mungu wa kweli ni kama sauti ya ngurumo ya maji mengi. Watu wote watasongamana katika ufalme Wangu.

Matarumbeta Yangu saba yatapaza sauti, kuamsha walio lala! Shughulika kwa haraka, muda hujakwisha. Angalia maisha yako! Fungua macho yako na uone ni wakati upi sasa. Ni nini unatafuta? Kuna nini ya kufikiri? Na ni nini kilicho cha kushikilia? Je, inawezekana kuwa bado hujafikiria tofauti katika thamani kati ya kupata maisha Yangu na mambo yote unayopenda na kushikilia? Acha kuwa makaidi na kucheza kila mahali. Usikose nafasi hii. Wakati huu hautakuja tena! Simama mara moja, tenda kufanyisha roho yako mazoezi, kutumia zana mbalimbali kukuwezesha na kuzuia kila njama na hila za Shetani, na umshinde Shetani, ili kwamba uzeofu wako wa maisha uweze kuwa wa kina zaidi na uweze kuishi kwa kudhihirisha tabia Yangu, ili maisha yako yaweze kukomaa na yawe yenye tajriba na ili uweze daima kufuata nyayo Zangu. Ukiwa bila hofu, ukiwa usiye udhaifu, daima ukisonga mbele, hatua kwa hatua, moja kwa moja hadi mwisho wa njia!

Wakati matarumbeta saba zitatoa sauti tena, itakuwa mwito wa hukumu, hukumu ya wana wa uasi, hukumu ya mataifa yote na watu wote, na kila taifa litajisalimisha mbele ya Mungu. Uso wa utukufu wa Mungu hakika utaonyeshwa mbele ya mataifa yote na watu wote. Kila mtu atakuwa ameridhishwa kabisa, kupiga kelele kwa Mungu wa kweli bila kikomo. Mwenyezi Mungu Atakuwa Mtukufu zaidi, na wanangu watashiriki katika utukufu, kushiriki ufalme nami, kuhukumu mataifa yote na watu wote, kuadhibu maovu, kuokoa na kuwa na huruma juu ya watu ambao ni Wangu, kuleta uthabiti na utulivu kwa ufalme. Kupitia sauti ya matarumbeta saba, kundi kubwa la watu litaokolewa, kurudi mbele Yangu kupiga magoti na kuabudu, kwa sifa daima!

Wakati matarumbeta saba zitatoa sauti mara nyingine tena, hilo litakuwa tukio la hitimisho la mwisho wa enzi, mlipuko wa sauti wa tarumbeta ya ushindi dhidi ya ibilisi Shetani, saluti katika mwanzo wa maisha ya wazi wa ufalme duniani! Sauti hii ya kifahari sana, sauti hii inayonguruma pande zote za kiti cha enzi, mlipuko wa sauti ya tarumbeta inayotikisa mbingu na dunia, ni ishara ya mpango Wangu wa usimamizi, na hukumu ya Shetani, kuadhibu duniani hii ya zamani kwa kifo kabisa, jahanamu! Huu mlipuko wa sauti ya tarumbeta unaashiria kwamba lango la neema ni linafungika, kwamba uhai wa ufalme utaanza duniani, ambayo ni kamilifu kabisa. Mungu Huokoa wale wanaompenda. Mara tu watakaporudi kwa ufalme Wake, watu duniani watakabili njaa, ndwele ya kufisha, na mabakuli saba ya Mungu, tauni saba zitaanza kutumika kwa mfululizo. Mbingu na dunia zitapita, lakini neno Langu halitapita!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 36

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 57)

Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo kwayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na maandiko, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hiyo ni kwa sababu yote walio nayo ni maji machafu ambayo yameshikiliwa kwa maelfu ya miaka badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi. Wale ambao hawajaruzukiwa maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya kuchezewa na Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za Mwanakondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambazo zisizoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, sembuse njia zinazoweza kukuongoza kuelekea kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa acha kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.

Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 58)

Kwamba siri Zangu zinafichuliwa na zinadhihirika wazi, na hazifichiki tena, ni kwa sababu ya neema na rehema Zangu kabisa. Zaidi ya hayo, kwamba neno Langu linaonekana kati ya wanadamu, na halifichiki tena, nako pia ni kwa sababu ya neema na rehema Zangu. Ninawapenda wote wanaojitumia na kujitoa wenyewe kwa dhati kwa ajili Yangu. Nawachukia wale wote waliozaliwa kutoka Kwangu ila bado hawanijui Mimi, na hata wananipinga Mimi. Sitamwacha yeyote ambaye kwa dhati yuko kwa ajili Yangu; badala yake, baraka zake Nitazifanya ziwe mara dufu. Nitawaadhibu mara dufu wale wasio na shukrani na wanaokiuka fadhila Zangu, na sitawaachilia kwa urahisi. Katika ufalme Wangu hakuna upotovu au udanganyifu, na hakuna udunia; yaani, hakuna harufu ya wafu. Badala yake, yote ni unyofu na haki; yote ni usafi na uwazi, bila kuwa na chochote kilichofichika au kisicho wazi. Kila kitu ni kipya, kila kitu ni starehe, na kila kitu ni cha kujenga. Yeyote ambaye bado ananuka wafu hawezi kamwe kubakia katika ufalme Wangu, na badala yake atatawaliwa na fimbo Yangu ya chuma. Siri zote zisizo na mwisho, tangu zamani sana hadi sasa, zinafichuliwa kikamilifu kwenu—kundi la watu ambao wanapatwa na mimi katika siku za mwisho. Je, hamhisi kuwa mmebarikiwa? Zaidi ya hayo, siku ambazo yote yanafunuliwa wazi, ni siku ambazo mtashiriki utawala Wangu.

Kundi la watu ambao kwa kweli hutawala kama wafalme hutegemea majaliwa na uchaguzi Wangu, na kamwe hakuna mapenzi ya mwanadamu ndani yake. Yeyote anayethubutu kushiriki katika hili lazima apate pigo kutoka kwa mkono Wangu, na watu kama hao watakabiliwa na moto Wangu mkali; huu ni upande mwingine wa haki na uadhama Wangu. Nimeshasema kwamba ninatawala vitu vyote, mimi ndiye Mungu mwenye hekima ambaye ana mamlaka kamili, na Sina huruma kwa mtu yeyote; Mimi ni katili kabisa, sina hisia za kibinafsi kamwe. Ninamtendea mtu yeyote (haijalishi anaongea vizuri namna gani, Sitamwachilia) kwa haki, uadilifu na uadhama Wangu, wakati huohuo Nikimwezesha kila mtu kuona maajabu ya matendo Yangu vizuri zaidi, na vilevile maana ya matendo Yangu. Mmoja baada ya mwingine, Niliwaadhibu pepo wabaya kwa kila aina ya matendo wanayotenda, nikiwatupa kila mmoja ndani ya shimo lisilo na mwisho. Kazi hii Niliimaliza kabla ya wakati kuanza, nikawaacha bila nafasi, nikiwaacha bila mahali pa kufanya kazi yao. Hakuna hata mmoja wa watu Wangu wateule—wale waliojaliwa na kuchaguliwa na Mimi—anayeweza kupagawa kamwe na roho waovu, na badala yake atakuwa mtakatifu daima. Lakini kwa wale ambao Sijawajalia na kuwachagua, Nitawakabidhi kwa Shetani, na sitaruhusu wabakie tena. Katika vipengele vyote, amri Zangu za kiutawala zinajumuisha haki Yangu na uadhama Wangu. Sitamwachilia hata mmoja wa wale ambao Shetani anatenda kazi kwao, lakini nitawatupa pamoja na miili yao kuzimuni, kwa maana namchukia Shetani. Sitamwachilia kwa urahisi hata kidogo, lakini nitamwangamiza kabisa, nisimruhusu hata fursa ndogo kabisa kufanya kazi yake. Wale ambao Shetani amewapotosha kwa kiwango fulani (yaani, wale ambao watakabiliwa na maafa) wako chini ya mpangilio wa hekima wa mkono Wangu. Msidhani kwamba hili limetokea kwa sababu ya ukali wa Shetani; jueni kuwa Mimi ni Mwenyezi Mungu anayetawala ulimwengu na vitu vyote! Kwangu Mimi, hakuna matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa, sembuse kitu ambacho hakiwezi kukamilishwa au neno lolote ambalo haliwezi kusemwa. Wanadamu hawapaswi kutenda kama washauri Wangu. Jihadharini na kuangushwa na mkono Wangu na kutupwa kuzimuni. Nakuambia hili! Wale ambao wanashirikiana na Mimi leo kwa vitendo ndio werevu kupita wote, na wataepuka hasara na kukwepa maumivu ya hukumu. Yote haya ni mipangilio Yangu, iliyojaliwa na Mimi. Usitoe matamshi yasiyo na busara na usizungumze maneno matupu, ukidhani wewe ni mkuu sana. Je, yote haya hayatokani na majaliwa Yangu? Ninyi, ambao mnataka kuwa washauri Wangu, hamwoni aibu! Hamjui kimo chenu wenyewe; jinsi kilivyo kidogo kiasi cha kusikitisha! Hata hivyo, mnafikiri hili silo jambo kubwa, na hamjijui wenyewe. Tena na tena, mnayapuuza maneno Yangu, na kusababisha juhudi Zangu kubwa kuwa za bure na hamgundui hata kidogo kuwa ni udhihirisho wa neema na rehema Zangu. Badala yake, mnajaribu kuonyesha ujanja wenu tena na tena. Mnakumbuka hili? Je, ni adhabu gani ambayo watu ambao wanafikiri ni wajanja sana wanapaswa kupokea? Mkiwa wasiojali na wasio waaminifu kwa maneno Yangu, na msioyaandika mioyoni mwenu, mnanitumia Mimi kama kisingizio cha kufanya hivi na vile. Watenda mabaya! Je, ni lini ambapo mtaweza kuufikiria moyo Wangu kikamilifu? Hamuuzingatii, kwa hivyo kuwaita “watenda maovu” sio kuwatendea vibaya. Inawastahili kabisa!

Leo Ninawaonyesha, moja baada ya jingine, mambo ambayo zamani yalikuwa yamefichika. Joka kubwa jekundu limetupwa ndani ya shimo lisilo na mwisho na kuangamizwa kabisa, maana kuendelea kuliweka hakutakuwa na faida kabisa; hii inamaanisha kuwa haliwezi kumhudumia Kristo. Baada ya hapa, vitu vya rangi nyekundu havitakuwapo tena; hatua kwa hatua, lazima vipotee kabisa. Ninatenda kile Ninachosema; huku ndiko kukamilika kwa kazi Yangu. Ondoeni fikira za kibinadamu; kila kitu ambacho Nimesema, nimefanya. Yeyote anayejaribu kuwa mjanja hujiletea uangamizi na dharau, na hataki kuishi. Kwa hivyo, Nitakuridhisha, na hakika sitawaweka watu kama hao. Baada ya hapa, idadi ya watu itaongezeka katika ubora, ilhali wote ambao hawashirikiana na Mimi kwa vitendo wataangamizwa kabisa. Wale ambao Nimewaidhinisha ndio ambao Nitawakamilisha, na sitamtupa hata mmoja. Hakuna ukinzani katika kile Ninachosema. Wale ambao hawashirikiani na Mimi kwa vitendo watapata adhabu zaidi, ingawa mwishowe, hakika nitawaokoa. Hata hivyo, kufikia wakati huo, kiwango cha maisha yao kitakuwa tofauti kabisa. Je, wewe unataka kuwa mtu kama huyo? Inuka na ushirikiane na Mimi! Hakika Sitamtendea vibaya yeyote anayejitumia kwa dhati kwa ajili Yangu. Kwa wale wanaojitolea Kwangu kwa bidii, Nitawapa baraka Zangu zote. Jitoe kikamilifu Kwangu! Kile unachokula, kile unachovaa, na siku zako zijazo vyote viko mikononi Mwangu; Nitapangilia kila kitu sawasawa, ili uwe na starehe isiyo na mwisho, ambayo hutaimaliza kamwe. Hii ni kwa sababu Nimesema, “Kwa wale ambao wanatumia rasilmali zao kwa ajili Yangu kwa dhati, hakika Nitakubariki sana.” Baraka zote zitakuja kwa kila mtu anayejitumia kwa dhati kwa ajili Yangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 70

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 59)

Umati unanishangilia, umati unanisifu; watu wote wanalitaja jina la Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanayainua macho yao kuviangalia vitendo Vyangu. Ufalme unashuka katika dunia ya wanadamu, nafsi Yangu ni ya fahari na yenye neema. Nani asingesherehekea kwa ajili ya hili? Ni nani asingecheza kwa ajili furaha? Ee Sayuni! Inua bendera yako ya ushindi unisherehekee! Imba wimbo wako wa ushindi ili ulieneze jina Langu takatifu! Viumbe wote hadi miisho ya dunia! Harakisheni kujitakasa ili muweze kufanywa kuwa sadaka Kwangu! Nyota juu mbinguni! Rudini kwenye maeneo yenu kwa haraka ili muonyeshe nguvu Yangu kuu katika anga! Nazisikiliza sauti za watu duniani, wanaomimina upendo na uchaji wao mwingi kwa ajili Yangu kwa nyimbo! Katika siku hii, huku viumbe wote wakirudishiwa uhai, Nashuka katika dunia ya wanadamu. Katika wakati huu, mambo yalivyo, maua yanachanua kwa wingi, ndege wote wanaimba kwa sauti moja, vitu vyote vinajawa na furaha! Kwa sauti ya saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani unaanguka, ukiangamizwa katika mngurumo wa wimbo wa ufalme, usiinuke tena kamwe!

Nani duniani anathubutu kuinuka na kupinga? Ninaposhuka duniani Naleta moto, Naleta ghadhabu, Naleta maafa ya aina yote. Falme za dunia sasa ni ufalme Wangu! Juu angani, mawingu yanagaagaa na kujongea kama mawimbi; chini ya anga, maziwa na mito inatapakaa na kutoa muziki wa kusonga kwa furaha. Wanyama wanaopumzika wanaibuka kutoka kwenye matundu yao, na watu wote ambao wamelala wanaamshwa na Mimi. Siku ambayo watu wengi wameingojea hatimaye imefika! Wananiimbia nyimbo nzuri sana!

Katika wakati huu mzuri, katika wakati huu wa kusisimua,

sifa zinasikika kila mahali, juu mbinguni na chini duniani. Nani asingesisimka kwa ajili ya hili?

Ni moyo wa nani usingechamka? Ni nani asingelia kwa sababu ya tukio hili?

Anga si anga ya zamani, sasa ni anga ya ufalme.

Dunia si dunia ya awali, sasa ni nchi takatifu.

Baada ya mvua kubwa kupita, ulimwengu mchafu wa kale unafanywa upya kabisa.

Milima inabadilika … maji yanabadilika …

watu pia wanabadilika … vitu vyote vinabadilika….

Aa, milima iliyo mitulivu! Inukeni na mnichezee!

Aa, maji yaliyotuama! Endeleni kutiririka kwa wingi!

Ninyi wanadamu mnaoota ndoto! Jiinueni na mfuate!

Nimekuja … Mimi ni mfalme….

Wanadamu wote watauona uso Wangu kwa macho yao wenyewe, wataisikia sauti Yangu kwa masikio yao wenyewe,

watafurahia wenyewe maisha katika ufalme….

Matamu sana… mazuri sana….

Yasiyosahaulika … yasiyoweza kusahaulika….

Katika mwako wa hasira Yangu, joka kubwa jekundu linapambana;

katika hukumu Yangu adhimu, pepo wanaonyesha sura zao za kweli;

kwa maneno Yangu makali, watu wote wanaona aibu sana, na hawana popote pa kujificha.

Wanakumbuka zamani, jinsi walivyonidhihaki na kunikejeli.

Hakukuwahi kuwa na wakati ambapo hawakujiringa, hakukuwa kamwe na wakati ambapo hawakuniasi.

Leo, nani halii? Nani hahisi majuto?

Ulimwengu dunia wote umejawa machozi …

umejaa sauti za kushangilia … umejaa sauti za vicheko….

Furaha isiyoweza kufananishwa … furaha isiyo na kifani….

Mvua nyepesi inatarakanya … theluji nzito inaanguka….

Ndani ya watu, huzuni na furaha zinachanganyika … baadhi wakicheka …

baadhi wakilia … na baadhi wakishangilia….

Kana kwamba watu wote wamesahau … ikiwa haya ni majira ya kuchipua yaliyojaa mvua na mawingu,

majira ya joto yenye maua yanayochanua, majira ya kupukutika kwa majani yenye mavuno mengi,

au majira ya baridi yaliyo baridi kama barafu na jalidi, hakuna anayejua….

Angani mawingu yanaenda pepe, duniani bahari zinavurugwa.

Wana wanapunga mikono yao … watu wanasogeza miguu yao wakicheza….

Malaika wanafanya kazi … malaika wanachunga….

Watu wote duniani wanashughulika, na vitu vyote duniani vinazidishwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Wimbo wa Ufalme

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 60)

Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu. Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani? Wakati Wanangu na watu Wangu wanarudi katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Ambayo ni kusema, Nianzapo binafsi kazi Yangu duniani, na wakati enzi ya hukumu inakaribia tamati yake, Naanza kuelekeza maneno Yangu kwa ulimwengu mzima, na kutoa sauti ya Roho Wangu kwa dunia nzima. Kupitia maneno Yangu, Nitasafisha wanadamu na mambo yote miongoni mwa yote yaliyo mbinguni na duniani, ili nchi si chafu na fisadi tena, lakini ni ufalme takatifu. Nitatengeneza upya mambo yote, ili yatolewe kwa matumizi Yangu, na yasiwe na pumzi ya dunia tena, na yasichafuliwe na ladha ya ardhi tena. Duniani, mwanadamu ametafuta malengo na asili ya maneno Yangu, na amechunguza matendo Yangu, lakini bado hakuna aliyewahi kujua kwa kweli asili ya maneno Yangu, na hakuna aliyewahi kuona kwa kweli matendo Yangu ya ajabu. Ni leo tu, Nikujapo binafsi miongoni mwa wanadamu na kuongea maneno Yangu, ndipo mwanadamu anapata maarifa kidogo kunihusu, kutoa nafasi “Yangu” ndani ya mawazo yao, badala yake kutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya fahamu zake. Mwanadamu ana dhana na amejawa na udadisi; ni nani ambaye hangetaka kumwona Mungu? Ni nani ambaye hangetamani kukutana na Mungu? Lakini bado kitu pekee kilicho na nafasi ya uhakika ndani ya moyo wa mwanadamu ni Mungu ambaye mwanadamu anahisi kuwa dhahania na asiye dhahiri. Nani angetambua haya kama Singewaeleza wazi? Nani angeamini kwa kweli Mimi nipo? Kwa hakika bila shaka yoyote? Kuna tofauti kubwa kati ya “Mimi” aliye ndani ya mwanadamu na “Mimi” wa ukweli, na hakuna anayeweza kuwalinganisha. Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi Nijua, na hata angekuja kunijua, je, maarifa kama hayo bado hayangekuwa dhana? Kila siku Natembea miongoni mwa watu wengi, na kila siku Nafanya kazi ndani ya kila mtu. Wakati mwanadamu kweli ananiona, ataweza kunijua kwa maneno Yangu, na kuelewa njia Ninazotumia kuzungumza na pia nia Zangu.

Ufalme ufikapo rasmi duniani, ni nini, kati ya mambo yote, sio kimya? Nani, kati ya watu wote, hana hofu? Natembea kila mahali katika ulimwengu dunia wote, na kila kitu kinapangwa na Mimi binafsi. Wakati huu, nani asiyejua vitendo Vyangu ni vya ajabu? Mikono Yangu inashikilia mambo yote, lakini bado Niko juu ya mambo yote. Leo, si kupata mwili Kwangu na kuwepo Kwangu binafsi miongoni mwa wanadamu maana ya ukweli ya unyenyekevu na kujificha Kwangu? Kwa nje, watu wengi wananipongeza kama mzuri, wananisifu kama mzuri, lakini ni nani anayenijua kweli? Leo, mbona Nauliza kuwa mnijue? Lengo Langu sio kuaibisha joka kubwa jekundu? Sitaki kumlazimisha mwanadamu kunisifu, lakini kumfanya anijue kupitia hapo atakuja kunipenda, na hivyo kunisifu. Sifa kama hiyo inastahili jina lake, na si mazungumzo yasiyokuwepo; ni sifa tu kama hii inaweza kufikia kiti Changu cha enzi na kupaa angani. Kwa sababu mwanadamu amejaribiwa na kupotoshwa na Shetani, kwa sababu amechukuliwa na fikira na kuwaza, Nimekuwa mwili ili kuwashinda binafsi wanadamu wote, kufichua dhana zote za mwanadamu, na kupasua mawazo ya mwanadamu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu hajionyeshi mbele Yangu tena, na hanitumikii tena akitumia dhana zake mwenyewe, na hivyo, “Mimi” katika dhana za mwanadamu ameondoka kabisa. Ufalme ufikapo, Naanza kwanza hatua hii ya kazi, na Nafanya hivyo miongoni mwa watu Wangu. Sababu nyinyi ni watu Wangu waliozaliwa kwa nchi ya joka kubwa jekundu, kwa hakika hakuna tu hata kidogo, ama kipimo cha sumu ya joka kubwa jekundu ndani yenu. Hivyo, hatua hii ya kazi Yangu hasa inawaangazia, na hiki ni kipengele kimoja cha umuhimu wa kupata mwili Kwangu Uchina. Watu wengi hawawezi kuelewa hata chembe cha maneno Ninayoyasema, na wanapoweza, uelewa wao ni wenye ukungu na ovyo. Hii ni ile hatua ya kugeuka amabayo Ninaizungumzia. Iwapo watu wote wangeweza kusoma maneno Yangu na kuelewa maana yao, basi nani miongoni mwa wanadamu angeweza okolewa, na kutupwa kuzimu? Mwanadamu anijuapo na kunitii ndio wakati Nitakapopumzika, na itakuwa wakati hasa ambapo mwanadamu ataweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Leo, kimo chenu ni kidogo sana, karibu kiwe kiwango cha kusikitisha, na hakistahili hata kuinuliwa—sembuse ujuzi wenu kunihusu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 11

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 61)

Wakati umeme unatoka Mashariki—ambao pia ni wakati hasa Naanza kutamka maneno Yangu—umeme unapotoka, mbingu yote inaangazwa, na mabadiliko yanatokea kwenye nyota zote. Wanadamu wote wanakuwa kana kwamba wamepangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya asili, macho yao yaking’aa, wakikosa uhakika wa kile wanachopsawa kufanya, na sembuse jinsi ya kuficha sifa zao mbaya. Wao pia ni kama wanyama wanaoitoroka kutoka kwa mwangaza Wangu amabao wanakimbilia usalama katika mapango ya milimani—ilhali, hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kufutiliwa mbali kutoka katika mwanga Wangu. Wanadamu wote wako na hofu na wasiwasi, wote wanangoja, wote wanatazama; na ujio wa mwanga Wangu, wote wanasherehekea katika siku waliozaliwa, na vilevile wote wanailaani siku waliyozaliwa. Hisia zinazopingana haziwezi kuelezeka; machozi ya kujiadhibu huunda mito, na yanabebwa mbali juu ya mvo unaofagia, kwenda mara moja yasionekane tena. Kwa mara nyingine, siku Yangu inakaribia jamii ya binadamu, mara nyingine ikiamsha jamii ya binadamu, ikiwapa binadamu hatua ya kutengeneza mwanzo mpya. Moyo Wangu unapiga na, kufuatia mdundo wa mpigo wa moyo Wangu, milima inaruka kwa furaha, maji yanacheza kwa furaha, na mawimbi, kwa wakati ufaao, yanagonga juu ya mawe ya mwamba. Ni vigumu kuonyesha kile kilicho ndani ya moyo Wangu. Nataka vitu vyote visivyo safi vichomeke na kuwa majivu Nikitazama, Nataka wana wote wa kutotii wapotee kutoka mbele ya macho Yangu, wasikawie tena katika uwepo. Sijatengeneza mwanzo mpya katika makao ya joka kubwa jekundu pekee, Nimeanza pia kazi mpya katika ulimwengu. Hivi karibuni falme za dunia zitakuwa ufalme Wangu; hivi karibuni falme za dunia zitakoma kuwepo milele kwa sababu ya ufalme Wangu, kwa sababu Nimetimiza ushindi tayari, kwa sababu Nimerejea kwa ushindi. Joka kubwa jekundu limetumia njia zote za kuweza kufikiriwa ili kuvuruga mpango Wangu, likitumaini kufuta kazi Yangu duniani, lakini Naweza kukata tamaa kwa sababu ya mbinu zake za udanganyifu? Naweza kutishwa hadi kukosa kujiamini na vitisho vyake? Hakujawahi kuwa na kiumbe hata mmoja mbinguni ama duniani ambaye Simshiki katika kiganja cha mkono Wangu; ni kiwango gani zaidi ambacho huu ni ukweli kuhusu joka kuu jekundu, chombo hiki kinachotumika kama foili[a] Kwangu? Je, pia si kitu cha kutawaliwa na mikono Yangu?

Wakati wa kupata mwili Kwangu katika dunia ya binadamu, binadamu alifika pasipo kujua katika siku hii na usaidizi wa uongozi wa mkono Wangu, pasipo kujua akaja kunifahamu. Lakini, kuhusu jinsi ya kutembea katika njia iliyo mbele, hakuna aliye na fununu, hakuna anayejua, na bado hakuna aliye na kidokezo juu ya mwelekeo ambao hiyo njia itampeleka. Mwenyezi pekee akimwangalia ndipo yeyote ataweza kutembea njia hiyo hadi mwisho; akiongozwa tu na umeme kutoka Mashariki ndipo yeyote ataweza kuvuka kizingiti kinachoelekea katika ufalme Wangu. Miongoni mwa wanadamu, hakujawahi kuwa na yeyote ambaye ameuona uso Wangu, ambaye ameona umeme katika Mashariki; sembuse yule ambaye amesikia sauti inayotoka kwa kiti Changu cha enzi? Kwa kweli, kutoka siku za zamani, hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye amewasiliana na nafsi Yangu moja kwa moja; leo tu, wakati Nimekuja duniani, ndipo wanadamu wana nafasi ya kuniona. Lakini hata sasa, wanadamu bado hawanifahamu, jinsi wanavyouangalia uso Wangu na kuisikia tu sauti Yangu, lakini bila kuelewa Ninachomaanisha. Wanadamu wote wako hivi. Ukiwa mmoja wa watu Wangu, je huhisi fahari ya kina unapoona uso Wangu? Na, je, huhisi aibu kwa sababu hunifahamu? Natembea kati ya wanadamu, na Naishi kati ya wanadamu, kwa kuwa Nimekuwa mwili na Nimekuja katika ulimwengu wa binadamu. Lengo Langu sio tu kuwawezesha binadamu kuutazamia mwili Wangu; cha muhimu zaidi, ni kuwawezesha binadamu kunifahamu Mimi. Zaidi, kupitia mwili Wangu, Nitamhukumu binadamu kwa dhambi zao; kupitia mwili Wangu, Nitashinda joka kuu jekundu na kuangamiza pango lake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 12

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 62)

Watu ulimwenguni kote wanasherehekea kufika kwa siku Yangu, na malaika wanatembea miongoni mwa watu Wangu wote. Shetani anapoleta vurugu, malaika, kwa sababu ya huduma yao mbinguni, daima huwasaidia watu Wangu. Wao hawadanganywi na ibilisi kwa sababu ya udhaifu wa binadamu, ila wanapata uzoefu mwingi wa maisha ya mwanadamu yaliyojawa na ukungu unaosababishwa na uvamizi wa nguvu za giza. Watu wote wananyenyekea chini ya jina Langu, na hakuna wakati ambapo mtu huinuka kwa wazi kunipinga Mimi. Kwa sababu ya shughuli za malaika, mwanadamu anakubali jina Langu na wote wako katika mtiririko wa kazi Yangu. Dunia inaanguka! Babeli imelemaa! Dunia ya kidini—itakosa kuharibiwa vipi na mamlaka Yangu duniani? Ni nani bado anathubutu kuniasi na kunipinga? Waandishi? Wakuu wote wa kidini? Viongozi na wenye mamlaka wa duniani? Malaika? Ni nani asiyesherehekea ukamilifu na wingi wa mwili Wangu? Miongoni mwa watu wote, nani asiyeimba sifa Zangu bila kukoma, ni nani asiye na furaha isiyoshindwa? Ninaishi katika nchi ya kiota cha joka kubwa jekundu, ilhali hili halinifanyi Mimi nitetemeke kwa uoga wala kutoroka, kwa maana watu wa nchi hii wote wameanza kulichukia. Hakuna wakatia ambapo kitu chochote kimefanya “wajibu” wake mbele ya joka kwa sababu ya joka hili; badala yake, vitu vyote vinatenda kama vinavyoona kuwa bora, na kila kitu kinaenda kufanya shughuli zake. Je, mataifa ya ulimwengu yatakosaje kuangamia? Mataifa ya ulimwengu yatakosaje kuanguka? Watu Wangu watakosaje kushangilia? Watakosaje kuimba kwa furaha? Je, hii ni kazi ya mwanadamu? Je, ni tendo la mikono ya mwanadamu? Nilimpa mwanadamu mzizi wa kuwepo kwake, na Nikampa vitu halisi vya dunia, ilhali mwanadamu haridhiki na hali yake ya sasa na anauliza kuingia katika ufalme Wangu. Lakini atawezaje kuingia katika ufalme Wangu kwa urahisi vile, bila kulipa gharama yoyote, na bila nia ya kujitoa kwa kujinyima? Badala ya kulazimisha chochote kutoka kwa mwanadamu, Mimi huweka mahitaji kwake, ili ufalme Wangu duniani ujawe na utukufu. Mwanadamu ameongozwa na Mimi mpaka enzi ya sasa, anaishi katika hali hii, na anaishi katika mwongozo wa mwanga Wangu. Kama haingekuwa hivyo, nani kati ya watu wote duniani angejua matarajio yake? Ni nani ambaye angeelewa mapenzi Yangu? Ninaongeza matoleo Yangu katika mahitaji ya mwanadamu; je, hii haiambatani na sheria za hali asili?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 22

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 63)

Katika ufalme, vitu vingi visivyohesabika vya uumbaji vinaanza kufufuka na kupata nguvu ya maisha yao. Kwa sababu ya mabadiliko katika hali ya dunia, mipaka kati ya nchi moja na nyingine pia inaanza kusonga. Hapo awali, Nimetabiri: Wakati ardhi itagawanywa kutoka kwa ardhi, na ardhi kujiunga na ardhi, huu ndio utakuwa wakati ambao Nitayapasua mataifa kuwa vipande vidogo. Katika wakati huu, Nitafanya upya uumbaji wote na kuugawa tena ulimwengu mzima, hivyo kuweka ulimwengu katika mpangilio, Nikibadilisha hali yake ya awali kuwa mpya. Huu ndio mpango Wangu. Hizi ni kazi Zangu. Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:

Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.

Sauti Yangu inapoimarika kwa uzito, pia Ninaichunguza hali ya ulimwengu. Kupitia kwa maneno Yangu, vitu visivyohesabika vya uumbaji vyote vinafanywa upya. Mbingu inabadilika, kama ifanyavyo dunia. Binadamu wanafunuliwa wakiwa katika hali yao halisi na, polepole, kila mtu anatengwa kulingana na aina yake, na kutafuta njia bila kujua wanajipata wakirejea katika ngome za familia zao. Hii itanifurahisha sana. Niko huru kutokana na vurugu, na bila kutambulika, kazi Yangu kuu inatimizwa, na vitu visivyohesabika vya uumbaji vinabadilishwa, bila kujua. Nilipoumba ulimwengu, Niliunda kila kitu kulingana na aina yake, Nikiweka vitu vyote vilivyo na maumbo pamoja na mifano zao. Wakati mpango wa usimamizi Wangu unapokaribia tamati, Nitarejesha hali ya awali ya uumbaji, Nitarejesha kila kitu kiwe katika hali ya awali, Nikibadilisha kila kitu kwa namna kubwa, ili kila kitu kirudi ndani ya mpango Wangu. Muda umewadia! Hatua ya mwisho katika mpango Wangu iko karibu kutimika. Ah, dunia ya kitambo yenye uchafu! Kwa hakika mtaanguka chini kwa maneno Yangu! Kwa hakika mtafanywa kuwa bure kwa mujibu wa mpango Wangu! Ah, vitu visivyo hesabika vya uumbaji! Wote mtapata maisha mapya katika maneno Yangu—utapata uhuru wako Bwana Mkuu! Ah, dunia mpya, safi isiyo na uchafu! Kwa kweli mtafufuka katika utukufu Wangu! Ah Mlima Zayuni! Usiwe kimya tena. Nimerudi kwa ushindi! Kutoka miongoni mwa uumbaji, Ninaichunguza dunia nzima. Duniani, wanadamu wameanza maisha mapya, wameshinda tumaini mpya. Ah, watu Wangu! Mtakosaje kurudi kwa maisha ndani ya mwanga Wangu? Mtakosaje kuruka kwa furaha chini ya uongozi Wangu? Ardhi zinapiga kelele kwa furaha, maji yanapiga kelele kali na vicheko vya furaha! Ah, Israeli iliyofufuka! Mtakosaje kuhisi fahari kwa mujibu wa majaaliwa Yangu? Ni nani amelia? Ni nani ameomboleza? Israeli ya kitambo haiko tena, na Israeli ya leo imeamka, imara na kama mnara, katika dunia, imesimama katika mioyo ya binadamu wote. Israeli ya leo kwa hakika itapata chanzo cha uwepo kupitia kwa watu Wangu! Ah, Misri yenye chuki! Hakika, bado hamsimami dhidi Yangu? Mnawezaje kuichukulia huruma Yangu kimzaha na kujaribu kuepuka kuadibu Kwangu? Mtakosaje kuwa katika kuadibu Kwangu? Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, ghadhabu, na kuadibu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 64)

Malaika wanapocheza muziki wakinisifu, hii inasisimua huruma kwa ajili ya binadamu. Moyo wangu unajawa na huzuni ghafla, na inakuwa vigumu kujiondoa katika hisia hii ya kuhuzunisha. Katika furaha na huzuni ya kutengana na kisha kuunganika Kwangu na mwanadamu, hatuwezi kubadilishana mawazo. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, nyakati ambapo Mimi na mwanadamu tunaweza kukutana ni nadra sana. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hangetamani kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena? Moyo Wangu una hofu nyingi, na nafsi ya binadamu imejaa wasiwasi mwingi. Licha ya sisi kuwa katika nafsi moja, hatuwezi kuwa pamoja mara kwa mara, na hatuwezi kuonana mara kwa mara. Kwa sababu hii, maisha ya wanadamu wote yamepata pigo kuu na hayana nguzo za nguvu muhimu, kwa sababu wamekuwa na hamu kuu Kwangu. Ni kana kwamba wao ni viumbe waliorushwa kutoka mbinguni, wakiliita jina Langu kutoka duniani, wakiinua macho yao Kwangu kutoka ardhini—lakini wanawezaje kuepuka kutoka kwa midomo ya mbwa mwitu mlafi? Wanawezaje kujiokoa kutokana na tishio na majaribu yake? Binadamu wanawezaje kukosa kujitolea kwa sababu ya kutii utaratibu wa mpango Wangu? Wanaponisihi kwa sauti, Ninageuza uso Wangu kutoka kwao, kwa maana Sitaki kushuhudia zaidi ya hayo; Lakini, itawezekanaje Nisisikie vilio vya watu hawa? Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakataza maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui Wangu wote waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu. Katika hali Yangu ya huzuni, hasira imechanganywa, Nitaukanyaga ulimwengu wote sawasawa, bila kumwacha yeyote, na kuwatia maadui Wangu hofu kubwa. Naiangamiza dunia nzima, na kuwafanya maadui Wangu waanguke katika maangamizo hayo, ili kuanzia sasa na kuendelea wasiwapotoshe wanadamu tena. Mpango Wangu tayari umeamuliwa, na hakuna yeyote, haijalishi ni nani, atakayeubadilisha. Ninapotembeatembea kwa fahari kuu ulimwenguni, wanadamu wote watafanywa wapya, na kila kitu kitapewa uhai tena. Mwanadamu hatalia tena, hatanililia tena akitaka msaada. Hapo, moyo Wangu utajawa na furaha tele, na wanadamu Watanirudia kwa shangwe. Ulimwengu mzima, kutoka juu mpaka chini, utabubujikwa na nderemo …

Leo hii, miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, Ninaendeleza kazi Niliyokusudia kukamilisha. Ninamtembelea kila mmoja, Nikifanya kazi Yangu jinsi Nilivyopanga, na binadamu wote wanayagawanya mataifa mengine kulingana na mapenzi Yangu. Watu walio duniani wameweka mawazo yao kwa hatima zao wenyewe, kwa maana siku yenyewe hakika inakaribia na malaika wanacheza parapanda zao. Hakutakuwa na kuchelewa tena, na kila kiumbe ataanza kucheza kwa shangwe. Ni nani anayeweza kusongeza siku Yangu kwa uwezo wake? Inawezekana kiwe kiumbe cha duniani? Zinaweza kuwa nyota angani au malaika? Ninapotoa tamko la kuanza ukombozi wa wana wa Israeli, siku Yangu inawaelekea watu wote wa ulimwengu. Kila mwanadamu anahofia kurejea kwa taifa la Israeli. Israeli itakaporejea, hiyo itakuwa siku Yangu ya utukufu, na pia, itakuwa siku ambayo kila kitu kitabadilika na kuwa kipya. Hukumu ya haki inapoukaribia ulimwengu, watu wote watakuwa na woga na hofu, kwa maana ulimwengu wa mwanadamu haufahamu haki. Wakati ambapo Jua la haki litaonekana, Mashariki itaangazwa, kisha litaangaza ulimwenguni kote, likimfikia kila mtu. Iwapo mwanadamu atatenda haki Yangu, ni kitu gani kitakuwa cha kuogopesha. Watu Wangu wote wanangoja siku ya kurudi Kwangu, wanatarajia kwa hamu siku Yangu. Wanangoja Mimi niwaadhibu wanadamu wote na kupanga hatima ya wanadamu katika wajibu Wangu kama Jua la haki. Ufalme Wangu unaenea katika ulimwengu mzima, na kiti Changu cha enzi kimenyakua mioyo ya mamia ya milioni nyingi za watu. Kwa usaidizi wa malaika wa mbinguni, utimilifu Wangu mkuu utakamilika hivi karibuni. Wanangu na watu Wangu wote wanangoja kwa hamu kurejea Kwangu, wakitarajia kuunganishwa Kwangu nao, tusije tukatengana tena. Itawezekanaje watu wote wa ufalme Wangu wasikimbie wakifurahiana kwa kuunganika pamoja na Mimi tena? Inawezekana huu uwe muungano usio na gharama yoyote iliyolipwa? Mimi Ninaheshimiwa machoni pa kila mtu, Ninadhihirika katika maneno ya kila mtu. Nitakaporejea, aidha, Nitashinda nguvu zote za adui. Wakati umewadia! Nitaianza kazi Yangu, Nitatawala miongoni mwa wanadamu! Tazama, Ninarejea! Ninaondoka! Hili ndilo kila mmoja anatarajia, ndilo kila mmoja anatumainia. Nitawaruhusu binadamu wote watazame kufika kwa siku Yangu na wote watakaribisha siku Yangu kwa furaha tele!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 27

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 65)

Siku hiyo ambayo vitu vyote vilifufuliwa, Nilikuja miongoni mwa wanadamu, na Nimeshinda naye kwa siku zilizokuwa za ajabu usiku na mchana. Ni katika hatua hii tu ndipo mwanadamu anaona wepesi Wangu wa kufikiwa, na vile uhusiano wake na Mimi unavyozidi kuwa mwingi, anaona baadhi ya kile Ninacho na Nilicho—na kwa sababu hii, anapata ufahamu kunihusu. Miongoni mwa watu wote, Ninainua kichwa Changu na kutazama, na wote wananiona. Hata hivyo, wakati maafa yanaikumba dunia, wanakuwa na wasiwasi mara moja, na sura Yangu inatoweka kutoka katika nyoyo zao; wakishikwa na hofu kutokana na kufika kwa maafa, hawasikii kusihi Kwangu. Nimepita kati ya wanadamu kwa miaka mingi, lakini hajawahi kufahamu hili, na hajawahi kunijua. Leo Namwambia hili kwa kinywa Changu mwenyewe, na kufanya watu wote waje mbele Yangu kupata kitu kutoka Kwangu, lakini bado wanaendelea kukaa mbali Nami, na hivyo basi hawanijui. Wakati nyayo Zangu zitaukanyaga ulimwengu mzima na hadi miisho ya dunia, mwanadamu ataanza kutafakari juu yake mwenyewe, na watu wote watakuja Kwangu na kusujudu mbele Zangu na kuniabudu. Hii itakuwa siku ya utukufu Wangu, siku ya kurudi Kwangu, na pia siku ya kuondoka Kwangu. Sasa, Nimeanza Kazi Yangu miongoni mwa watu wote, Nimeanza kirasmi, katika ulimwengu wote, ukamilishaji wa mpango Wangu wa usimamizi. Kuanzia sasa na kuendelea, wowote ambao si waangalifu wanastahili kutumbukizwa katikati ya kuadibu kusiko na huruma wakati wowote. Hii si kwa sababu Mimi sina utu, lakini ni hatua ya mpango Wangu wa usimamizi; zote lazima ziendelee kulingana na hatua za Mpango Wangu, na hakuna mwanadamu anayeweza kubadili hali hii. Ninapoanza kirasmi Kazi Yangu, watu wote wanatembea kama Mimi hatua kwa hatua, kiasi kwamba watu katika ulimwengu wote wanakuwa katika hatua na Mimi, kuna “shangwe” ulimwengu mzima, na mwanadamu anaendelezwa mbele na Mimi. Kwa sababu hii, joka kubwa jekundu mwenyewe anachapwa na Mimi mpaka anakuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na wazimu, na anahudumia Kazi Yangu, na, licha ya kutokuwa na nia, anashindwa kufuata tamaa zake mwenyewe, na kukosa njia nyingine ila kujiwasilisha kwa udhibiti Wangu. Katika mipango Yangu yote, joka kubwa jekundu ni foili[a] Yangu, adui Wangu, na pia mtumishi Wangu; kwa hivyo, Sijawahi kushusha “mahitaji” Yangu kwake. Kwa hivyo, hatua ya mwisho ya kazi Yangu katika mwili inakamilika katika nyumba ya joka huyu. Kwa njia hii, joka kubwa jekundu anapata uwezo zaidi wa kunitumikia Mimi vizuri, kwa njia ambayo Mimi Nitamshinda na kukamilisha Mpango Wangu. Ninapofanya kazi, malaika wote wanaanzisha vita vya maamuzi na Mimi na kuamua kutimiza matakwa Yangu katika hatua ya mwisho, ili watu walio duniani wajitoe Kwangu kama malaika, na wasiwe na haja ya kunipinga Mimi, na wasifanye chochote ambacho kinaniasi. Hii ndio elimumwendo ya kazi Yangu kotekote katika ulimwengu.

Madhumuni na umuhimu wa kuwasili Kwangu miongoni mwa mwanadamu ni kuwaokoa wanadamu wote, kuwaleta watu wote katika nyumba Yangu, kuunganisha mbingu pamoja na ardhi, na kufanya mwanadamu kufikisha “ishara” kati ya mbingu na dunia, kwa maana hiyo ndiyo kazi asili ya mwanadamu. Wakati Nilimuumba mwanadamu, Nilifanya mambo yote yawe tayari kwa ajili ya mwanadamu, na baadaye, Mimi Nikamruhusu mwanadamu kupokea utajiri Niliompa kulingana na masharti Yangu. Ndio maana Nasema ni kwa uongozi Wangu ndio maana wanadamu wote wamefikia siku hii. Na haya yote ni Mpango Wangu. Miongoni mwa watu wote, idadi kubwa ya watu ipo chini ya ulinzi wa Upendo Wangu, na idadi kubwa inaishi chini ya kuadibu kwa chuki Yangu. Ingawa watu wote wanaomba Kwangu, bado hawana uwezo wa kubadili hali yao ya sasa; mara tu wamepoteza matumaini, wanaweza tu kuwacha hali asili ichukue mkondo wake na kusitisha uasi Kwangu, kwa maana haya ndiyo yote yanayoweza kukamilishwa na mwanadamu. Inapokuja kwa hali ya maisha ya mwanadamu, mwanadamu bado hajapata maisha halisi, yeye bado hajaona kupita katika udhalimu, ukiwa, na hali duni ya dunia—na hivyo, kama haingekuwa ujio wa maafa, watu wengi bado wangekumbatia hali halisi ya dunia, na bado wangejishughulisha katika ladha ya “uzima.” Je, hii si hali halisi ya dunia? Je, hii si sauti ya wokovu Ninayonena kwa mwanadamu? Kwa nini, miongoni mwa wanadamu, hakuna kamwe aliyenipenda kwa kweli? Ni kwa nini mwanadamu ananipenda tu katikati ya kuadibu na majaribu, lakini hakuna mwanadamu Anayenipenda chini ya ulinzi Wangu? Mimi Nimetoa kuadibu Kwangu mara nyingi juu ya mwanadamu. Wao wanaiangalia, kisha wanaipuuza, na hawawezi kujifunza na kutafakari juu yake kwa wakati huu, na hivyo yote yanayokuja juu ya mwanadamu ni hukumu isiyo na huruma. Hii ni mojawapo tu ya mbinu Zangu za kazi, lakini bado ni kwa ajili ya kumbadili mwanadamu na kumfanya aweze kunipenda.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 29

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 66)

Mimi Natawala katika ufalme, na zaidi ya hapo, Ninatawala katika ulimwengu mzima; Mimi ni Mfalme wa ufalme na pia Mkuu wa ulimwengu. Kutoka wakati huu na kuendelea, Nitawakusanya wote wasio wateule na Nitaanza kufanya kazi Yangu katika mataifa, Na Nitatangaza amri Yangu ya utawala kwa ulimwengu mzima, ili kwa mafanikio Niweze kuingia katika hatua ifuatayo ya Kazi Yangu. Mimi nitatumia kuadibu ili kueneza kazi Yangu katika Mataifa, ambayo ni kusema, Nitatumia nguvu dhidi ya wale wote walio watu wa Mataifa. Kwa kawaida, kazi hii itafanyika kwa wakati mmoja na ile Kazi Yangu miongoni mwa wale waliochaguliwa. Wakati watu Wangu wanatawala na kushika madaraka duniani ndio pia itakuwa siku ambayo watu wote duniani watakuwa wameshindwa, na zaidi ya hayo, utakuwa wakati Wangu wa mapumziko—na hapo tu ndipo Nitawaonekania wale walioshindwa. Mimi huonekana kwa ufalme mtakatifu, na kujificha kutoka kwa nchi ya uchafu. Wote walioshindwa na kuwa watiifu mbele Yangu wana uwezo wa kuuona uso Wangu kwa macho yao wenyewe, na uwezo wa kusikia sauti Yangu kwa masikio yao wenyewe. Hii ni baraka ya wale waliozaliwa katika siku za mwisho, hii ni baraka Niliyoamua kabla, na hii haiwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Leo, Ninafanya kazi kwa namna hii kwa ajili ya kazi ya baadaye. Kazi Zangu zote zinahusiana, katika yote kuna wito na mwitikio: Kamwe hakuna hatua yoyote iliyokoma kwa ghafla, na kamwe hakuna hatua yoyote iliyofanywa kwa kujitegemea kivyake. Je, hivi sivyo ilivyo? Je, kazi ya siku za nyuma siyo msingi wa kazi ya leo? Je, maneno ya zamani si utangulizi wa maneno leo? Je, hatua za zamani si asili ya hatua za leo? Wakati Ninafungua rasmi hati ya kukunjwa ndio wakati watu ulimwenguni kote wanaadibiwa, wakati watu wote duniani wanakabiliwa na majaribu, na ndicho kilele cha Kazi Yangu; watu wote wanaishi katika nchi bila mwanga, na watu wote wanaishi huku kukiwa na tishio la mazingira yao. Kwa maneno mengine, ni maisha ambayo mwanadamu hajawahi kupitia kutoka wakati wa uumbaji mpaka siku ya leo, na hakuna yeyote katika enzi zote aliyeweza “kustarehe” na aina hii ya maisha, na hivyo Ninasema kwamba Ninafanya kazi ambayo haijawahi kufanyika mbeleni. Hii ndiyo hali halisi ya mambo, na hii ni maana ya ndani. Kwa sababu siku Yangu inakaribia kwa wanadamu wote, kwa sababu haionekani kuwa mbali, lakini iko mbele ya macho ya mwanadamu, ni nani asiyeweza kuwa na uoga kwa sababu ya jambo hili? Ni nani asiyekuwa na furaha katika hili? Mji mchafu wa Babeli hatimaye umefika mwisho wake; mwanadamu amekutana na dunia mpya kabisa, na mbingu na dunia zimebadilishwa na kufanywa mpya.

Wakati Najitokeza kwa mataifa yote na watu wote, mawingu meupe yanaenea angani na kunifunika. Na pia, ndege duniani wanaimba na kunichezea kwa shangwe, wakiangazia hali duniani, na hivyo kusababisha vitu vyote duniani kuwa hai, kusiwe tena na “kuwa vumbi” lakini badala yake kuishi katika hali ya uzima. Wakati Niko mawinguni, mwanadamu anatambua uso Wangu na macho Yangu kwa umbali, na kwa wakati huu yeye anahisi uoga kidogo. Katika siku za nyuma, yeye alisikia “kumbukumbu za kihistoria” kunihusu katika ngano, na matokeo yake ni kuwa anayo imani nusu na nusu shaka Kwangu. Yeye hajui Niliko Mimi, au ukubwa wa uso Wangu—je ni mpana kama bahari, au kama usio na mwisho kama malisho ya majani mabichi? Hakuna anayejua mambo haya. Ni wakati tu mwanadamu anapouona uso Wangu katika mawingu leo ndipo anapohisi kwamba Mimi wa hadithi ni wa kweli, na hivyo anakuwa na upendeleo zaidi Kwangu, na ni kwa sababu tu ya matendo Yangu ndio upendo wake Kwangu unazidi kuwa mkubwa kidogo. Lakini mwanadamu bado hanijui, na anaona tu sehemu moja Yangu katika mawingu. Baada ya hapo, Ninanyosha mikono Yangu na kuionyesha kwa mwanadamu. Mwanadamu anashangaa, na kufunika mdomo kwa mikono yake, akiwa na uoga kuwa Nitampiga chini kwa mkono Wangu, na hivyo anaongeza heshima kidogo kwa upendo wake. Mwanadamu anaweka macho yake juu ya kila hatua Yangu, akiwa na hofu kuu kuwa Nitampiga chini wakati yeye hayuko makini-lakini kutazamwa na mwanadamu hakunizuii Mimi, na Ninaendelea kufanya kazi iliyo mikononi Mwangu. Ni tu katika matendo yote Ninayofanya ndipo mwanadamu ana upendeleo fulani Kwangu, na hivyo hatua kwa hatua anakuja mbele Zangu kujiunga Nami. Wakati ukamilifu Wangu unafichuliwa kwa mwanadamu, mwanadamu atauona uso Wangu, na kutoka hapo Sitauficha au kujikinga kutoka kwa mwanadamu. Katika ulimwengu, Nitaonekana hadharani kwa watu wote, na walio nyama na damu wote wataona matendo Yangu yote. Wale wote ambao ni wa roho hakika wataishi kwa amani katika Nyumba Yangu, na bila shaka watafurahia baraka za ajabu pamoja na Mimi. Wale wote ambao Ninawajali hakika wataepuka kuadibu, na kwa hakika wataepuka maumivu ya roho na maumivu makali ya mwili. Mimi Nitaonekana hadharani kwa watu wote na kutawala na kutumia mamlaka, ili harufu ya maiti isisambae tena ulimwenguni; badala yake, manukato Yangu yataenea katika dunia nzima, kwa sababu siku Yangu inakaribia, mwanadamu anaamka, kila kitu kilicho duniani kiko katika utaratibu, na siku za kunusurika kwa dunia hazipo tena, kwa maana Mimi Nimefika!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 29

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 67)

Nitajaza mbingu na maonyesho ya kazi Yangu, ili kila kitu kilicho chini ya ardhi kisujudu chini ya nguvu Zangu, Nikitekeleza mpango Wangu wa “umoja wa ulimwengu” na kusababisha hili tamanio Langu moja kufaulu, na ili binadamu wasiweze “kuzurura kote” juu ya uso wa dunia lakini wapate hatima ya kufaa bila kuchelewa. Naifikiria jamii ya binadamu kwa kila njia, Nikifanya hilo ili kwamba wanadamu wote waje kuishi katika nchi ya amani na furaha hivi punde, ili siku za maisha yao zisiwe na huzuni na ukiwa tena, na ili mpango Wangu hautakuwa bure duniani. Kwa kuwa mwanadamu yupo pale, Nitalijenga taifa Langu duniani, kwani sehemu ya maonyesho ya utukufu Wangu iko duniani. Juu mbinguni, Nitaiweka miji Yangu kwenye haki na hivyo kufanya kila kitu kiwe kipya juu na chini. Nitaleta yote yaliyopo juu na chini ya mbingu kuwa katika umoja, ili vitu vyote duniani viungane na vyote vilivyo mbinguni. Huu ndio mpango Wangu, ndio Nitakaoutimiza katika enzi ya mwisho—mtu asiingilie sehemu hii ya kazi Yangu! Kupanua kazi yangu katika nchi za Mataifa ni sehemu ya mwisho ya kazi Yangu duniani. Hakuna anayeweza kuelewa kazi Nitakayoifanya, na hivyo watu wamepumbazwa kabisa. Na kwa sababu Nina shughuli nyingi za kazi Yangu duniani, watu huchukua fursa hiyo “kufanya mzaha.” Ili kuwazuia kuwa watundu sana, Nimewaweka chini ya kuadibu Kwangu kwanza ili wastahamili nidhamu ya ziwa la moto. Hii ni hatua moja katika kazi Yangu, nami Nitatumia uwezo wa ziwa la moto kutimiza kazi hii Yangu, la sivyo haitawezekana kutekeleza kazi Yangu. Nitawafanya wanadamu ulimwenguni kote kutii mbele ya kiti Changu cha enzi, Nikiwagawanya katika makundi mbalimbali kulingana na hukumu Yangu, Nikiwaainisha kulingana na makundi haya, na kuwaainisha zaidi katika jamii zao, ili binadamu wote wakome kuniasi, badala yake waingie katika mpango mzuri na wa taratibu kulingana na makundi ambayo Nimeyataja—mtu yeyote asitembee huku na huko bila kufikiria! Katika ulimwengu wote, Nimefanya kazi mpya; katika ulimwengu wote, binadamu wote hutunduwaa na kupigwa na bumbuwazi kwa kuonekana Kwangu kwa ghafla, upeo wao wa macho ulibubujika kwa namna ambayo haijawahi kutendeka awali kwa ajili ya kuonekana Kwangu wazi. Je, leo haiko hivi hasa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 43

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 68)

Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika watu wa nyota-nyota-nukta-nukta, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa. Kuanzia wakati huu kuendelea, Nimeingia katika enzi mpya, kuwaleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Niliporudi katika “nchi Yangu,” Nilianza sehemu nyingine tena ya kazi katika mpango Wangu wa asili, ili mwanadamu aje kunijua zaidi. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, kwa hiyo Naharakisha mbele na nyuma kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu. Hii ni enzi mpya, hata hivyo, na Nimeleta kazi mpya ili Niwachukue watu wapya wengi zaidi katika enzi mpya na kuachana na wengi wa wale Nitakaowaondoa. Katika taifa la joka kubwa jekundu, Nimetekeleza hatua ya kazi isiyoeleweka kwa wanadamu, kuwafanya kuyumba katika upepo, ambapo baadaye wengi wanabebwa kwa siri na upepo unaovuma. Kweli, huu ni “uwanja wa kupura” Ninaotaka kuusafisha; ni kile Ninachotamani na pia ni mpango Wangu. Kwa maana wengi waovu wameingia ndani kimya wakati Niko kazini, lakini Sina haraka ya kuwafukuza. Badala yake, Nitawatawanya wakati utakapofika. Ni baada ya hapo tu ndipo Nitakuwa chemchemi ya uzima, kuwakubalia wanaonipenda kweli wapokee kutoka Kwangu tunda la mtini na harufu ya yungiyungi. Katika nchi ambako Shetani huishi, nchi ya vumbi, hakuna dhahabu safi iliyobaki, ila ni mchanga tu, na kwa hiyo, Nikikabiliwa na hali hizi, Nafanya hatua hiyo ya kazi. Lazima ujue kwamba Ninachopata ni dhahabu safi, iliyosafishwa, wala si mchanga. Ni jinsi gani waovu wanaweza kubaki katika nyumba Yangu? Ninawezaje kuruhusu Mbweha kuwa vimelea ndani ya paradiso Yangu? Natumia kila mbinu inayoweza kufikiriwa kuvifukuza vitu hivi. Kabla ya mapenzi Yangu kufichuliwa, hakuna anayefahamu Ninachotaka kufanya. Nikichukua fursa hii, Ninawafukuza wale waovu, na wanalazimika kuondoka machoni Pangu. Hili ndilo Mimi huwafanyia waovu, lakini bado kutakuwa na siku ya wao kunifanyia huduma. Hamu ya watu kupata baraka ni kubwa mno; Kwa hivyo Ninageuza mwili Wangu na kuonyesha uso Wangu wa utukufu kwa watu wa Mataifa, ili watu wote waishi katika dunia yao wenyewe na kujihukumu, huku Naendelea kusema maneno ambayo Napaswa kuyasema na kuwaruzuku wanadamu wanachohitaji. Wakati wanadamu wanapata fahamu, Nitakuwa Nimeeneza kazi Yangu kitambo. Kisha Nitawaonyesha wanadamu mapenzi Yangu, na kuanza sehemu ya pili ya kazi Yangu juu ya wanadamu, kuwaruhusu watu wote wanifuate kwa karibu ili waambatane na kazi Yangu, na kuwaruhusu watu kufanya kila wawezalo kutekeleza nami kazi Ninayopaswa kufanya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili hayana kauli “kuona kwamba.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 69)

Hakuna aliye na imani kwamba atauona utukufu Wangu, na Mimi simlazimishi, badala yake Nauondoa utukufu Wangu kutoka miongoni mwa wanadamu na kuupeleka kwa ulimwengu mwingine. Wakati watu watatubu tena, basi Nitauchukua utukufu Wangu na Nitauonyesha kwa wengi wa wale wanaoamini. Hii ni kanuni ambayo Mimi hufuata katika kazi Yangu. Kwa maana kuna wakati ambapo utukufu Wangu unaondoka Kanaani, na pia kuna wakati ambapo utukufu Wangu unawaacha waliochaguliwa. Zaidi ya hayo, kuna wakati ambapo utukufu Wangu unaiacha dunia nzima, kuisababisha kuwa hafifu na kuitumbukiza katika giza. Hata nchi ya Kanaani haitaona mwanga wa jua; wanadamu wote watapoteza imani yao, lakini hakuna hata mmoja anayeweza kuiacha nchi ya Kanaani ya kupendeza. Ninapopita katika mbingu na nchi mpya tu ndipo Ninachukua sehemu nyingine ya utukufu Wangu na kuifichua kwanza katika nchi ya Kanaani, Nikisababisha nuru kuiangazia dunia nzima, iliyozama katika giza totoro la usiku, ili kuruhusu dunia nzima kuja kwa nuru hiyo. Wacha watu wote duniani kote waje kupata nguvu kutoka kwa nuru, kuruhusu utukufu Wangu uongezeke na kuonekana upya kwa kila taifa. Wacha binadamu wote utambue kwamba Nilikuja zamani katika ulimwengu wa wanadamu na Nilileta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki zamani; kwani utukufu Wangu unang’aa kutoka Mashariki, ambako uliletwa kutoka Enzi ya Neema hadi leo. Lakini Nilitokea Israeli na kutoka huko Nikawasili Mashariki. Wakati nuru ya Mashariki inapong’aa polepole tu ndipo giza kote duniani litaanza kugeuka na kuwa nuru, na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba Nilishatoka Israeli zamani na Nimeanza kuchomoza upya Mashariki. Niliwahi kushuka Israeli na baadaye Niliondoka kutoka huko, Siwezi tena kuzaliwa Israeli kwa mara nyingine, kwa kuwa kazi Yangu inauongoza ulimwengu mzima na, zaidi ya hilo, umeme unamulika moja kwa moja kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hii ndiyo sababu Nimeshuka Mashariki na kuwaletea watu wa Mashariki Kanaani. Ningependa kuwaleta watu kutoka dunia nzima waje katika nchi ya Kanaani, na kwa hiyo Naendelea kutoa maneno Yangu katika nchi ya Kanaani ili kuudhibiti ulimwengu mzima. Kwa wakati huu, hakuna nuru katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani, na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi. Niliipa Israeli utukufu Wangu kisha Nikauchukua na baadaye Nikawaleta Waisraeli Mashariki, na vilevile binadamu wote Mashariki. Nimewaleta wote kwenye nuru ili waweze kuungana tena nayo, na kushirikiana na nuru, na wasilazimike kuitafuta tena. Nitawaacha wote wanaotafuta waione nuru tena na kuuona utukufu Niliokuwa nao katika Israeli; Nitawaacha waone kwamba tayari Nimeshuka juu ya wingu jeupe miongoni mwa wanadamu, kuwaacha waone mawingu mengi meupe na vishada vingi vya matunda, na, zaidi ya hayo, Nitawaacha wamwone Yehova Mungu wa Israeli. Nitawaacha waone Mkuu wa Wayahudi, Masihi aliyengojewa kwa hamu, na kuonekana kamili kwa Mimi niliyeteswa na wafalme kotekote katika enzi. Nitafanya kazi katika ulimwengu mzima na Nitatekeleza kazi kubwa, Nikifichua utukufu Wangu wote na matendo Yangu yote kwa mwanadamu katika siku za mwisho. Nitaonyesha uso Wangu uliojaa utukufu kwa wale ambao wameningoja kwa miaka mingi, kwa wale ambao wametamani kuniona Nikija juu ya wingu jeupe, kwa Israeli ambayo imengoja Nionekane kwa mara nyingine, na kwa wanadamu wote wanaonitesa, ili wote wajue kwamba Niliuchukua utukufu Wangu zamani na kuuleta Mashariki, Ili usiwe katika Uyahudi tena. Kwani siku za mwisho tayari zimewadia!

Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu, kana kwamba mtoto mchanga amezaliwa hivi karibuni. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye “Mlima wa Mizeituni” wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni “mtoto mchanga” Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 70)

Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani aweze kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamemtamani sana na kumwonea shauku kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, kwa Yesu Mwokozi kuwarudia watu ambao Amekuwa mbali nao kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumai kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atazisamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Anatamani Yesu Mwokozi awe jinsi Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi ambaye anapendeka, mwema na wa heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kumhusu. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya “wingu jeupe” (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu hafahamu jambo hili: Ingawa Mwokozi Yesu mtakatifu Amejawa na upendo na mapenzi kwa mwanadamu, Angewezaje kufanya kazi katika “mahekalu” yaliyomilikiwa na uchafu na pepo wachafu? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Angewezaje kuwaonekania wale wanaokula mwili wa wasio na haki, kunywa damu ya wasio na haki, kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini lakini hawamfahamu, na wanaompokonya kila wakati? Mwanadamu anajua tu kuwa Yesu Mwokozi amejawa na upendo na huruma, naye ni sadaka ya dhambi iliyojawa na ukombozi. Lakini mwanadamu hana habari kwamba Yeye pia ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, uadhama, ghadhabu, na hukumu, na Aliye na mamlaka na kujawa na hadhi. Kwa hiyo ingawa mwanadamu anazamia kwa hamu na kuonea shauku kurudi kwa Mkombozi, na hata Mbingu inaguswa kwa maombi ya mwanadamu, Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 71)

Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaisha, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnasubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? Wale wote wanaosubiri kuonekana kwa Mungu wanakumbana na maswali kama haya. Nyinyi nyote mmewahi kuyafikiria zaidi ya mara moja—ila matokeo ni gani? Mungu hujidhihirisha wapi? Nyayo za Mungu zipo wapi? Mmepata majibu? Majibu ya watu wengi yangekuwa: Mungu hudhihirika miongoni mwa wale wanaomfuata na nyayo Zake zimo miongoni mwetu; ni rahisi hivyo! Mtu yeyote anaweza kutoa jibu kwa kutumia mbinu fulani, lakini je, mnafahamu kuonekana kwa Mungu ni nini, na nyayo za Mungu ni nini? Kuonekana kwa Mungu hurejelea kuwasili Kwake duniani kufanya kazi Yake. Akiwa na utambulisho na tabia Yake, na katika njia ambayo ni ya asili Kwake, Yeye hushuka miongoni mwa wanadamu kufanya kazi ya kuanzisha enzi mpya na kukamilisha enzi nyingine. Kuonekana kwa aina hii si aina fulani ya sherehe. Si ishara, picha, muujiza, au ono kuu, na hata zaidi si mchakato fulani wa kidini. Ni ukweli halisi ambao waweza kushikwa na kuonekana. Kuonekana kama huku si kwa ajili ya kufuata taratibu, au kwa ajili ya shughuli ya muda mfupi; ni, badala yake, kwa ajili ya hatua ya kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Kuonekana kwa Mungu daima ni kwenye maana na daima huenda pamoja na mpango wa usimamizi. Kuonekana huku ni tofauti kabisa na udhihirisho wa uongozi wa Mungu, utawala na kupata nuru kwa mwanadamu. Mungu hufanya kazi kubwa kila mara Anapojifunua. Kazi hii ni tofauti na enzi yoyote nyingine. Haiwezi kufikirika na mwanadamu na haijawahi kupitiwa mwanadamu. Ni kazi ambayo huanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya awali, na ni aina mpya ya kazi na iliyoboreshwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu; aidha, ni kazi ya kuleta wanadamu katika enzi mpya. Huo ndio umuhimu wa kuonekana kwa Mungu.

Katika wakati uo huo wa kuelewa kuonekana kwa Mungu, mnapaswa kutafuta nyayo za Mungu vipi? Swali hili si gumu kueleza: Palipo na kuonekana kwa Mungu; mtapata nyayo za Mungu. Maelezo kama haya yanaonekana yapo wazi sana, ila si rahisi kutekeleza kwani watu wengi hawafahamu pale Mungu anapojidhihirisha, wala pale ambapo Angependa kujidhihirishia ama iwapo Anapaswa kujidhihirisha. Wengine kwa msukumo huamini kuwa palipo na kazi ya Roho Mtakatifu kuna kuonekana kwa Mungu. Ama sivyo watu huamini kuwa palipo na watu mashuhuri wa kiroho ndipo Mungu huonekana. Vinginevyo, wanaamini kuwa palipo na watu wanaojulikana vyema ndipo Mungu huonekana. Kwa sasa tusishauriane ikiwa imani hizi ni sahihi au la. Kujibu swali kama hilo, kwanza ni lazima tuwe wazi kuhusu lengo: tunazitafuta nyayo za Mungu. Hatutafuti viongozi wa kiroho, wala kutafuta watu mashuhuri; tunafuata nyayo za Mungu. Kwa hivyo, kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa “Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.” Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani! Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulinganishwa na fikira za mwanadamu, sembuse Mungu kuonekana kwa amri ya mwanadamu. Mungu hufanya uamuzi Wake mwenyewe na huwa na mipango Yake Afanyapo kazi; aidha, Ana malengo Yake, na mbinu Zake. Si lazima Ajadiliane kazi Azifanyazo na mwanadamu au Atafute ushauri wa mwanadamu, sembuse kumfahamisha kila mtu kuhusu kazi Yake. Hii ndiyo tabia ya Mungu na, zaidi ya hayo, inafaa kutambuliwa na kila mmoja. Kama mnatamani kushuhudia kuonekana kwa Mungu, kama mnatamani kufuata nyayo za Mungu, basi kwanza ni sharti mzishinde dhana zenu. Ni sharti muache kudai kuwa Mungu afanye hiki au kile sembuse kumweka Yeye ndani ya mipaka yenu wenyewe na kumwekea upeo kwa dhana zenu. Badala yake, mnafaa kujua ni vipi mtazitafuta nyayo za Mungu, na vipi mnapaswa kukubali kuonekana kwa Mungu na ni vipi mnapaswa kutii kazi mpya ya Mungu; hiki ndicho kinapaswa kufanywa na mwanadamu. Kwa kuwa mwanadamu si ukweli, na hamiliki ukweli, mwanadamu anafaa kutafuta, kukubali na kutii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 72)

Mungu ni Mungu wa wanadamu wote. Hawi mali binafsi ya nchi au taifa lolote na hufanya kazi ya mpango Wake bila kuzuiwa na mfumo wowote, nchi au taifa. Labda hujawahi kuwazia mfumo huu, au labda wewe hukana kuwepo kwake, au labda nchi au taifa ambapo Mungu huonekana limebaguliwa na lina maendeleo duni sana duniani. Na bado Mungu ana busara Yake. Na uwezo Wake kupitia ukweli na tabia Zake kwa hakika Amepata kundi la watu wenye mawazo sawa na Yeye. Na Amepata kundi la watu ambao alitaka kutengeneza: kundi lililoshindwa Naye, watu ambao wameyavumilia majaribu machungu na aina zote za mateso na wanaweza kumfuata mpaka mwisho. Malengo ya kuonekana kwa Mungu, bila vizuizi vya nchi yoyote, ni kumruhusu Akamilishe kazi ya mpango Wake. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kutimiza kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kuwa mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu na hatimaye ikawa kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, na vilevile kukushutumu kuonekana huku; “kutowezekana” kwao kwa mara nyingine kunabana kuonekana kwa Mungu katika mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakicheka na kuanguka baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kukufuru kwa Wayahudi? Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama huwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? Mahali ambapo Mungu anajitokeza, kuna maonyesho ya kweli, na kuna sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Weka dhana zako kando. Tafakari na kusoma maneno haya kwa makini. Ukitamani ukweli, Mungu atakupa nuru ya kuyafahamu mapenzi Yake na maneno Yake. Wekeni kando mitazamo yenu ya “haiwezekani”! Kadiri watu wanavyozidi kuamini kuwa jambo fulani haliwezekani, ndivyo uwezekano wa utukiaji wake unavyoendelea kujiri, kwani ufahamu wa Mungu hupaa juu kuliko mbingu, mawazo ya Mungu yako juu ya yale ya mwanadamu, na kazi ya Mungu inapita mipaka ya fikira za mwanadamu. Kadiri kitu kinavyokuwa hakiwezekani, ndivyo kunavyokuwepo na ukweli wa kutafutwa; kadiri kitu kilivyo nje ya mipaka ya dhana na fikira za mwanaadamu, ndivyo kinavyozidi kuwa na mapenzi ya Mungu. Kwani bila kujali Mungu anajidhihirishia wapi, Mungu bado ni Mungu, na kiini chake hakitawahi kubadilika kwa sababu ya mahali ama namna ya kuonekana Kwake. Tabia ya Mungu hubaki kuwa vilevile bila kujali nyayo Zake ziko wapi. Bila kujali nyayo za Mungu zilipo, Yeye ndiye Mungu wa wanadamu wote. Kwa mfano, Bwana Yesu si Mungu tu wa Waisraeli, lakini vilevile ni Mungu wa watu wote wa Asia, Ulaya, na Marekani, na hata zaidi, ndiye Mungu pekee wa ulimwengu mzima. Hivyo basi, tuyatafute mapenzi ya Mungu na tugundue kuonekana Kwake kutoka kwa matamshi Yake na tufuate nyayo Zake. Mungu ndiye ukweli, njia na uzima. Maneno Yake na kuonekana Kwake yanakuwepo sawia, na tabia na nyayo Zake daima zitapatikana na wanadamu. Ndugu wapendwa, natumaini kwamba mnaweza kuona kuonekana kwa Mungu katika maneno haya, na kwamba muanze kuzifuata nyayo Zake kuelekea enzi mpya, na hadi katika mbingu mpya yenye kupendeza na dunia mpya iliyoandaliwa kwa wale wanaosubiri kuonekana kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 73)

Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimama. Yeye huangalia dunia nzima, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Yeye huendesha usimamizi Wake kwa hatua zilizopimwa na kulingana na mpango Wake kwa kimya, na bila madhara ya kutia shauku, ilhali nyayo Zake hukaribia, moja baada ya nyingine, daima hukaribia binadamu, na kiti Chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, na baada yake kiti Chake cha enzi mara moja hushuka kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, tukio hilo ni mandhari ya adhimu na yenye taadhima! Kama njiwa, na kama simba anayenguruma, Roho huja kati yetu. Yeye ni hekima, Yeye ni haki na uadhama, na Yeye huja kwa ukimya kati yetu, akiwa na mamlaka na akiwa amejawa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuwasili Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote ambacho yuko karibu kufanya. Maisha ya mwanadamu yanaendelea kama awali moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu huishi kati yetu, mwanadamu kama watu wengine, kama mmoja wa wafuasi wasio na maana kabisa na kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na zaidi ya hayo, Ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa katika macho yetu, Yeye ni muumini asiye wa maana tu. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu yote yanawekwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye huwaza chochote kuhusu kazi Yake na isitoshe,hakuna aliye na shuku hata kidogo kuhusu kitambulisho Chake. Chote tunachofanya ni kuendelea na shughuli zetu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi …

Kwa bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia” Kwake, na hata ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa sana, tunalitambua hata hivyo kama tamko kutoka kwaa Mungu, na tunaukubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya, ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hatufai kuyakana. Tamko linalofuata linaweza kuja kupitia mimi, au wewe, ama kupitia yeye. Yeyote yule, yote ni neema ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu huyo ni nani, hatufai kumwabudu mtu huyu, kwa kuwa bila kujali chochote, mtu huyu hawezi kuwa Mungu, wala hatuwezi kwa njia yoyote ile kumchagua mtu wa kawaida kama huyu kuwa ndiye Mungu wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika sana; mtu asiye na maana kama huyu anawezaje kusimama katika nafasi Yake? Zaidi ya hayo, tunamsubiri Mungu aje na kuturudisha kwa ufalme wa mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu hivyo anawezaje kuwa na sifa zinazostahili kufanya kazi ngumu na muhimu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima iwe juu ya wingu jeupe, ambalo halaiki ya watu wanaweza kuliona. Huo utakuwa wa adhimu namna gani! Itawezekanaje kwamba Anaweza kujificha kwa siri kati ya kundi la watu wa kawaida?

Na bado ni huyu mtu wa kawaida, aliyefichika kati ya watu, ndiye anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hatupi maelezo yoyote, wala Hatuambii kwa nini amerudi, lakini Yeye anafanya tu kazi anayotarajia kufanya kwa hatua zilizopimwa, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya, kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu; kuanzia kutumia sauti ya upole na laini mpaka kutumia maneno makali na ya adhimu—lakini hakuna inayompa mwanadamu huruma na kumtia hofu. Kila kitu Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu, maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha tukiwa tumejaa aibu isiyovumilika, tusijue pa kujificha. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anafanya. Labda tunaweza tu kunyakuliwa baada ya kuvumilia mateso haya? Vichwani mwetu tunafanya hesabu … kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado, kama awali, hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili tayari ili kutenda kazi kati yetu. Japokuwa Ametuandama kwa muda mrefu sana, ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado tunabaki bila hiari ya kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa mustakabali wetu, na bado hatuna nia ya kumwaminisha mtu huyu asiye na maana udhibiti wa mustakabali na majaliwa yetu. Kutoka Kwake, tunafurahia ugavi usioisha wa maji ya uhai, na kupitia Kwake tunaishi uso kwa uso na Mungu. Lakini tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Bado, kama awali Yeye kwa unyenyekevu, hufanya kazi Yake akiwa amefichwa ndani ya mwili, akipeana maonyesho a moyo Wake wa ndani zaidi, kana kwamba hafahamu kukataliwa Kwake na binadamu, kana kwamba yeye milele husamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele huvumilia mtazamo wa mwanadamu Kwake usioheshimu.

Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua moja baada ya nyingine ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, kuvumilia kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, kufahamu mapenzi ya Mungu, kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi “tufe,” na tena hutufanya “kuzaliwa upya”; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa sana. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake wenye upole; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, na chini ya macho Yake tunageuzwa majivu na ghadhabu Yake. Sisi ni jamii ya wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao, usiku na mchana, Yeye hunuia kuwapata. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Usiku na mchana, Yeye hakomi kamwe kuwa na wasiwasi nasi na hutulinda na kututunza usiku na mchana, Asiwache upande wetu kamwe, bali humwaga damu ya moyo Wake kwa ajili yetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa matamshi ya mwili huu mdogo na wa kawaida wa nyama, tumefurahia ukamilifu wa Mungu na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Licha ya haya, majivuno bado yanazua rabsha mioyoni mwetu, na sisi bado hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana nyingi sana, nyingi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambalo linaweza kuchukua nafasi ya Bwana katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum na hadhi ya huyu mwanadamu kwa kusita sana. Bora hafungui mdomo Wake kututaka tukiri kwamba Yeye ni Mungu, sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu ambaye yuko karibu kuja na ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu sana.

Mungu huendelea na matamshi Yake, akitumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya kuhusu kile tunachofaa kufanya na wakati uo huo akipea moyo Wake sauti. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na hisia za ndani kabisa za mwanadamu huyu asiye wa ajabu. Yeye hutema damu ya moyo Wake kwa niaba yetu, hupoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na uasi wetu na kufa ganzi kwetu kunatoa machozi na damu kutoka kwa moyo Wake. Njia hii ya kuwa na kumiliki si ya mtu wa kawaida, wala haiwezi kumilikiwa au kufikiwa na mtu yeyote aliyepotoka. Anaonyesha uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake si kitu ambacho kiumbe chochote kimepewa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ametuwezesha kuishi tena na kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele. Wakati huu, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, hatupingi tena kazi Yake na neno Lake, na tunasujudu, mbele Yake. Hakuna tunachotaka zaidi yakufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila Yake, na kulipa upendo Wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio Yake, na kushirikiana na kazi Yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile Anachotuaminia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 4: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 74)

Mungu na mwanadamu hawawezi kuzungumziwa kama wa kulingana. Dutu ya Mungu na kazi Yake ni vitu visivyoeleweka na kufahamika kwa mwanadamu. Ikiwa Mungu hawezi kufanya kazi Yake binafsi na kuzungumza maneno Yake katika ulimwengu wa mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kuelewa mapenzi ya Mungu, na kwa hivyo, hata wale waliotoa maisha yao yote kwa ajili ya Mungu hawataweza kupata idhini ya Mungu. Bila kazi ya Mungu, haijalishi jinsi gani mwanadamu anatenda mema, haitahesabika kama chochote, kwa maana fikira za Mungu daima zitakuwa juu ya fikira za mwanadamu, na hekima ya Mungu haieleweki kwa mwanadamu. Na kwa hivyo Nasema kwamba wale ambao “wanaona kwa wazi”. Mungu na kazi Yake ni wasioweza kufanikisha chochote, wao wote ni wenye kiburi na wapumbavu. Mwanadamu hafai kufafanua kazi ya Mungu; zaidi ya hayo, mwanadamu hawezi kufafanua kazi ya Mungu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu ni mdogo kushinda mchwa, kwa hivyo mwanadamu atawezaje kuelewa kazi ya Mungu? Wale wasemao daima, “Mungu hafanyi kazi kwa njia hii ama ile” au “Mungu yuko hivi ama vile”—je hawa wote si wenye kiburi? Tunafaa sote kujua kwamba watu, ambao ni wa mwili, wote wamepotoshwa na Shetani. Ni katika hali yao asili kumuasi Mungu, na hawako katika usawa na Mungu, sembuse kuweza kutoa mawaidha kwa kazi ya Mungu. Jinsi Mungu anavyomwelekeza mwanadamu ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mwanadamu anafaa kunyenyekea, na hafai kuwa na wazo hili ama lile, kwani mwanadamu ni mchanga tu. Kwa sababu tunajaribu kumtafuta Mungu, hatufai kuwekelea dhana zetu katika kazi ya Mungu ili Mungu Aziwaze, na zaidi hatufai kutumia tabia zetu potovu kwa kupinga kazi ya Mungu kwa makusudi. Je hili halitatufanya wapinga Kristo? Je, watu kama hawa watawezaje kusema kuwa wanamwamini Mungu? Kwa maana tunaamini kuwa kuna Mungu, na kwa maana tunatamani kumtosheleza na kumwona, tunapaswa kutafuta njia ya ukweli, na tunapaswa kutafuta njia ya kulingana na Mungu. Hatupaswi kuwa katika upinzani sugu kwa Mungu; Matendo kama haya yatakuwa na matokeo gani mazuri?

Leo hii, Mungu Anayo kazi mpya. Unaweza kuyakataa maneno haya, yanaweza kuhisi yasiyo ya kawaida kwako, lakini Nakushauri usifichue asili yako halisi, kwa maana wale tu walio na njaa ya kweli na kiu cha haki mbele za Mungu ndio wanaweza kupata ukweli, na wale wanaomcha Mungu kwa ukweli tu ndio wanaweza kupata nuru na kuongozwa na Mungu. Hakuna litakalotoka kwa kutafuta ukweli kupitia ugomvi. Ni kwa kutafuta kwa utulivu ndio tunaweza kupata matokeo. Ninaposema kwamba “leo, Mungu Anayo kazi mpya,” Ninaashiria Mungu kurudi katika mwili. Pengine huyajali maneno haya, pengine unayachukia, au pengine una haja kubwa sana nayo. Haijalishi ni hali gani, Natumai kuwa wote walio na tamaa ya kweli ya kuonekana kwa Mungu wataweza kuukabili ukweli huu na kutafakari juu yake kwa makini. Ni vyema usiamue jambo upesi bila kuzingatia suala zima. Hivi ndivyo watu wenye hekima wanapaswa kutenda.

Kuchunguza kitu cha aina hii sio vigumu, lakini kunahitaji kila mmoja wetu ajue ukweli huu: Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu. Sura ya nje haiamulii dutu; na zaidi, kazi ya Mungu haiwezi kamwei kuambatana na dhana za mwanadamu. Je, si sura ya nje ya Yesu ilikinzana na dhana za mwanadamu? Je sura Yake na mavazi Yake hayakuweza kutoa dalili yoyote ya utambulisho Wake? Je, si sababu ya Mafarisayo wa zamani kabisa kumpinga Yesu hasa ilikuwa ni kwa sababu waliiangalia tu sura Yake ya nje, na hawakuyaweka moyoni maneno Aliyoongea? Ni matumaini Yangu kuwa ndugu wanaotafuta kuonekana kwa Mungu hawatarudia tanzia ya kihistoria. Hampaswi kuwa Mafarisayo wa wakati huu na kumsulubisha Mungu msalabani tena. Mnafaa kufikiria kwa makini jinsi ya kukaribisha kurudi kwa Mungu, na kuwa na mawazo dhahiri ya jinsi ya kuwa mtu anayetii ukweli. Hili ni jukumu la kila mtu anayengoja Yesu arudi na mawingu. Tunafaa kusugua macho yetu ya kiroho, na tusiwe waathiriwa wa maneno yaliyojaa mambo ya kufurahisha masikio. Tunafaa kuwaza juu ya kazi ya Mungu ya matendo, na tunafaa kuangalia upande wa hakika wa Mungu. Msijisahau ama kupotelea ndotoni, mkitazamia daima ile siku ambayo Bwana Yesu atashuka kwa ghafla juu ya mawingu kuwachukua nyinyi ambao hamjawahi kumjua wala kumwona Yeye, na msiojua kutenda mapenzi Yake. Ni vyema kufikiri juu ya mambo ya kiutendaji!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Tanbihi:

a. Nakala halisi ya mwanzo inasema “na kwa.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 75)

Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 76)

Uaminifu wenu uko kwa maneno pekee, maarifa yenu ni ya kiakili tu na ya dhana, kazi yenu ni kwa sababu ya kupata baraka za mbinguni, na kwa hivyo imani yenu inafaa kuwa vipi? Hata leo, bado mnapuuza kila neno la ukweli. Hamjui Mungu ni nini, hamjui Kristo ni nini, hamjui jinsi ya kumcha Yehova, hamjui jinsi ya kuingia katika kazi ya Roho Mtakatifu, na hamjui jinsi ya kutofautisha kati ya kazi ya Mungu Mwenyewe na uongo wa mwanadamu. Unajua tu kukashifu neno lolote la ukweli linaloelezwa na Mungu lisilolingana na mawazo yako. Unyenyekevu wako uko wapi? Utiifu wako uko wapi? Uaminifu wako uko wapi? Tamaa yako ya kupata ukweli iko wapi? Uchaji Mungu wako uko wapi? Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua mambo bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe wenye kuchukulia mambo bila uzito na wenye msiofikiria katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Iliyotangulia: Hatua Tatu za Kazi

Inayofuata: Hukumu Katika Siku za Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp